Nimekubali kweli Afrika ni Bara giza

Nimekubali kweli Afrika ni Bara giza

ARDHI, WATU, SIASA SAFI na UONGOZI BORA..kwangu bado ninaamni kuwa hayo ni mambo mtambuka katika maendeleo ya nchi. Je, kwa kiasi gani tunajipambanua kwayo?
 
Bara la watoto yatima ili.Mungu alijua akili zetu ndo maana akatuweka kwenye bara lenye kila kitu ili angalau tujikomboe ila akil sasa ndo kaputii.
 
Bara la watoto yatima ili.Mungu alijua akili zetu ndo maana akatuweka kwenye bara lenye kila kitu ili angalau tujikomboe ila akil sasa ndo kaputii.
hadi sasa dunia ilipofikia mwafrika ndio mwanadamu pekee aliyebaki na akili au uwezo mkubwa kichwani maana haujatumika. Ndio maana naomba angalau waje wazungu watuboost maana peke yetu tumeshindwa bila ushawishi wa nje...
 
Mzee mmoja alisema Waafrika tuna FRESH and UNUSED BRAIN. Siku tukisema tubadilishane BONGO wazungu watumie hizi zetu, dunia wanaweza kuihamishia MARS.

GIZA LA NJAA
Kwa mshtuko kabisa, 60% ya ardhi ifaayo kwa kilimo duniani, inapatikana afrika.
60% ya wakazi wa afrika ni vijana miaka chini ya 25 wenye nguvu mpya,akili safi
na uwezo lakini mamillioni ya watu
wanakwenda vitandani usiku kulala bila kula.
Nchi nyingi za afrika zinatumia mabillioni ya dola kuagiza vyakula nje.
Hii inaacha mwanya mkubwa kwa mzungu/mchina kuja kuwa billionea kwa fursa hii.

GIZA LA AJIRA
Afrika tuna uhaba wa ajira, kuna uhaba mwingine unasababishwa na kutokuwepo na
taarifa kati ya muajiri na muajiriwa. ndio maana ukienda uarabuni wanasema utakuta
waasia kibao wakifanya kila kazi huku waafrika wakionekana kwa kusuasua.
Pili ni Kutokuajirika. Kuna ombwe la maarifa kati ya muajiriwa na kazi anayotaka kufanya au
aliyesomea. Hii inatoa fursa kwa Mzungu Kuziba hilo ombwe huku akijiingizia mamilioni.

GIZA LA AFYA na MAGONJWA
Afrika inachukua 15% ya watu wote duniani, lakni 24% ya magonjwa duniani yanapatikana afrika.
HAYA MATATIZO YAMEIBUA Uhitaji mkubwa sana na walazima wa dawa afrika kuliko sehemu nyingine.
Mzungu/Mchina hapa anaweza kuwekeza na kuwa billionea kwa muda mfupi.

GIZA LA UMEME
Ukienda NASA ukapewa lift kwenye ile rocket inayoenda angani, ikifika usiku iangalie dunia kupitia upande wa afrika.
Utakuta ni kama shimbo kubwa jeusi lenye giza la kutisha.
Hivi ulikuwa unajua nchi zote 48% za kusini mwa jangwa la sahara, zenye wakazi takribani Millioni 750 zinazalisha umeme
sawa na wa nchi ya SPAIN yenye wakazi Millioni 50 idadi karibu sawa na watanzania.
Mzungu/Mchina njoo Afrika uwe billionea kwa kutuwashia taa akilini na nje ya mwili.
Mwanamuziki AKON ni miongoni kwa watu weusi wanaojikongoja kutengeneza mabillioni kutatua hili giza kwa kusambaza SOlar.

