manning
JF-Expert Member
- Apr 1, 2013
- 5,093
- 11,948
Nakumbuka mara baada ya kumwapisha anaeyeitwa Prof Muhongo na Katibu wake mkuu Maswi walitamba sana kwamba KWA SASA MGAO UTAKUWA NI HISTORIA. Kwa sasa niko hapa Mwanza kikazi. Tangu nifike hapa Mwanza ni karibu masaa 70 lakini sijauona umeme wa TANESCO hapa tangu nifike hapa . Niliporejea Tangazo la Tanesco la mgao wala Mwanza haimo lakini hali ndo hii na hakuna taarifa nyingine zaidi ya tangazo lao katika magazeti. Tahadhari kwa wanaozaa bado muwe waangalifu kuchagulia watoto wenu majina , unaweza kumpa mototo jina likaja kuendena na matendo yake.