Nimekuta mahali ikijadiliwa, kauli ngumu na ndio ukweli wenyewe

Kosae1

JF-Expert Member
May 16, 2016
211
151
Hicho cheti ni karatasi Tu Chenye Nembo ya Taifa ili kukutambulisha kisheria kama wewe ni Mke wa Mtu. Shetani hakiogopi wala wanawake wa Nje hawakiogopi. Na hizo Pete ni kama urembo vidoleni mwako. Usidhani Kuwa zimemfunga Mume wako kufanya maamuzi magumu Ikiwa utamvuruga kichwa.

UKWELI ni kwamba sijawahi kuona Mwanaume anayeogopa Pete wala Cheti labda wapo ila Mimi sijawaona. Nakushauri mwanamke mwenzangu usikose adabu ukajivunia Pete na Cheti. Hata Kama Mtajenga Nyumba kwa majina yenu, Mwanaume atakapo kosa Amani anaweza kuacha gorofa akaenda kupanga Chumba kimoja uswahilini. Usidhani wote wanao paki magari hapo ofisini huku wameacha Nyumba zao Beach zenye Jacuzzi na kwenda kuoga na kopo uswahilini........ Sio kwamba wamefungwa na uchawi lahasha wamekimbia Makelele na ugomvi usio koma.

Mdomo wako unapaswa kuleta Faraja kwa Mumeo na Sio Maumivu ya kupasua Moyo wake. Sheria ya Maisha unavuna unachokipanda na Asilimia KUBWA ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo Yao na kutunga Sheria.. Akitoka huko Hata ukaja na Jeshi la malaika wa mbinguni na baragumuu hatobadilisha Maamuzi atakayo chukua.

USIJIBWETEKE. Nyumba inajengwa na Mwanamke Mwenye akili na inabomolewa na Mwanamke mpumbavu kwa mikono yake mwenyewe, yote yako mikononi mwako... Ukitakupendwa pendeka.. Ukitaka kukalia kaa la moto Jifanye pasua kichwa. Asili ya Mwanaume ni michezo ukianza kushindana naye kwa kibesi ligi haitaisha.. ILA UKIJISHUSHA NA KUKAA NAFASI YAKO UTADEKEZWA KAMA YAI.

Inawezekana kuna ukweli?
 
Sawa kabisa ila na wao wapunguze tamaa wakiona makalio makubwa tu balaa hata kama yupo na mkewe atageuza shingo utazan kibaka kaona pochi
 
Kwanini alaumiwe mwanamke wa nje? Kati ya yeye na huyo mwanaume ni nani amekula kiapo cha kuilinda ndoa yake? Ni kwanini macho yetu huyapeleka kwa huyu mwanamke na siyo mwanaume anayeshindwa kutumia akili zake?

Kuna kitu hakipo sawa kwenye jamii zetu.
 
naamini ni two way traffic ... si mimi najenga wewe uje kubomoa tu unabomoa tu... wanaume huchangia matatizo mengi katika ndoa japo jamii inawabeba kwa sababu tu pale mwanamke atakapo loose temper na kuonekana mbaya..

Ni kweli. Mwanaume akikuchoka anakufanyia kila aina ya visa. Mwanamke akiondoka anaonekana kavunja ndoa kwa upumbavu wake. Ila jamii huwa haijui kinachoendelea chumbani, wanawake tunateswa sana. Tunaumizwa kwa kauli zenye kujeruhi nafsi, wengne wanapigwa. Sasa ukisema uondoke ndo hapo unaitwa mwanamke mpumbavu umevunja nyumba kwa mikono yako mwenyewe. Linapokuja suala la ku fight for a relationship lisiwe la upande mmoja tu. Sote tunatakiwa kulinda mahusiano yaliyopo ili yasivunjike. Na ikitokea yamevunjika basi lawama zisielekezwe upande mmoja tu wa mwanamke. Wanaume nao wana mchango mkubwa sana ktk kuvunja mahusiano yawe ya ndoa ama mapenzi.
 
Kwanini alaumiwe mwanamke wa nje? Kati ya yeye na huyo mwanaume ni nani amekula kiapo cha kuilinda ndoa yake? Ni kwanini macho yetu huyapeleka kwa huyu mwanamke na siyo mwanaume anayeshindwa kutumia akili zake?

Kuna kitu hakipo sawa kwenye jamii zetu.
Nakubaliana na wewe ni kweli pande zote mbili zinahusika katika kuijenga nyumba/ndoa
 
Ni kweli. Mwanaume akikuchoka anakufanyia kila aina ya visa. Mwanamke akiondoka anaonekana kavunja ndoa kwa upumbavu wake. Ila jamii huwa haijui kinachoendelea chumbani, wanawake tunateswa sana. Tunaumizwa kwa kauli zenye kujeruhi nafsi, wengne wanapigwa. Sasa ukisema uondoke ndo hapo unaitwa mwanamke mpumbavu umevunja nyumba kwa mikono yako mwenyewe. Linapokuja suala la ku fight for a relationship lisiwe la upande mmoja tu. Sote tunatakiwa kulinda mahusiano yaliyopo ili yasivunjike. Na ikitokea yamevunjika basi lawama zisielekezwe upande mmoja tu wa mwanamke. Wanaume nao wana mchango mkubwa sana ktk kuvunja mahusiano yawe ya ndoa ama mapenzi.
kabisa lawama ni kwa wote .. wanawake tunabeba mengi mbaya zaidi anyekuhukumu ni mwanamke mwenzio
 
Back
Top Bottom