GIZA LA MAJI
Kwa maji haya matamu,masafi na mazuri yaliyoko afrika ni dhahiri Muda sio mrefu wazungu,waarabu na waasia wataanza kuja
Kuteka maji afrika. Kuna mamillioni ya wanaafrika wanakufa kwa kiu na kuhara kwa
kukosa maji safi katikati ya chanzo cha maji safi.
Mzungu/Mchina njoo utuokoe safari hii usititawale washa taa kwenye bongo zetu. Haya maombi Tungemuomba Mungu
Lakini ni ya kiwango cha chini kiasi kwamba Mungu tutamsumbua bure.
Mzungu/Mchina njoo basi utuokoe wanadamu wenzako. Safari hii ukija Usitupige fimbo,
usituibie, Tutakupa pesa wenyewe huku ukitatua matatizo yetu.
Tusaidieni wanadamu wenzenu
Hili giza lililotapakaa UBONGONI bila nyie linazidi kutapakaa kwenye afya,Umeme,Maji,mahusiano kila kona.
Wahini haraka jamani mtusaidie safari hii msitufitini, Washeni taa kwenye bongo zetu na nje ya bongo kisha mrudi kwenu.

Wazungu/Wachina tafadharini sana, chondechonde tusaidieniii wote ni wanadamu...
Nineipenda hii you made my day. Kwani hizi fursa tunaweza tumia wenyewe badala ya wageni
 
Baada ya kuona hayo matatizo umeamua kufanya nini kutatua? Badala ya kutumia bongo kutatua hutaki kabisa kufikiri unaamua kukimbilia nje waje kusaidia. Huo ndo uafrika wenyewe mnajua kulalamika tu ila hamtaki kufikiria njia za kutatua
nimeandika kutufikirisha sisi sote kila mmoja kwa angle yake, hayana uhusiano na maisha yangu binafsi.
ndio maana ya forum, mahali ambapo watu wanajadili IDEAS na sio maisha binafsi ya mtu mkuu. Mimi ni mwafrika, na nakubali ni Mjinga, na asilimia karibu Tisini na kitu ya Ubongo wangu haujatumika vilivyo, mimi na wewe na wengine wengi tuko katika tafakari ya afrika yetu. Maamuzi kila mtu atajua na maisha yake, ila kianzio ni Utambuzi...
 
Umesema ukiomba lift. Wewe ulishapewa lift mara ngapi kwenye hicho chombo cha wazungu na kuliona hilo shimo lililoko Africa
 
Hivi binadamu wote kama vile, waafrika, wazungu, waarabu, wa Asia n.k waliumbwa na Mungu kama binadamu wote au kuna ambaye walikuwa kwenye kikundi cha 'let there be...' nawakawepo ila wakawa wamefanana na binadamu sana wakaunganishwa humo by mistake. sbb hapa afrika sijui tutakufa bila kuyaona maendeleo jameni na wenzetu wameshaanza kufunga mipaka ni hawataki immigrants. Sasa maendeleo tutayaonea wapi?
Kama ngozi ni nyeusi unategemea akili iwe nyeupe
 
Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu na ambao inatakiwa uendane na jamii hatua kwa hatua,bara la afrika halijulikani liko katika hatua ipi ya maendeleo.

Wenzetu ulaya,walianza na mapinduzi ya Kilimo,wakaenda kwenye mapinduzi ya viwanda na kuendelea,sisi ni kama tunaenda mbele tunarudi nyuma,Kilimo tangu azimio la Iringa la siasa ni Kilimo,hakijawahi kuleta mapinduzi ya kijani,na hata serikali inakiri kwamba nchi hii haijawahi kupita stage ya mapinduzi ya Kilimo,ndio maana viwanda kama ZZK-Mbeya vilikufa,akaja mwinyi naye akakalia kimya,hakuongelea Kilimo,Mkapa,hakuongelea,akaja kikwete na Mizengo Pinda, slogan yao ya Kilimo kwanza sijui ilifanikiwa wapi,lakini walau nchi ilinunua matrekta mengi sana pengine kuliko wakati wowote.

Serikali ya awamu ya tano, kwao Kilimo sio kipaumbele,kipaumbele chao ni viwanda,hapa tayari ni mkanganyiko,hatujafanya mapinduzi ya Kilimo,tumekimbilia kwenye viwanda,hivi viwanda vitatumia malighafi gani?

