Msamaha jambo muhimu kwenye mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msamaha jambo muhimu kwenye mahusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Mar 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  KWA MAANA WOTE WAMEFANYA DHAMBI NA KUPUNGIKIWA NA UTUKUFU WA MUNGU!!!AKUNA ALIE PERFECT MPE NAFASI MWENZI WAKO AKIKOSEA

  KUINGIA kwenye ndoa ni jambo zuri, lakini unatakiwa kuwa makini na aina ya mtu ambaye unamchagua ili awe wako, kwa sababu si kila mtu anafaa.

  Kitaalam, wapo wanawake au wanaume ambao hawafai kuwa nawe, labda ni kwa sababu ya tabia zao nk, akili zao, elimu zao na hata utajiri au umaskini wao.

  Kauli zenu zinakwenda sawa? Na kama sivyo, mnafanya jitihada gani kuweka mambo sawa? Hili ni jambo la msingi sana kulitafakari, kinyume na hivyo, ni vigumu kuwa na maendeleo mazuri.

  Haijalishi mno katika uhusiano gani, ni jambo la msingi sana kutafakari kwa makini aina ya uhusiano wenu na kuangalia ni papi kuna kasoro, kisha anzeni kuchukua hatua kurekebisha.

  Unapokuwa na mwenzi wako na ikatokea kasoro, ni jambo la msingi sana kusameheana, hasa kama anaonekana ni mtu mwenye kuwa na mwelekeo mzuri baadaye. Kusamehe ni muhimu, lakini ni muhimu zaidi kuangalia kama kweli mtu huyu anafaa au ameharibika kabisa.

  Kuna aina ya watu, kasoro zao ni kubwa, kiasi kwamba ni kweli hata kama unaamua kuwasamehe, ni vizuri kutofikiria kuwa nao, kwa sababu tu labda ya staili zao za maisha yasiyovutia nk.

  Ikiwa mmekwazana, mtu wako anaonekana mwenye mwelekeo wa kubadilika kitabia, jitahidi kujifunza namna ya kumsamehe.

  Siku zote katika maisha waza mbinu za kuwa na maisha bora, acha kuendekeza tabia ya kuendekeza tabia ambazo si za msingi katika maisha yako.

  Unapojenga tabia ya kusamehe, ndio unasaidia kuimarisha uhusiano wako. Unaposema nimesamehe, iwe ni kweli umesamehe, siku si nyingi unarudia kauli ambazo tayari ulishasema kuwa nimesamehe.

  Yale yamepita, anza mapya. Kwa maneno mengine ni kuwa unaposamehe, samehe kweli, angalia mbele, wala usirudie tena maneno ya zamani.

  Unaposamehe, usisamehe kwa unafiki. Maana kuna wengine wanasamehe si kwa ajili yako bali kwa ajili yake aliyekukosea na wakati
  mwingine ni kwa sababu wanataka uthibitisho kwanza kuwa kosa hilo halitarudiwa na ndipo usamehe.

  Ni lugha ya kawaida kusikia mtu akisema 'nasamehe lakini sitasahau'. Katika maisha unatakiwa usamehe na kusahau.

  Mtu akikufanyia ubaya, na kama unaona ni mtu ambaye haonyeshi dalili ya kubadilika, na kama yale anayofanya ni mabaya sana, kila mtu aanze upya kwa heshima.

  Msamaha wa kweli unadhihirisha upendo ulio ndani ya mtu. Pasipokuwa na upendo, kusameheana hakupo. Palipo na upendo wa kinafiki, pia pana kusameheana kinafiki.


  Kusameheana hakuonekani siku hizi, katika ndoa, kati ya ndugu, kati ya majirani, kati ya watu, KWA SABABU UPENDO WA WENGI
  UMEKWISHA POA!

  Wengine wapo kwenye uhusiano, lakini chuki imejaa, ndoa zinaharibika kwa sababu ya chuki, undugu unakufa kwa sababu ya chuki. Baadhi ya wale wenye hali hii ni wanaosema wanaishi kwa kumtegemea Mungu.

