Mbimbinho
JF-Expert Member
- Aug 1, 2009
- 8,328
- 7,804
Devi alichelewa kujiunga na chuo, hivyo alipofika akakuta kuna kitanda kimoja tu kimebaki katika chumba ambacho kulikuwa na mwanachuo ambae wenzake wote waligoma kulala nae chumba kimoja, maana alikuwa anakoroma mpaka kulala inakuwa haiwezekani. Devi akataarifiwa kuhusu tatizo hilo na kuambiwa kuwa wote waliojaribu kulala chumba kimoja na jamaa walikesha macho mpaka asubuhi kwa kero ya mkoromo wa jamaa. Devi akawaambia dawa amekwisha ipata. Kesho yake asubuhi, Devi kaamka fresh tayari kwa breakfast, wenzie wakamuuliza kama alilala vizuri,
DEVI; Nimelala fresh kabisa bila matatizo, si mnaniona?.
Jamaa wakamuuliza alitumia dawa gani?
DEVI: Nilipoingia jana chumbani nikamsalimia jamaa vizuri. Kisha nikamsifu kuwa ye mzuri sana. Na nilikuwa namkumbushia mara kwa mara kuwa sijawahi kuona mwanaume ana sura nzuri kama yeye, NAONA JAMAA AKAAMUA KUTOLALA