Hapa lazima nchi iwe na kilio cha njaa,karne ya 21 tunaombea mvua makanisani wakati vifaa vya umwagiliaji vimejaa duniani,tunavuna mpunga kwa mikono na sio combine harvester ,majirani zetu kila mwaka wanalia njaa,sisi badala ya kuona kama fursa,tunachofanya ni kuzuia chakula kisiende nje,na si kuzalisha

Kuhusu ajira,nadhani tatizo hili linaenda kwenye mzizi wa elimu wanayopewa watanzania,haiko practical mtaani,hasa elimu ya kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita,haimfungulii dunia mtanzania

Ukitaka kujua maendeleo yetu yanapandikizwa kutoka ulaya,angalia Baraza la Kiswahili wanavyohangaika kutafsiri/kutafuta maneno ya kiteknolojia kadri ulaya wanavyovumbua kitu kipya,

Neno Television,kwa mzungu mwemyewe lina maana hata bila kutafuta dictionary,Tele-vision, sisi tunaita Runinga,hakuna uhusiano wa kilugha,kimantiki kati ya kifaa na jina kinachopewa,
 
Africa tumejaaliwa kuwa na watu, tunazaana sana!
Siasa safi na uongozi bora tumewaachia wazungu, lazima tubadilike ili tuenadane na kasi ya ulimwengu...
 
Tunaweza kusema mchakato wa kimaendeleo wa bara hili ulikuwa "hijacked" na biashara ya utumwa,ukoloni na sasa ukoloni mamboleo.

Yale mapiramidi ya Misri yako Afrika,Kwa hiyo Afrika ilianza mchakato wa maendeleo mapema,ila ukazuiwa kwa karne karibu nne,bara likasimama kufanya jambo lolote la maendeleo,kila kona mwafrika alikuwa anasakwa apelekwe utumwani,atatulia saa ngapi afanye maendeleo?

Kuna maeneo kama Timbuktu,kwa nini yalifutika baada ya utumwa na ukoloni?biashara iliyokuwa inafanyika pale ilipotelea wapi? He mzungu angekubali biashara yake ishindanishwe na ya mwafrika?

Baadae ukaja ukoloni,walichofanya wakoloni ni kuziba njia zote za waafrika kufanya maendeleo na biashara,waafrika wakawa wanalima ili mavuno yapelekwe ulaya na faida yote

Madini yakawa yanachimbwa na kusombwa kupelekwa ulaya,afrika inabaki bila chochote!

Kwa hiyo Afrika ikawa "kibarua" wa bara la ulaya,mwafrika kwa zaidi ya miaka 400 hakupata fursa ya kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yake na bara lake,bara la afrika lilikuwa "jela" kwa zaidi ya miaka 400,karibu vizazi 7 !

Mpaka sasa makanisani mapadri,maaskofu hujisikia raha sana kutubatiza kwa majina ya kizungu,john,emmanuel,Felix,paul,wachungaji wetu na mapadri wanachukia ukiwaambia nataka mtoto wangu abatizwe kwa jina la @mitale midimu,

Na hii ni hatua ya kwanza,kama kitu ni mali yako lazima ukipe jina,sisi mpaka leo tunajisika raha kuitwa kwa jina la anayetumiliki,majina yetu ya babu zetu hatuyataki
Baada ya Uhuru.......
 
Aseee ndugu ni kweli kabisa hasa kwenye giza la umeme na maji.
 
SAWA, Mkwamo huu ulitakiwa uyeyuke taratibu tangu 1960s.
china walianza 1978, Singapole 1965 sisi bado hakuna hata dalili ya nukta ya mabadiliko.
Mzungu njoo tena, Ila safari hii tuonee huruma usitufitini wala kutuibia, washa taa za bongo zetu ili na sisi tufurahie mema ya nchi...
Hakuna namna...
 
Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu na ambao inatakiwa uendane na jamii hatua kwa hatua,bara la afrika halijulikani liko katika hatua ipi ya maendeleo.

