Nimekubali kushindwa narudi kijijini

Nimekubali kushindwa narudi kijijini

Fahari ya kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2022
Posts
427
Reaction score
1,668
Chumba kimoja ninachoishi kimenikumbuka kuwa napoteza muda na maisha ya mjini; heri nirudi kijijini.

Haiwezekani nina miaka 35 halafu bado naishi kwenye chumba kimoja.

Ukiachilia mbali majirani kuniona 'mhuni' niliyegoma kukua, kuna sababu nyingine nyingi zimenilazimisha nihame.

1. Haiwezekani hadi leo nalala chumba kimoja na magudulia ya maji. Naweka viatu uvunguni. Napikia chumbani. Miaka 35?

2. Kila siku nawatembelea jamaa makwao, nakwepa waje kwangu kwa sababu sebuleni nd'o chumbani. Si jambo jema kila mgeni kuona ninapolala.

3. Nikipata mgeni wa maana, tunakutana barabarani, kwa sababu naona haya kumkaribisha kwangu. Wanaona siko 'serious' na maisha yangu.

4. Miaka 35 bado namletea michezo ya kombolela mwenye nyumba. Kodi ikiisha nawahi kuamka na kuchelewa kulala, alimradi kumkwepa tu. Miaka 35 bado nashindwa kulipa kodi ya 35,000? Yaani kila mwaka nilioishi duniani thamani yake ni buku, lakini bado ndefu. Huu ni utani, watu wa rika langu wana nyumba za kupangisha, mimi bado nakimbizana na kodi. Najitambua kweli?

Heri nirudi nyumbani kijijini, huko nitajenga kibanda katika shamba kubwa la urithi. Mwembe wa nje utakuwa sebule; hapo ndipo nitakapofanyia vikao na wageni wangu. Madumu nitayaweka nje kwa kuwa kule kijijini hatuibiani.

Haya maisha ya kuishi mjini kwenye chumba kimoja ilhali mali pekee ya thamani ninayomiliki ni king'amuzi, si maisha. Au niseme, yana ukomo. Si maisha ya sisi 35+.

Nimekubali kushindwa vita. Narudi kijijini...

Naenda kuandaa mikorosho na ufuta
 
Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, naona uamuzi wako si wa kushindwa, bali ni wa ujasiri na kujitambua. Watu wengi wanakwama kwenye maisha wasiyoyataka kwa sababu ya kuogopa maneno ya watu. Wewe umeamua kuchukua hatua.

Hapa kuna ushauri kidogo, ukizingatia uamuzi wako wa kurudi kijijini:

1. Andaa Mpango wa Mpito (Transition Plan)​

Kabla hujaondoka mjini, jaribu kufanya yafuatayo:
  • Weka Akiba Kidogo: Hata kama ni kidogo, jaribu kuweka akiba ya kujikimu kwa mwezi mmoja au miwili kijijini wakati unaanza kujipanga. Itakupa nafasi ya kupumua bila presha.
  • Wasiliana na Ndugu: Waambie ndugu na jamaa wa karibu kijijini kuhusu mpango wako. Wanaweza kukusaidia kwa mawazo, nguvu kazi ya kuanza, na kukupa moyo.
  • Uza Vitu Usivyovihitaji: Angalia vitu ulivyonavyo chumbani. Vile ambavyo hutavihitaji kijijini (labda isipokuwa king'amuzi chako), unaweza kuviuza ili kupata nauli na kianzio kidogo.

2. Anza Kidogo Lakini kwa Malengo (Start Small but with a Goal)​

Umerithi shamba, hiyo ni neema kubwa na mwanzo mzuri kuliko wengi.
  • Kilimo cha Chakula Kwanza: Anza kwa kulima mazao ya chakula kwa ajili yako na familia. Hii itapunguza gharama ya maisha mara moja. Lima mahindi, maharage, mboga za majani.
  • Tafuta Zao la Biashara: Baada ya kuhakikisha una chakula, chunguza ni zao gani la biashara linalokubali vizuri eneo lenu. Inaweza kuwa alizeti, ufuta, mbogamboga, au matunda. Anza na eneo dogo, hata robo eka. Lengo ni kujifunza kwanza.
  • Ufugaji Mdogo: Kuku wa kienyeji au mbuzi wachache ni mradi mzuri sana wa kuanzia. Hawa huhitaji mtaji mkubwa na wanaweza kuongezeka haraka, wakikupa chanzo cha fedha na chakula.

