Nimemharibia rafiki yangu ili niwe na mpenzi wake

youngsharo

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
2,491
Reaction score
500
Mu hali gani wanajukwaa?

Nahisi ukisoma title ya hii thread kidogo utastuka, lakin ukweli ni kwamba;Niliamua kumkandia [kumharibia] rafiki yangu kwa msichana wake ili mimi nimpate, na nilifanya ivo kwa sababu kwanza yule msichana alikuwa na upendo wa dhati lakini alipenda asipopendwa, alikuwa mtu wa kuomba msamaha hata kila anapobebeshwa lawama.

TATIZO yule rafiki yangu, hakuujua umuhimu wa mwanamke,alipenda sana kumlaumu hata kwa kosa dogo anaweza kumsimanga mpaka unamkuta anakosa raha,kwa kutambua anapendwa alimnyanyasa kwa kujua kwamba hawezi kumuacha.

Jambo ambalo lilinifanya nikawa naumia kumuona mtoto mzuri akiteswa ndipo nilipoamua kuingiza swaggz [kumtongoza] na kumshauri aachane na yule bwana wake.

Na mpaka sasa anaishi/tunaishi kwa raha kabisa, sema kuna tatizo ambalo limejitokeza ni kwamba yule rafiki yangu sasa hatuongei nae, ndo nawaza je nivunje penzi langu na huyu demu ili nirudishe urafiki na jamaa yangu au niendeleze mapenzi na msichana urafiki wetu na jamaa ufe?
 
soma kwanza shule bado kijana mdogo sana yani form three unakuja kuandika humu umepata mda saa ngapi?
nyambafuuu wew
 
Ninaamini ulifanya kosa kubwa sana katika hili jambo...kitendo chakuona kuwa jamaa anamuendesha vibaya huyo mwanamke wakat unatakiwa kuelewa kuwa katika maisha kila mtu ana jinsi yakuendesha mahusiano kulingana na mtazamo wa mtu aliyenaye anavyouona.....sasa wewe kujiona ni bingwa wakuanalyis mateso ya mwanamke bila kusikiliza upande wa pili ulichemka,na hakuna namna nyingine hapo zaid ya mtu kuelewa kuwa wewe ndio pengine ulikuwa unamjaza huyo mwanamke ujinga/kiburi......lakini cha zaidi kabisa ni uhakika usio na shaka kuwa huwez dumu na huyo mwanamke(njia uliyoingilia ndio utayotokea na pengine utapata maumivu makubwa zaid)....nakushauri endelea nae ili upate majibu kuwa ni je huyo mwanamke alikuwa anaonewa au ilikuwa sahihi...
 
Ulichokifanya sio cha kistaarabu.. Umeharibu na kuuvunja urafiki wa maana kwa sababu ya tamaa za mwili wako dhidi ya shemeji yako.. Ni rahisi kwa marafiki kuja kupatana baadae kama chanzo cha ugomvi wao ni kudhulumiana hela, kupigana, kutukanana na mengine yote but sio kwa kuchukuliana wanawake.. Ulitakiwa ulifahamu hili..
 
asante ndugu kwa ushauri
 
Ninaamini ulifanya kosa kubwa sana katika hili jambo...kitendo chakuona kuwa jamaa anamuendesha vibaya huyo mwanamke wakat unatakiwa kuelewa kuwa katika maisha kila mtu ana jinsi yakuendesha mahusiano kulingana na mtazamo wa mtu aliyenaye anavyouona.....sasa wewe kujiona ni bingwa wakuanalyis mateso ya mwanamke bila kusikiliza upande wa pili ulichemka,na hakuna namna nyingine hapo zaid ya mtu kuelewa kuwa wewe ndio pengine ulikuwa unamjaza huyo mwanamke ujinga/kiburi......lakini cha zaidi kabisa ni uhakika usio na shaka kuwa huwez dumu na huyo mwanamke(njia uliyoingilia ndio utayotokea na pengine utapata maumivu makubwa zaid)....nakushauri endelea nae ili upate majibu kuwa ni je huyo mwanamke alikuwa anaonewa au ilikuwa sahihi...

poa ngoja nicheki.
 
Back
Top Bottom