Wenzetu ulaya,walianza na mapinduzi ya Kilimo,wakaenda kwenye mapinduzi ya viwanda na kuendelea,sisi ni kama tunaenda mbele tunarudi nyuma,Kilimo tangu azimio la Iringa la siasa ni Kilimo,hakijawahi kuleta mapinduzi ya kijani,na hata serikali inakiri kwamba nchi hii haijawahi kupita stage ya mapinduzi ya Kilimo,ndio maana viwanda kama ZZK-Mbeya vilikufa,akaja mwinyi naye akakalia kimya,hakuongelea Kilimo,Mkapa,hakuongelea,akaja kikwete na Mizengo Pinda, slogan yao ya Kilimo kwanza sijui ilifanikiwa wapi,lakini walau nchi ilinunua matrekta mengi sana pengine kuliko wakati wowote.

Serikali ya awamu ya tano, kwao Kilimo sio kipaumbele,kipaumbele chao ni viwanda,hapa tayari ni mkanganyiko,hatujafanya mapinduzi ya Kilimo,tumekimbilia kwenye viwanda,hivi viwanda vitatumia malighafi gani?

Hapa lazima nchi iwe na kilio cha njaa,karne ya 21 tunaombea mvua makanisani wakati vifaa vya umwagiliaji vimejaa duniani,tunavuna mpunga kwa mikono na sio combine harvester ,majirani zetu kila mwaka wanalia njaa,sisi badala ya kuona kama fursa,tunachofanya ni kuzuia chakula kisiende nje,na si kuzalisha

Kuhusu ajira,nadhani tatizo hili linaenda kwenye mzizi wa elimu wanayopewa watanzania,haiko practical mtaani,hasa elimu ya kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita,haimfungulii dunia mtanzania

Ukitaka kujua maendeleo yetu yanapandikizwa kutoka ulaya,angalia Baraza la Kiswahili wanavyohangaika kutafsiri/kutafuta maneno ya kiteknolojia kadri ulaya wanavyovumbua kitu kipya,

Neno Television,kwa mzungu mwemyewe lina maana hata bila kutafuta dictionary,Tele-vision, sisi tunaita Runinga,hakuna uhusiano wa kilugha,kimantiki kati ya kifaa na jina kinachopewa,
Angalau umeleta mwangaza kwenye njia ya kupita kuliko malalamiko ya mtoa mada. Afrika ni lazima ifikirie namna ya kujikomboa yenyewe badala ya kufikiria misaada ya watu wa mabara mengine. Afrika inaweza kusogea ikiwa wafrika wenyewe tutaanza kuyasimamia tuyoyaamini na kuacha malalamiko. sisi watanzania tuna nafasi kubwa ya kuitumia ardhi nzuri na kubwa tuliyonayo kwa mtu mmoja mmoja na vikundi kufanya mageuzi ya kilimo. hata kama serikali imeshindwa kutosogezea maji bado tunayo fursa ya kuyafuata maji mahali yalipo, ruvuma, morogoro, katavi, rukwa, kigoma, mwanza, na kwingineko. lakini makundi ya nguvukazi tumejazana mijini kuwasubiri wawekezaji wa kichina ili tupate ajira. kisa una elimu huwezi kuishi kijijini!!
 
SAWA, Mkwamo huu ulitakiwa uyeyuke taratibu tangu 1960s.
china walianza 1978, Singapole 1965 sisi bado hakuna hata dalili ya nukta ya mabadiliko.
Mzungu njoo tena, Ila safari hii tuonee huruma usitufitini wala kutuibia, washa taa za bongo zetu ili na sisi tufurahie mema ya nchi...
Hakuna namna...
Mkuu hakuna haja wala sababu za kuwafikiria wale waliosababisha tuwe hapa tulipo. Tututumie elimu tuliyoipata kwao kujitoa kwa ajili ya nchi zetu. Huu ni muda wa kuangalia fursa na kuzifanyia kazi. Naamini tukiweka NIA tutasogea na kufika tunapotaka
 
Back
Top Bottom