kufuli zile VIP zinazopanda kifuani ..
Umitashumta moja hivi hii kitu ilisababisha nishike nafasi ya pili pamoja na uchovu wangu, hahahaha!
Duu mkuu wangu umenikumbusha mbali kweli! enzi za suruali za mchelemchele, vitu - moka (mocasin), Kulikuwa na sabuni za Hisoap/Hiwhite / Hiblue na premium za kiwanda fulani kule Mbeya, sijui kiliishia wapi kiwanda kile? raba za DH (Double Happiness),vibati au ngozi (jeans) codrai , travolta we acha tu.Enzi zile mambo ya kujitupia kwa "Juliana", BioAct, BenQ, NINO, TOMATO (kwa wale wa QUarters kama line polisi au JWTZ, Waalimu nk ni nunulie shati kama lako ukienda mjini..) ...imenikumbusha mafuta ya kupaka SHANTI, "RAYS", SNOW CREAM,YORANDA, kuchoma nyewele kwa kigae cha chungu (kwa kina dada), ambo ya Rangi mbili (Tetracycline).Viatu vya chacha, suzana, bora nk (wapo tuliovaa "Mwaka wa Mtoto")...kufuli acha zile VIP zinazopanda kifuani ikikatika kiungo, zilikuwa boxers zenyebango 007 au chapa mamba..saluni chini ya mwembe..fundi cherehani Mzaire..
Thanks Mzee RUKSA..
Duu mkuu wangu unikumbusha mbali kweli! enzi za suruali za mchelemchele, vitu - moka (mocasin), Kulikuwa na sabuni za Hisoap/Hiwhite / Hiblue na premium za kiwanda fulani kule Mbeya, sijui kiliishia wapi kiwanda kile? raba za DH (Double Happiness),vibati au ngozi (jeans) codrai , travolta we acha tu.
Hii teknolojia ilikuwa nishai sana, yaani mtu anacheza zake mpira ghafla kitu inatokeza shingoni,,shabash