Wewe acha mbwembwe wewe whom the hell do you think you are kumwita binadamu mwezio ana sura chafu?we ndo umemuumba?angalia sana kijana hujafa hujaumbika huwezi kujua nini kitatokea kesho wewe leo ni kijana mtanashati sijui handsome,kesho waweza kugeuka kituko na kichekesho kwenye macho ya watu,kwa taarifa yako hakuna anyependa kuwa na sura isiyovutia ila mtu anakosa jinsi kwa sababu ndivyo alivyoumbwa na mungu,kama mtu angekuwa anjiamulia kuwa na sura ipi basi kila mmoja duniani hapa angekuwa ameridhika na jinsi alivyo,ila kwa kuwa tunaumbwa basi mtu anakuwa hana la kusema,
wewe kama mungu kakujalia sura na umbo zuri mshukuru na uwaonee huruma wale ambao hawakujaaliwa na sio kuanza kuwa dharau na kuwaita majina yasiyofaa,kwani wao pia ni binadamu kama wewe au labda kwa kuwa wewe ni mzuri una tofauti gani nao,unakula dhahabu?unavuta almasi unapumua tanzanite?una.................naomba niishie hapa nisije nikaongea visivyoongeleka bure,kijana rekebika maneno uliyotumia kucoment picha ya mdada hapo juu hayafai hata kuwa dekio.
me ni kijana mtanashati am model nina tabia ya kutuma namba yngu kwenye radio na kutafuta marafiki wa kike niliwapata wasichana wengi tu wengine niliwatongoza baadhi walikubali na wengine walikataa wale waliokubali nikapanga nikutane na mmoja badala ya mwingine hao nilikutana nao haikuwa type yngu niliporudi hme nikawachana wote nikawaambia hatuendani kabisa nimekoma kutuma namba yngu kwenye radio