  NDIO UKWELI WENYEWE; Upendo wa kweli huvumilia, hufadhili, upendo hauoni uchungu, hauhesabu Masaya, haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli huvumilia yote, huamini yote, hustahimili yote. Je, wewe ukoje? Ukiwa kinyume na hivi, jua kuwa upendo wako haupo sawa. Upendo wa kweli hauendekezi unafiki.

  Mtu mwenye upendo wa kweli hana chuki za mara kwa mara. Upendo unamuondolea mtu chuki, uchoyo na ubinafsi.

  Kama ulikuwa husalimiani na adui yako, chukua hatua ya upendo, msalimie na ikibidi mtembelee nyumbani mwake. Kula pamoja naye, furahi pamoja naye, na omba pamoja naye.

  Kuna watu wengine hawasalimiani wala kutembeleana na wazazi wao, au baba au mama, kwa sababu ya mambo yaliyofanyika zamani ambayo hawakuyapenda. Anza kujenga nao uhusiano mzuri, ikiwemo kuwaandikia barua nk.

  "Je! mbona kila mkikosana unakumbusha makosa ya nyuma?" Ikiwa wewe uko hivi, jua kuwa unakosea. Maisha yanayofaa ni kusamehe moja kwa moja. Kusamehe na kusahau ni kitendo cha ambacho ni budi kionekane kwa
  njia ya matendo ya mtu.

  Ukiishaamua kumsamehe mtu hakikisha hulisemi tena jambo hilo katika kinywa chako. Kumbuka kinywa kinanena yaujazayo moyo.

  Katika maisha ukipingana na mabaya na kusaka mazuri hakika utafanikiwa. Je, wewe unayojenga kila siku ni mazuri au mabaya?

  JIHADHARI NA HASIRA: Hasira ilivyofananishwa na uchawi, uasherati, uadui, na mambo mengine kama hayo ambayo yanamzuia mtu kushindwa kuishi kwa raha.

  Ni kweli wakati mwingine unaweza kujikuta mwenye hasira, lakini ni jambo la msingi sana kuwa mwangalifu, kwa sababu hasira huchangia mtu kufa haraka, kwa maana kuwa mtu anapokuwa na hali hiyo, mzunguko wa damu yake, huwa tofauti, hasa kuwa kasi zaidi, na hapo huwa ni mwanzo wa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo.

  Kukasirika ni jambo la hatari; Ndio unaweza kuona baadhi ya watu wanapokasirika juu ya jambo fulani, wanaugua vichwa, vidonda vya
  tumbo, kifua, moyo, damu kwenda mbio, homa, na magonjwa mengine. Tatizo si ugonjwa hapo.Tatizo ni hasira! Yanini ukae na hasira kifuani kwako?

  Usiwe mwepesi kumwambia mtu maudhi, wala usipende kusengenya, vitendo kama hivi hurudisha nyuma maendeleo.

  Kuna wengine wana hasira na wake au waume zao, kwa mfano utakuta mwanamke analalamika �Mume wangu huwa hanipi fedha ya kununulia chumvi nyumbani��kwa hiyo ukikasirika ndio fedha ya kununulia chumvi inapatikana?

  Dismas Lyassa ni mtaalam wa uhusiano aliyesajiliwa na serikali kutoa ushauri (social Welfare Counselor), anapatikana kwa simu 0754 498972, www.DismasLyassa.com
   
 2. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,018
  Trophy Points: 280
  Na msamaha wa kweli ndio tatizo kwa binadamu siku zote na hapo ndio kipimo cha imani yake
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  naungana nanyi na nishwahi kusema Msamaha ni dawa kwa aliyejeruhiwa; mnaweza kutusaidia hatua za kuchukua ili misamha inayotolewa isiew feki; kwa faida ya wasikilizaji ooops wana JF
   
 4. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,018
  Trophy Points: 280
  Kwanza uwe unaifahamu sala ya BWANA kama ni Mkristo hasa pale "utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe wanaotukosea huku duniani"

  Na husiwe mtu wa kukumbushia makosa yaliyopita utaweza kusamehe kwa ukweli
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Na kama si mkristo?
   
Loading...