Nimemfumania mke wa rafiki yangu na ameniingizia zaidi ya 1,200,000/= kwa njia ya M-PESA

Kobongobongo usipooa / olewa kuna stigma ya uhuni.

I turn that stigma into glory.

Hapo nimekupata mkuu, kwa sababu uhuni ni neno pana na linajumuisha mambo mengi sana. Ndio maana nikasema wewe ni bora kuliko wahuni. Kwa maelezo yako haya nimekupata vizuri.
 
Tulioa tukisoma hii inaumiza sana ....mimi nashauri kama kweli unampenda rafiki yako mwambie ili umuepushe na magonjwa na huko kudhalilishwa na mke wako kiasi cha kusema mzazi mwenzie kuna uwezekano hata hao watoto si wake. Ili iwe fundisho kwa wengine ni heri kumwambia Rafiki yako kama una mpenda wanaosema ukae kimya hakika hawamtakii mema jamaa yako. Ipo siku atakulaumu sana maana dunia haina siri.
Mi mwenyewe kuna siku shemeji yangu niligundua ana mahusiano na jamaa mmoja hakika niliumia sana na shemeji yangu alijitahidi kunihadaa na kuniweka karibu lakini nilimwambia yote nitafanya siri si hili.Hakika nilimwambia na ulizuka ugomvi mkubwa sana na kupelekea ndoa kutaka kuvunjika lakini walielewana na kusameheana pamoja na yule jamaa pia tulimuweka kitimoto. Nae alikiri na kusema hatorudia.....Sasa siri si nzuri ili tutoe fundisho kwa wasaliti wa ndoa bora kuweka mambo wazi liwalo na liwe.....
 
Duu aisee una bahati ya kupata mradi isio na jasho. 1.2m kwa muda mfupi! Kama ni mm nikiishiwa pesa nastua mutu kwamba nipe hela la sivyo nasema!
 
Mara nyingi huwa nashindwa kuelewa misimamo ya sisi waswahili, nimeangalia karibu post zote hapa ushauri umekuwa jamaa apige kimya kwa rafiki yake wa karibu sana. Kisa hiki kinanikumbusha jamaa wawili ambao walitoka chuoni pamoja na kuanza kazi kituo kimoja, na baada ya miaka kadhaa hapo kazini mmoja wa hao jamaa wawili akapata mchumba hapo kazini na baadae wakaoana. Hata hivyo kumbe yule mke wa jamaa alikuwa anatembea na kibosile mmoja tokea wakiwa wachumba, lakini mwenzake hakumwambia kwa hoja kama hii kwamba ataingilia mambo ya watu, hivyo mpaka jamaa anaoa hakujua chochote. Baada ya ndoa kibosile aliendelea kugonga mke wa jamaa na watu wengine hapo kazini pia wakawa wanajua na kusikitika lakini hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kumtonya jamaa (hata kwa mafumbo). Mwishowe alijitikeza bwana mmoja courageous na kumueleza jamaa mbele ya kibosile kwamba kwa nini anafanya hivyo (ulitokea ugomvi mkubwa sana but ukweli ukajulikana) laikini hata hivyo tayari damage ilishakuwa kubwa sana kwani kati ya watoto 3 jamaa aliozaa na huyo mkewe 2 wakawa wa kibosile. Sasa utaona kwamba kama angetokea rafiki wa kweli (na si rafuki wa mashaka!!?) na kumweleza jamaa au kutafuta hata mtu mwingine wa kumweleza (kama yeye hawezi) basi pengine athari jamaa alizozipata zisingekuwa kubwa na kuharibu kabisa maisha ya mtu, pengine jamaa angevunja uchumba na kutafuta mwingine na maisha yangeenda tu.
 
Hebu acheni unafiki hasa nyie mlio kwenye ndoa. Hilo ni kosa kubwa kuliko yote kwenye ndoa. Na mnasahau mficha maradhi kifo humuumbua? Mbona hamuwatakii mema wanandoa hawa? Mbona mwajinafikisha kwa kutaka ndoa isivunjike wakati mnajua ukimwi ukiingia kwao ndoa itavunjwa na kifo cha aibu? Hivi binadamu tumejuwaje? Yaani unasema asiseme? Ili wakifa na ukimwi mfurahie chakula msibani na kuleta story kuwa "marehemu hakuwa mtulivu aliwahi hata kushikwa ugoni"? Ole wenu!

USHAURI:

Rudisha hizo pesa, mwambie shemeji yako huyo kuwa alilofanya ni kosa na hupendi aendelee, na usikubali kuwa msiri wake, tafuta siku mchukue rafiki yako mpeleke mahali patulivu muongee na umshauri kama mwanaume, mwambie ukweli kuwa awe mwangalifu aishi na mke wake vizuri ili mke ajirudi na aache tabia hiyo, mueleze ukweli kuwa umewahi kumuona kwa macho yako ila si lazima umtaje uliyemwona naye, then muache afuatilie mwenyewe athibitishe. Pia usimshauri ampige au amfukuze mke, ila afuatilie athibitishe kwanza kisha amuonye na kumwambia wazi kuwa anajua habari yote. Kisha waache waamue wenyewe.

Sipendi unafiki hapa, mwambie ukweli unusuru maisha yao sio kulinda ndia itakayoingiwa na ukimwi ukabaki unajilaumu kuwa ungesema ukweli, sema sasa!
 
Mnaomshauri jamaa arudishe bingo mnanikera sana!Ningekuwa mimi masimbi ningechukua,jamaa ningemuambia kila kitu halafu mtu aniguse aone!
 
.nachojiuliza hapa je ulifanikiwa kupata picha ya shem wako akiwa hayo maeneo, najua kwa kazi yenu mara nyingi ushahidi tena baada ya uchunguzi yakinifu ndo umpeleka mtu hukumuni, yani hapo we funga kinywa chako tena umwambie na huyo shem wako pamoja na mzazi mwenzie kwamba hukukutana nao sehemu yeyote, manake hapa unaweza kuwa wapanga namna gani ya kuwasilisha jambo kwa rafikiyo akati wenzio washapanga sinema nzima ambayo mwisho wa siku we ndo utakuwa mhalifu anayestahili adhabu kali.
 
piga kimya!ndio maana wanaume tumeumbwa na koromeo(hapa namaanisha hiyo kitu wazungu wanaita adam's apple),kazi yake ni kuzuia mwanaume kupayuka kila ajuacho na awazacho!narudia tena piga kimya mwanaume kusutwa haipendezi
Anaweza kumwambia rafiki yake, akimuuliza mkewe na akamjibu kuwa rafiki yake ni muongo, anamsingizia kwa kuwa alimtaka akamkataa, itakula kwake. Bora akae kimya tu
 
wake wengi wa maafande ni malaya kufa mtu kwa nini sababu ni kuwa wanaoa wanawake walioshindikana kwenye jamii
 
Wanawake!!!........ Wakat mwingne tunawaonea huruma tu. Hawa sio viumbe yaan ukimkuta mwanamke anagombana na nyoka bora umsaidie nyoka..... Hello chalii papaa/ au papaa chalii ww meza mdeki kamanda na hlo duhuri achana nalo hela ya dhambi hyo.


Wweeeee tafadhal usiniudhi,,,,hvi huyo mwanamke huko gest Alikuwa mwenyewe????au alienda na mwanamke mwezie?????kwan huyo mwanaume kama ni mume wa mtu?????achen kuwaona wanawake wachafu sana na nyie mwanaume wasafi,,, tena wakat mwingine nyie ndio mnamambo machafu kuliko wanawake.
 
Kwa nini?

Hujaona mtu hajaoa na anahonga kuanzia mume wa mtu mpaka mke, na mume mwenyewe anam pimp mke wake?

Kwa sababu kama unaogopa kuoa ili watu wasikuibie, kwa nini wewe uibe vya wengine? Kwani wao wana mioyo ya stainless steel?

Kama hutaki kuibiwa basi na wewe usiibe?

Unaweza?
 
Usipomwambia, mkewe ataenda kusema unamtongoza na kuvunja urafiki wako na wake na kukuaibisha.

Mwambie msumulie mwonyeshe pesa kwa simu yako zilizotumwa, ataona na jina la mtu aliekutumia then acha aamue yeye.

Au mwambie ake kimya achukue watoto afanye dna na hapo ajue cha kufanya kutokana na majibu. Sababu ni kwamba yeye atakuwa na proof toka kwako. Bila hivyo usipomwambia mke LAZIMA atakuwahi siku moja au kukutegeshea bila kujua na kukusema vibaya kuwa unamtaka etc.

Utaamua mwenyewe as huyo wakumuona live na pesa kakutumia unalo. Chagua rafiki au no urafiki.

Ikiwezekana mpe za kufanyia dna ya haraka haraka, na mkamywee pombe. Au mwambie mgawane etc si mko karibu kama ndugu au?
 
Usimwambie jamaa yako maana utavunja ndoa ya watu,huyo shemeji yako anaweza naye kukuzushia kwamba na wewe ulikuwa na mzigo mkagongana.
Unaweza kumuonya asiendelee na mchezo huo kama anaipenda ndoa yake maana mapenzi ni kikoozi,N siku nyingine anaweza asitunziwe siri,Jitahidi na wewe asije akakuhonga ngono.
Usiendelee kusimulia habari hii maana ukiisimulia huyo rafiki yako ndo atapata taarifa kwamba wewe unamzushia mkewe ili waachane,maana kama habari hizo ni za kweli ungemwambia mapema.
Warudishie fedha yao na waahidi kutomwambia jamaa yako na ulitimize hilo kwa vitendo.
Nyumba zinaficha siri nyingi,hata ya kwako unaweza ukakuta kuna mambo nyuma ya pazia ila watu wametunza na maisha yanakwenda.
 
Back
Top Bottom