Funzo tosha kwa maisha ya ndoa, hasa za vijana wa kileo (.com).

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Makala hii ameandika Gladys Chiduo kwenye FaceBook, yaliyomo ni funzo tosha kwa maisha ya ndoa, hasa za vijana wa kileo (.com).

"Mwanangu nisikufiche watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuoneshana fahari ukoo wa Mume vs wa Mke, hawa kwenye send-off na hawa wanajibu kwenye harusi.

Na ule usiku baada ya 'reception' sijui ndio mnaita hivyo mnaingia kwenye fungate. Hapo hata wanakamati huwa wanakimbiana, ninyi mkishaondoka, kwani shughuli yao inakua imeishia pale. Hata wasimamizi watawasindikiza tu mpaka chumba mnacholala kisha wanaacha hapo. Lakini kazi yako ndio inaanzia hapo. Wewe humalizii siku ya harusi. Hapa ndio unaosha 'make up' na kubandua hizo kope 'artificial' na kucha na kuingia kwenye mapambano, kupigania ndoa yako.

Ukweli ni kwamba wanaotarajia NDOA itakushinda ni wengi nikiwemo Mimi, na tunapokupigia simu kuuliza "Mnaendeleaje?" huwa tunatarajia jibu lolote kutoka kwako. Kwa sababu NDOA inaanza baada ya harusi. Usiingie huko ndani kwenda kucheza,

Naomba nikwambie kauli ngumu na ndio ukweli kwa sababu nakupenda. Hicho cheti ni karatasi tu yenye nembo ya Taifa ili kukutambulisha kisheria kama mke wa Mtu. Shetani hakiogopi wala wanawake wa nje hawakiogopi. Na hizo Pete ni kama urembo vidoleni mwako, usidhani kuwa zimemfunga mume wako kufanya maamuzi magumu ikiwa utamvuruga kichwa. Ukweli ni kwamba sijaona mwanaume anayeogopa cheti, labda wapo ila Mimi sijaona.

Nakushauri binti yangu usikose adabu ukajivunia Pete na Cheti. Hata kama mtajenga nyumba kwa majina yenu, mwanaume anapokosa amani anaweza kuacha ghorofa akaenda kupanga chumba kimoja uswahilini. Usidhani wote wanaopaki magari huko Kigogo huku wameacha nyumba zao bahari beach, zenye 'Jacuzzi' na wanaenda kuoga kwa ndoo na kopo uswahilini, sio wote wamefungwa na uchawi. Wapo wengi wamekimbia makelele na ugomvi usiokoma. Mdomo wako unapaswa kuleta faraja kwa mmeo na sio maumivu ya kupasua moyo wake.

Sheria ya maisha ni kuvuna unachopanda na asilimia kubwa ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo yao na kutunga sheria, akitoka huko hata uje na jeshi la malaika wa mbinguni na baragumu, hutarudisha nyuma maamuzi atakayofanya. Usijibweteke. Nyumba inajengwa na Mwanamke mwenye akili au kubomolewa na Mwanamke Mpumbavu. Yote yako mikononi mwako. Ukitaka kupendwa pendeka, ukitaka kukalia kaa la moto, jifanye pasua kichwa. Asili ya mwanaume ni 'games', ukianza kushindana naye na wewe unataka kibesi, ligi haitaisha. Ila ukishuka na kukaa nafasi yako, utadekezwa kama yai.

Namalizia na hili binti yangu, usimnange Mumeo, amekuamini mpaka kukufanya mkewe. Anashambuliwa na kila kitu kwenye maisha yake. Hebu msaidie, nyumba yake iwe sehemu ya makimbilio. Usimfanye moyo kupasuka kila anapowaza kurudi nyumbani, utajitengenezea taabu ambazo kuzituliza itakuwia vigumu. Hii NDOA ni yenu, usitumie mfumo wa 'mashost' zako kuendeshea nyumba yako, wanaume hawafanani. Ushauri mwingine uishie kwenye 'magroup' usilete nyumbani.

