Nimekusamehe lakini sitasahau

Nimekusamehe lakini sitasahau

Kusamehe ni somo kubwa sana na inabidi ujifunze kusamehe. Kusamehe kunaendana na kusahau kwa sababu msamaha wa kweli ni kuyaacha yaliyopita na kuanza upya ukiwa mweupe (clean) moyoni. Ukikumbuka makosa uliyofanyiwa utaumia na hapo utamchukia aliyekukosea na msamaha utakuwa haujafanya kazi.

Binafsi kuna mtu alinikosea sana na nilipitia situation kama yako ila kuna vitabu nilivisoma na kusikiliza kama why forgive (audio book), when forgiveness seems impossible ( discovery series) n.k ambavyo vilinisaidia kusamehe na kusahau.

Kusamehe kunaendana na kusahau na kusamehe bila kusahau basi si msamaha wa kweli kwa kuwa bado utateseka na kosa ulilofanyiwa na mwisho wake ni chuki kwa aliyetenda kosa.

please nisaidie kujua vitabu ulivyosoma coz naisi huyu mtu sikataa nimsamehe.recently nimekuwa nakutana sana na izi thread za misamaha nimekuwa nazisoma na kumwomba Mungu anisaidie kuondoa chuki/hasira nlionayo kwa huyu mtu.Please nisaidie.......!!!!!
 
ni kumuomba Mungu akusaidie uachilie, once you really forgive with Gods help, u just forget it, inakuwa nyuma kabisa ya akili yako, yani hata ukijaribu kukumbuka it just doesnt work, niamini!unaweza kusamehe na kusahau, naongea from experience...unaweza kumbuka ila haikupi tatizo, haikuletei hasira...yani ni kama kitu kingine tu kisicho na maana ambacho kitakupotezea mda ukikipa mda

Kuna kipindi i tried very hard to forgv n forget na kuomba pia Mungu nlifanikiwa kwa kiasi kikubwa nkaanza kusahau na hata nkikukumbuka nakuwa siskii hasira cha ajabu mtu aliyeniumiza akarudisha mawasiliano na mimi yaani hasira/chuki/maumivu yameenza upya namchukia sana.
 
Nimetumia logic ya kidini, Mungu anasema anasamehe na kusahau alafu anatutaka sasa tufanye hivyo. Angekua anasamehe na hasahau hakuna maana ya kusamehe.

Jifunzeni kutoka kwangu maana mimi ni mnyenyekevu na mpole, nadhani umenipata.

Kusamehe na kutosahau vina uhusiano gani?
Kwani kusamehe ni kujikumbusha unachokikumbuka?

Samehe 7x70 maana yake ni kusahau mara 490? utahesabu vipi kma umesahau...Baada ya pale usisamehe tena?
Maana halisi ni usamehe kadri uwezavyo. Mara ngapi wewe binafsi umewakumbusha watu uliowasamehe! Au wewe saint?

Kusamehe kutabaki kuwa kusamehe tu, na kusahau ni kihusishi cha sifa kisichoondoa au kuongeza maana ya kusamehe, ukisamehe sio lazima usahau.. kibinadamu kila jambo lina guide line ukivuka mstari hatua zingine zinafuata. Ntakupa mfano kunavitu havisameheki kisheria na kibinadamu mfn ubakaji..nk aliebakwa hata kama alikusamehe hatakusahau.
 
Kuna kipindi i tried very hard to forgv n forget na kuomba pia Mungu nlifanikiwa kwa kiasi kikubwa nkaanza kusahau na hata nkikukumbuka nakuwa siskii hasira cha ajabu mtu aliyeniumiza akarudisha mawasiliano na mimi yaani hasira/chuki/maumivu yameenza upya namchukia sana.

Kusamehe ni kupuuza kile kilichotendeka kukuudhi, so puuza tu ni njia sahihi ya kusamehe.
 
Kuna kipindi i tried very hard to forgv n forget na kuomba pia Mungu nlifanikiwa kwa kiasi kikubwa nkaanza kusahau na hata nkikukumbuka nakuwa siskii hasira cha ajabu mtu aliyeniumiza akarudisha mawasiliano na mimi yaani hasira/chuki/maumivu yameenza upya namchukia sana.

endelea kusali, there is a reason kwa nini amerudi...unajua usipo samehe na wewe hausamehewi so unaweza ukawa unamuomba Mungu kitu na hauoni results, unabaki stuck hapo hapo...endelea kusali
 
Taahira tu na mwenye mtindio wa ubongo ndio anaweza kusamehe na asisahau. Mwenye akili timamu husamehe na kusahau au kutokusamehe na kutokusahau. Umesamehe alafu husahau ya nini umesamehe.

Hilo neno tunasamehe hatusahau wewe na nani? Kama wewe unasamehe ila husahau sema wewe sio kujumlisha watu wote. Wengine tuna akili timamu na hatuma matatizo ya mtindio wa ubongo.
we umewahi kusamehe na kusahau?
 
the weak can never forgive, forgiveness is the attribute of the strong.
 
Kusahau ni jambo jingine ili mkuu,na cdhani kama kuna anayesahau hasa kwa jambo kubwa.

Tofauti yetu kubwa ni moja tu,

*Wapo ambao wakisamehe jambo ambalo liliwaumiza sana basi ikitokea umemkwaza tena ujue atakumbushia (ingawa ni kweli alikusamehe)

*Pia wapo ambao wakisamehe jambo zito na ikatokea ukawakwaza tena kwa jambo jingine zito au jepesi basi yeye hatokumbushia (ingawa moyoni anakuwa kalikumbuka tukio la zamani na linamuumiza)
 
Hautaweza kusahau kama haujajisamehe wewe binafsi. Kuna kusamehe na kujisamehe.
 
kusahau ni tofauti na kusamehe kuna matukio mtuu unafanya utotoni mazuri au ma baya. ila unakua unayakumbuka ata sherehe au msiba kuna ambazo utakua unakumbuka sana tu lakini unapo kuja kwenye makosa na kusamehana mtu umsamehe na usahau alilo kutendea pengine ulinganishe kosa ndo unaeza msahau kama kosa ni dogo unasahau tu ila ni kubwa sana let say alikukata kidole cha mguu. ata usamehe vip. bado kusahau ni ndoto. na kubwa ya yote when we come to mapenzi..
mapenzi ndo yana kua na michezo iyo sugu. kusamehe lakini sikusahau uko ndo kumebobea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom