Nimekumbwa na tatizo la hair loss na ninavyoona sio hair loss ya kawaida, ni upara kabisa

Super Charged

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
926
1,640
Habari Wana Jamvi,

Wakubwa Zangu Shikamoo.

Natumaini Mungu Anabariki kwa Kila Changamoto mpya mnazopitia
Naombeni Ushauri, Maoni, Kujuzwa kuhusu Hali Nayopitia kwa sasa

Nimekumbwa na Tatizo La Hair Loss Na ninavoona sio hair loss ya Kawaida Ni upara kabisa.

Maana Nywele za Mbele Zinaisha, Zinakuwa Dhaifu(Kupoteza density), Pembeni Kunajichonga Kwa sababu Ya Nywele Kuisha. Mbaya Zaidi Niko below 25, Baba yangu Ana Upara lakini Umeanza Akiwa 35+

Je, kuna Dawa Yoyote za kuondoa Upara au Kuchelewesha Hilo. Je, vipi kuhusu Dawa?

Kuna dawa Nazoziona zinatangwazwa Instagram N.k kuna Mtu alishajaribu au anajua lolote?

Nimeskia Pia Kuhusu Minoxidil Je Kuna Yoyote Anaifahamu? inasaidia? Mbali na Hiyo Kuna Dawa yoyote au Niia Yoyote ya asili au Mitishamba.

Naomba Maoni/ushauri wako juu ya chochote unachokijua

NB: Ni muhimu kupambana Na Tatizo kabla ya kukubaliana Nalo.

Natanguliza Shukrani.
 
hakuna dawa ya upara, usijepigwa
dawa yake ni kunyoa upara, mwendo wa dongo kama mie

nimenunua mashine ya kunyolea, kila siku asubuhi ni mwendo wa dongo
mda huu naiwasha hapa, naiwekea oil napiga dongo
Asante mkuu Ila Kuna watu walirudisha Nywele zao Kama akina Wayne rooney. Pia mbali na Hivo dawa zipo nyingi zinatangazwa Lisemwalo Lipo.
 
Asante mkuu Ila Kuna watu walirudisha Nywele zao Kama akina Wayne rooney.
Pia mbali na Hivo dawa zipo nyingi zinatangazwa Lisemwalo Lipo
Kwanza we ni me au ke?
Kama wewe ni me na kama uko below 25, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuwa na hormonal imbalances kwenye mwili namaanisha dihydrotestosterone Iko kwa kiwango cha juu kuliko testosterone . Je unakula kitunguu maji Kwa wingi sana?

Dihydrotestosterone ikiwa kwa kiwango cha juu inaleta hair loss kwa haraka kwa mwanaume.
Ila tukidraw hypothesis yetu nyingine kama Mzee wako alianza kupata upara akiwa na 35 kabla ya 40-45 basi itakuwa tu ni genetics.
 
hakuna dawa ya upara, usijepigwa
dawa yake ni kunyoa upara, mwendo wa dongo kama mie

nimenunua mashine ya kunyolea, kila siku asubuhi ni mwendo wa dongo
mda huu naiwasha hapa, naiwekea oil napiga dongo
Kama hawezi kunyoa kila siku anaziacha tu zitajiseti zenyewe kama mzee Wasira huwa hana shida

images (25).jpeg
 
Habari Wana Jamvi,
Wakubwa Zangu Shikamoo.
Natumaini Mungu Anabariki kwa Kila Changamoto mpya mnazopitia
Naombeni Ushauri,Maoni,Kujuzwa kuhusu Hali Nayopitia kwa sasa

Nimekumbwa na Tatizo La Hair Loss Na ninavoona sio hair loss ya Kawaida Ni upara kabisa.
Maana Nywele za Mbele Zinaisha,Zinakuwa Dhaifu(Kupoteza density),Pembeni Kunajichonga Kwa sababu Ya Nywele Kuisha
Mbaya Zaidi Niko below 25,
Baba yangu Ana Upara lakini Umeanza Akiwa 35+
Je kuna Dawa Yoyote za kuondoa Upara au Kuchelewesha Hilo
Je vipi kuhusu Dawa?
Kuna dawa Nazoziona zinatangwazwa Instagram N.k kuna Mtu alishajaribu au anajua lolote?
Nimeskia Pia Kuhusu Minoxidil Je Kuna Yoyote Anaifahamu? inasaidia?
Mbali na Hiyo Kuna Dawa yoyote au Niia Yoyote ya asili au Mitishamba

Naomba Maoni/ushauri wako juu ya chochote unachokijua

Nb:Ni muhimu kupambana Na Tatizo kabla ya kukubaliana Nalo.

Natanguliza Shukrani
Dawa ya uhakika ni kupandikiza na ni very simple procedure muone dr octay yavuzy ana clinic dar ila ni gharama mil 3 ,kuhusu minoxidil sikushauri ufanisi wake ni mdogo na unatakiwa unywe kila siku
 
Asilimia kubwa ya wanaosema wana dawa ya kuotesha nywele ni waongo na hasa kama ni vipara vya kurithi ni issue kubwa na gharama pia.

Ukizingatia umri wako kusema kuweka nywele bandia ni utumwa ingawa kuna saloon sinza wanafanya hivyo.

Kwa upande wangu ushauri ambao naweza kukupa ni kunyoa kipara na ikiwezekana kuwa na machine yako mwenyewe kama mdau mmoja alivyoshauri.
 
Asiweke nywele bandia kama ana uwezo aende kwa dr octay yavuzy apandikize
 
Back
Top Bottom