Nimekwambia haya ili NDOA yako ikadumu. Zaidi sana katika adhabu zote unazoweza kumpa Mumeo usimnyime tendo la ndoa. Huo mwili ni mali yake. Hizo 'moods' zako ziishie sebuleni, kule chumbani wasilisha rejesho la siku.

Nimetumwa kwako asubuhi ya leo nikusaidie,
MUNGU AKUBARIKI SANAAAA".

Dada, shangazi, mama na bibi zetu humu jamvini kujeni mwongeze neno, hasa 'single mothers' mtakuwa na uzoefu wa yaliyotamkwa na mwenzenu. Miss Chagga, Miss Natafuta, Heaven Sent, nk uwanja wenu.
 
Mwanamke ( Mke ), anatakiwa kufundishwa na Mume peke yake, Mke akifundishwa na mtu mwingine ... kutakuja kua na mushkeli tu ndani ya mjengo. Mwanaume timiza wajibu wako kumfundisha mkeo, ukifundishiwa utalia au kuona hana adabu ... Mtoto umleayo ndivyo akuavyo.
sasa mkuu mbona wana kitchen party zao ?
 
Kitchen part, ni sejemu ndogo sana ... ni training ya mda mfupi sana.

Nikupe mfano.
Mimi ni Ninja alafu nakaa na mtu X, nitamfundisha ya uninja ni ninja na lifeyfe style langu nae pia kuna vitu atanifundisha.

Akitoka kwangu akienda kwa Ethical, ataenda na tabia za huku kwangu baadhi, na itamchukua mda kuchange kabisa na hadi awe na nia ya dhati. Utata unakuja Je? Ethical ni Ninja .... Jibu ni hapana ... hakuna chemistry,, Ndio maana hata nw days wadada hawa ridhiki, alipotoka alikua nakula vi 6, alafu anapoe enda anakula vi 2 ... Hakui hardcore sex anakuta soft sex .... duh!
Tabia zao zinabadilika sana nowadays mkuu sijui kwa nini
 
Mwanamke ( Mke ), anatakiwa kufundishwa na Mume peke yake, Mke akifundishwa na mtu mwingine ... kutakuja kua na mushkeli tu ndani ya mjengo. Mwanaume timiza wajibu wako kumfundisha mkeo, ukifundishiwa utalia au kuona hana adabu ... Mtoto umleayo ndivyo akuavyo.
Sasa mkuu naona umekuja pindua bandiko
 
Kwa nyogeza tu, mwanamke anaweza kuigeuza ndoa ikawa uwanja wa vita. Mwanamziki Tommy Lee alisema "NDOA ni uwanja wa vita ambao mtu hulala na adui".

Baraka Obama yeye alisema "A good wife always forgives her husband when she's wrong"
 
Ameandika vizuri ila pia aandike na yale yanayokimbiza wanawake nje ya ndoa au kuwafanya wabadilike na kuwa watu ambao hata wenyewe wanaume hawawafahamu wanadai wameolewa wakabadilika.
Maisha ya ndoa huanza baada ya harusi kwa wote mume na mke na ni wajibu wao wote kutunza ndoa na kuifanya idumu.
 
Ameandika vizuri ila pia aandike na yale yanayokimbiza wanawake nje ya ndoa au kuwafanya wabadilike na kuwa watu ambao hata wenyewe wanaume hawawafahamu wanadai wameolewa wakabadilika.
Maisha ya ndoa huanza baada ya harusi kwa wote mume na mke na ni wajibu wao wote kutunza ndoa na kuifanya idumu.
huo ni ushauri wake kwa wanawake unaweza andika wako kwa wanaume...
 
Waache kuwatisha wakina dada yeye yote hayo experience kaipatia wapi, Au anadhani kuishi na bwana heri ni sawa na bwana jumah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom