Usia wa baba kwa binti kabla ya harusi (nimeikopi sehemu iwafunze wadada)

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Nakuhusia Wewe mwana.....



Mwanangu nisikufiche watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuoneshana fahari, ukoo wa Mume Vs ukoo wa mke hawa kwenye Send-off na hawa wanajibu kwenye harusi.

Na ule usiku baada ya reception sijui ndio mnaita hivyo mnaingia kwenye gari kuelekea kwenye fungate. Hapo hata wanakamati huwa wanakimbiana ninyi mkishaondoka, kwani shughuli yao inakua imeishia pale. Hata wasimamizi watawasindikiza tu mpaka chumba mnacholala kisha wanawaacha hapo. Lakini kazi yako ndio inaanzia hapo.

Wewe humalizii siku ya harusi. Hapa ndio unaosha make up na kubandua hizo kope artificial na kucha na kuingia kwenye mapambano kupigania Ndoa yako. Ukweli ni kwamba wanaotarajia NDOA itakushinda ni wengi nikiwemo Mimi, na tunapokupigia simu kuuliza "Mnaendeleaje? " huwa tunatarajia jibu lolote kutoka kwako. Kwa sababu NDOA Inaanza baada ya harusi. Usiingie huko ndani kwenda kucheza.

Naomba nikwambie kauli ngumu na ndio ukweli kwa sababu nakupenda. Hicho cheti ni karatasi tu yenye nembo ya Taifa ili kukutambulisha kisheria kama mke wa Mtu. Shetani hakiogopi wala wanawake wa nje hawakiogopi. Na hizo Pete ni kama urembo vidoleni mwako, usidhani kuwa zimemfunga mume wako kufanya maamuzi magumu ikiwa utamvuruga kichwa.

Ukweli ni kwamba sijaona mwanaume anayeogopa cheti, labda wapo ila Mimi sijaona. Nakushauri binti yangu usikose adabu ukajivunia Pete na cheti. Hata kama mtajenga nyumba kwa majina yenu, mwanaume anapokosa amani anaweza kuacha ghorofa akaenda kupanga chumba kimoja uswahilini. Usidhani wote wanaopaki magari huko kigogo huku wameacha nyumba zao bahari beach, zenye Jacuzzi na wanaenda kuoga kwa ndoo na kopo uswahilini, sio wote wamefungwa na uchawi. Wapo wengi wamekimbia makelele na ugomvi usiokoma.

Mdomo wako unapaswa kuleta faraja kwa Mumeo na sio maumivu ya kupasua moyo wake. Sheria ya maisha ni kuvuna unachopanda na asilimia kubwa ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo yao na kutunga sheria, akitoka huko hata uje na jeshi la malaika wa mbinguni na baragumu hutarudisha nyuma maamuzi atakayofanya. Usijibweteke. Nyumba inajengwa na Mwanamke mwenye akili au kubomolewa na Mwanamke Mpumbavu. Yote yako mikononi mwako. Ukitaka kupendwa pendeka, ukitaka kukalia kaa la moto, jifanye pasua kichwa. Asili ya mwanaume ni games, ukianza kushindana naye na wewe unataka kibesi ligi haitaisha. Ila ukishuka na kukaa nafasi yako utadekezwa kama yai. Namalizia na hili binti yangu usimnange Mumeo, amekuamini mpaka kukufanya mkewe. Anashambuliwa na kila kitu kwenye maisha yake. Hebu msaidie nyumba yake iwe sehemu ya makimbilio. Usimfanye moyo kupasuka kila anapowaza kurudi nyumbani utajitengenezea tabu ambazo kuzituliza itakuwia vigumu.

Hii NDOA ni yenu, usitumie mfumo wa mashost zako kuendeshea nyumba yako, wanaume hawafanani. Ushauri mwingine uishie kwenye magroup usilete nyumbani. Nimekwambia haya ili NDOA yako ikadumu. Zaidi sana katika adhabu zote unazoweza kumpa Mumeo usimnyime tendo la Ndoa. Huo mwili ni mali yake. Hizo moods zako ziishie sebuleni, kule chumbani wasilisha rejesho la siku. Nimetumwa kwako asubuhi ya leo nikusaidie.
 

Attachments

  • Sincere-Father-12.jpg
    Sincere-Father-12.jpg
    41.9 KB · Views: 56
  • maxresdefault.jpg
    maxresdefault.jpg
    72.5 KB · Views: 112
Huu usia ukisomwa na wanawake wenye akili na kuyazingatia hayo na akipata mume anayejitambua; watadumu hadi Kristo atakaporudi.

Hapo kwenye paragraph ya kauli ngumu na hiyo paragraph inayofuata kama wanawake wangekuwa wanaelewa vichwa vya kiume vinavyowaza wasingekuwa wanachezea ndoa zao.
 
Sheria ya maisha ni kuvuna unachopanda na asilimia kubwa ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo yao na kutunga sheria, akitoka huko hata uje na jeshi la malaika wa mbinguni na baragumu hutarudisha nyuma maamuzi atakayofanya. Usijibweteke. Nyumba inajengwa na Mwanamke mwenye akili au kubomolewa na Mwanamke Mpumbavu. Yote yako mikononi mwako. Ukitaka kupendwa pendeka, ukitaka kukalia kaa la moto, jifanye pasua kichwa. Asili ya mwanaume ni games, ukianza kushindana naye na wewe unataka kibesi ligi haitaisha. Ila ukishuka na kukaa nafasi yako utadekezwa kama yai. Namalizia na hili binti yangu usimnange Mumeo, amekuamini mpaka kukufanya mkewe. Anashambuliwa na kila kitu kwenye maisha yake. Hebu msaidie nyumba yake iwe sehemu ya makimbilio. Usimfanye moyo kupasuka kila anapowaza kurudi nyumbani utajitengenezea tabu ambazo kuzituliza itakuwia vigumu.
Mafundisho kama haya yalipaswa kuwepo kwenye ratiba za 'kitchen party' huku mtoa somo akiwa mwanaume, maana ndiye anajua kwa uhalisia jinsi wanaume wanavyowaza, ili kunusuru ndoa tarajiwa..
 
Back
Top Bottom