Ni ngumu kuwasemea watu lakini wakati mwingine unaweza ukakuta mwanadada anataka kulipiza kisasi kutokana na aliyotendewa na wanaume wengine
pia yawezekana wakati anachukuliwa na huyu mwanaume yeye alikubali ili apate comfort and shelter kwa kipindi kile tu ila ndani yake hakuwa na upendo hata chembe ndani yake
wanawake huwa tunasifika kwa tabia ya huruma sana lakini mwanamke ni kiumbe hatari kupita maelezo hasa pale anapokuwa alitendwa mara kadhaa..huu ni mtizamo wangu binafsi
watu8,,mm! Kama bila gravitation force tusingekuwa na balance ya kutembea basi nayo inachangia watu kutetea upendo wao!
Maana ya hayo maneno ni kuwa once you start falling in love there won't be nothing(sort of external force or circumstance) holding back....kwa mantiki hiyo basi mioyo yetu ipo katika risk ya kuumia maana hakuna kizuiacho kuanguka...
afadhali umedadavua huu ujumbe wako maana hapo awali sikuelewa ulichomaanisha
promiseme,,ntamfikishia ila kama alijua anampenda wa zamani mbona anamuumiza huyu..life
Wallah naelewa imesha nitokea lakini kila likuepukalo lina kheir na wewe,najua sio rahisi kukubali matokeo lakini ajitahidi na mungu atamsaidia na huyo mwanamke atajuta mwisho wake............
Always handle your scandal.
haya mambo yanahitaji uangalifu lasivyo unaishia kuoa kisu na si mke....take your time
Kama hii ni true story basi jamaa katendwa kweli kweli, pole yake ila ajikaze kiume ndo maisha.
aise huyu mwanamke hana shukrani kabisa. Mume alikutosa na mtoto mchanga kwa mateso halafu unampata wa kukufariji tena anakutunza na kukufungulia biashara halafu unamrudia!!! Kweli wanawake nyie ni vinyonga kabisa!!! For sure nikimuacha mtu namuacha jumla, never go back to matapishi hata aje akiwa anatambaa.
Hivi kwanini mtu ukiwa 'hutakiwi' kimapenzi unaumia!? Je, si rahisi tu kukubali hali halisi kwamba 'hutakiwi' maisha yakaendelea!? Unaumia weee...wengine wanajiua (pumbaff, miaka yote uliyoishi bila yeye mbona hukufa), wengine wanakonda kwisha kabisa, wengine wanalia usiku kuchwa, wengine wanakuwa walevi, wengine wanashindwa kula kabisaa... Ebo, unataka kila unayemtaka naye akutake!? We nani!? Kama hutakiwi 'chapa lapa'...katafute mbele ya safari huko! Hata kama ulishampata, ikitokea kwa sababu moja ama nyingine hakutaki tena..'chapa lapa'!