3. Jenga Heshima Kijijini (Build Respect in the Village)​

Watu wa kijijini wanaweza kuwa na mitazamo tofauti. Wengine watakuona umeshindwa mjini, wengine watakupongeza. Jinsi utakavyoishi ndiyo itakayojenga heshima yako.
  • Shiriki Kwenye Shughuli za Kijamii: Usijitenge. Shiriki kwenye misiba, harusi na shughuli za maendeleo ya kijiji. Hii itakufanya uwe sehemu ya jamii.
  • Kuwa Mchapakazi: Watu wakuone unajituma kwenye shamba lako. Heshima ya mwanaume kijijini mara nyingi inapimwa kwa jinsi anavyohudumia shamba na familia yake.
  • Tumia Ujuzi wa Mjini: Uzoefu na maarifa uliyoyapata mjini (hata kama ni kujua kusoma habari, kuelewa mambo, au kuwa na mtazamo mpana) unaweza kuutumia kusaidia jamii na kukuletea fursa.

4. Mtazamo (Mindset)​

Hili ndilo jambo la muhimu zaidi.
  • Acha Kujilinganisha: Safari yako ni yako. Acha kuwaza kuhusu wenzako wenye nyumba za kupangisha mjini. Mafanikio yako sasa yapime kwa amani ya moyo, kuwa na chakula cha kutosha, na uhuru wako.
  • Kubali Mwanzo Mpya: Jione kama mtu anayeanza sura mpya, si kama aliyefeli. Ile "sebule ya chini ya mwembe" ni ishara ya maisha halisi na ya uhuru, si umasikini.
Uamuzi wako ni sahihi kwa sababu unatanguliza utu na amani yako. Maisha si mashindano. Nenda kajenge maisha yako kwa masharti yako. Anza taratibu, Mungu atakuongoza.
 
Chumba kimoja ninachoishi kimenikumbuka kuwa napoteza muda na maisha ya mjini; heri nirudi kijijini.

Haiwezekani nina miaka 35 halafu bado naishi kwenye chumba kimoja.

Ukiachilia mbali majirani kuniona 'mhuni' niliyegoma kukua, kuna sababu nyingine nyingi zimenilazimisha nihame.

1. Haiwezekani hadi leo nalala chumba kimoja na magudulia ya maji. Naweka viatu uvunguni. Napikia chumbani. Miaka 35?

2. Kila siku nawatembelea jamaa makwao, nakwepa waje kwangu kwa sababu sebuleni nd'o chumbani. Si jambo jema kila mgeni kuona ninapolala.

3. Nikipata mgeni wa maana, tunakutana barabarani, kwa sababu naona haya kumkaribisha kwangu. Wanaona siko 'serious' na maisha yangu.

4. Miaka 35 bado namletea michezo ya kombolela mwenye nyumba. Kodi ikiisha nawahi kuamka na kuchelewa kulala, alimradi kumkwepa tu. Miaka 35 bado nashindwa kulipa kodi ya 35,000? Yaani kila mwaka nilioishi duniani thamani yake ni buku, lakini bado ndefu. Huu ni utani, watu wa rika langu wana nyumba za kupangisha, mimi bado nakimbizana na kodi. Najitambua kweli?

Heri nirudi nyumbani kijijini, huko nitajenga kibanda katika shamba kubwa la urithi. Mwembe wa nje utakuwa sebule; hapo ndipo nitakapofanyia vikao na wageni wangu. Madumu nitayaweka nje kwa kuwa kule kijijini hatuibiani.

Haya maisha ya kuishi mjini kwenye chumba kimoja ilhali mali pekee ya thamani ninayomiliki ni king'amuzi, si maisha. Au niseme, yana ukomo. Si maisha ya sisi 35+.

Nimekubali kushindwa vita. Narudi kijijini...

(Similiki picha hii)

kama upo na Afya njema mshukuru Mungu mambo mengine yatakaa sawa .

At ur age nilikuwa under parent and I used to rent a single room me with my Families.

Usikate tamaa grind. 24/7 ur time is near.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom