Nimekubali kweli Afrika ni Bara giza

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Mzee mmoja alisema Waafrika tuna FRESH and UNUSED BRAIN. Siku tukisema tubadilishane BONGO wazungu watumie hizi zetu, dunia wanaweza kuihamishia MARS.

GIZA LA NJAA
Kwa mshtuko kabisa, 60% ya ardhi ifaayo kwa kilimo duniani, inapatikana afrika.
60% ya wakazi wa afrika ni vijana miaka chini ya 25 wenye nguvu mpya,akili safi
na uwezo lakini mamillioni ya watu
wanakwenda vitandani usiku kulala bila kula.
Nchi nyingi za afrika zinatumia mabillioni ya dola kuagiza vyakula nje.
Hii inaacha mwanya mkubwa kwa mzungu/mchina kuja kuwa billionea kwa fursa hii.

GIZA LA AJIRA
Afrika tuna uhaba wa ajira, kuna uhaba mwingine unasababishwa na kutokuwepo na
taarifa kati ya muajiri na muajiriwa. ndio maana ukienda uarabuni wanasema utakuta
waasia kibao wakifanya kila kazi huku waafrika wakionekana kwa kusuasua.
Pili ni Kutokuajirika. Kuna ombwe la maarifa kati ya muajiriwa na kazi anayotaka kufanya au
aliyesomea. Hii inatoa fursa kwa Mzungu Kuziba hilo ombwe huku akijiingizia mamilioni.

GIZA LA AFYA na MAGONJWA
Afrika inachukua 15% ya watu wote duniani, lakni 24% ya magonjwa duniani yanapatikana afrika.
HAYA MATATIZO YAMEIBUA Uhitaji mkubwa sana na walazima wa dawa afrika kuliko sehemu nyingine.
Mzungu/Mchina hapa anaweza kuwekeza na kuwa billionea kwa muda mfupi.

GIZA LA UMEME
Ukienda NASA ukapewa lift kwenye ile rocket inayoenda angani, ikifika usiku iangalie dunia kupitia upande wa afrika.
Utakuta ni kama shimo kubwa jeusi lenye giza la kutisha.
Hivi ulikuwa unajua nchi zote 48za kusini mwa jangwa la sahara, zenye wakazi takribani Millioni 750 zinazalisha umeme
sawa na wa nchi ya SPAIN yenye wakazi Millioni 50 idadi karibu sawa na watanzania.
Mzungu/Mchina njoo Afrika lena haraka uwe billionea kwa kutuwashia taa akilini na nje ya mwili.
Mwanamuziki AKON ni miongoni kwa watu weusi wanaojikongoja kutengeneza mabillioni kutatua hili giza kwa kusambaza SOlar.

GIZA LA MAJI
Kwa maji haya matamu,masafi na mazuri yaliyoko afrika ni dhahiri Muda sio mrefu wazungu,waarabu na waasia wataanza kuja
Kuteka maji afrika. Kuna mamillioni ya wanaafrika wanakufa kwa kiu na kuhara kwa
kukosa maji safi katikati ya chanzo cha maji safi.
Mzungu/Mchina njoo utuokoe safari hii usititawale washa taa kwenye bongo zetu. Haya maombi Tungemuomba Mungu
Lakini ni ya kiwango cha chini kiasi kwamba Mungu tutamsumbua bure.
Mzungu/Mchina njoo basi utuokoe wanadamu wenzako. Safari hii ukija Usitupige fimbo,
usituibie, Tutakupa pesa wenyewe huku ukitatua matatizo yetu.
Tusaidieni wanadamu wenzenu
Hili giza lililotapakaa UBONGONI bila nyie linazidi kutapakaa kwenye afya,Umeme,Maji,mahusiano kila kona.
Wahini haraka jamani mtusaidie safari hii msitufitini, Washeni taa kwenye bongo zetu na nje ya bongo kisha mrudi kwenu.

Wazungu/Wachina tafadharini sana, chondechonde tusaidieniii wote ni wanadamu...
 
Kama rangi yetu tu... ni giza kila kona.

Mapenzi yake Mungu.
acha kabisa, unafiki sio kitu kizuri waje tu watsaidie wametuibia tulikubali walivyotuachia vinatutoa jasho, waje watusaidie chondechonde tumeaibika vya kutosha.

Mungu mwenyewe hapendi vyu vya hovyohovyo ndio maana hle mji tunaousikia ameandalia wateule ni mzuri saana.
angesema tutaishi porini siku akituchukua kwenda kwake. bali ni sehemu pazuri sana tu. Wanadamu tumeumbwa kwa ajili ya mazuri. Kama tumeshindwa waje watusaidie ni wenzetu wale.
 
tumerogwa
hatujarogwa mkuu, Tunaakili nyingi ambazo hazitumiki.
Mimi nakubali naanza kujifunza kuwa mkweli.
Maana hata mzungu akitupa msaada, utaona sisi sisi tunanunua V8 wakati enzi za nyerere walikuwa wanatumia land lover na miundombinu ilikuwa ovyo kupindukia.
 
Baada ya kuona hayo matatizo umeamua kufanya nini kutatua? Badala ya kutumia bongo kutatua hutaki kabisa kufikiri unaamua kukimbilia nje waje kusaidia. Huo ndo uafrika wenyewe mnajua kulalamika tu ila hamtaki kufikiria njia za kutatua
 
Na kweli haiwezekani ununue v8 wakati huyo aliye kupa msaada wanatumia gari za kawaida .Africa tuombe sana mungu atupe vioongozi wenye mapenzi na nchi zao maana tunaangamia nakuonekana km wajinga wakubwa
 
Mojawapo ya nyuzi makini sana mkuu… wanikumbusha mistari ya mwanamuziki Bob Marley kwa wimbo wa rat race… in the abundance of water a fool is thirsty…
 
acha kabisa, unafiki sio kitu kizuri waje tu watsaidie wametuibia tulikubali walivyotuachia vinatutoa jasho, waje watusaidie chondechonde tumeaibika vya kutosha.

Mungu mwenyewe hapendi vyu vya hovyohovyo ndio maana hle mji tunaousikia ameandalia wateule ni mzuri saana.
angesema tutaishi porini siku akituchukua kwenda kwake. bali ni sehemu pazuri sana tu. Wanadamu tumeumbwa kwa ajili ya mazuri. Kama tumeshindwa waje watusaidie ni wenzetu wale.
Very sorry
samahani nani kakuibia wewe!!!
tumia macho yako na akili zako hakuna aliyekuibia "sibure miundombinu yao na elimu zao zime staarabisha to this present extent....."
miaka 60 ya uhuru na kujitawala...... fyuuuu
 
Baada ya kuona hayo matatizo umeamua kufanya nini kutatua? Badala ya kutumia bongo kutatua hutaki kabisa kufikiri unaamua kukimbilia nje waje kusaidia. Huo ndo uafrika wenyewe mnajua kulalamika tu ila hamtaki kufikiria njia za kutatua
Mm binafsi na familia yangu nimeamua kujikwamua kwenye lindi la umaskini wa kipato.. Hali.. Na akili.. By any means necessary…
 
Hivi binadamu wote kama vile, waafrika, wazungu, waarabu, wa Asia n.k waliumbwa na Mungu kama binadamu wote au kuna ambaye walikuwa kwenye kikundi cha 'let there be...' nawakawepo ila wakawa wamefanana na binadamu sana wakaunganishwa humo by mistake. sbb hapa afrika sijui tutakufa bila kuyaona maendeleo jameni na wenzetu wameshaanza kufunga mipaka ni hawataki immigrants. Sasa maendeleo tutayaonea wapi?
 
Back
Top Bottom