nzilwa
Member
- Nov 6, 2016
- 23
- 23
Kipindi nikiwa likizo kijijini kwetu,nilikuwa na tabia ya kwenda matembezini vijiji vya jirani na mdogo wangu!
Usafiri wetu mahili ilikuwa ni baiskeli ya phonex tuliyokuwa nayo hapo nyumbani!
Kuna siku nikiwa likizo ya mwezi Juni na mdogo wangu tukaamua kutembelea kijiji cha jirani kilichokuwa kinaitwa Igunda!
Muda wa saa 1 usiku tukawa tumefika pale kijijini! Tabia yetu ilikuwa ni ubabe na kuwapokonya vijana mabinti kwa ubabe!
Tukiwa kwenye kilabu fulani cha pombe za kienyeji,tukafanya fujo takatifu,kwani tulinunua pombe ya komoni pipa zima na kuwaambia walevi wote wanywe bure! Wakashangilia! Lengo letu ilikuwa tuondoke na binti mmoja mrembo jina lake Kabula!
Kumbe yule binti alikuwa mchumba wa babu mmoja ambaye naye alikuwepo pale kilabuni!
Yule babu kumbe alikuwa anatuchora tu kila kitu tulichokuwa tunakifanya!
Baadaye yule babu alishindwa kuvumilia akaamua kuja kutupa tahadhari kuwa kuwa huyo binti tumuache ni wa kwake!
Nilimjibu kwa kumfokea na kumwambia wachawi hawaoni ndani kwetu!
Ilikuwa mida ya saa 6 usiku tukaamua na dogo turudi nyumbani na baiskeri yetu! Ilikuwa ni giza na baiskeli yetu haikuwa na taa!
Dogo alikuwa anaendesha baiskeli mimi nikiwa nimekaa siti ya nyuma!
Baada ya kukiacha kile kijiji kama umbali wa km 2, kwenye kimteremko fulani,nikasikia puuu!
Tulipiga mweleka na baiskeli yetu! Nikainuka na kumjulia hali mdogo wangu,akanijibu kuwa hajambo isipokuwa baiskeli ilikuwa imevunja in form of 2 pieces,tairi ya nyuma na vyuma vyake na tairi ya mbele na usukani kivyake!
Ikabidi tugawane kila mtu na kipisi chake na safari ikawa kwa mguu!
Tulitembea umbali wa kama mita 100,mbele kikatokea kitu cha ajabu! Yaani eneo LA duara ya mita hamsini hivi palikuwa ni mchana kwenye eneo hilo na kulikuwa na watu wengi wanafanya kazi mbali mbali! Na yule babu alikuwa anauza mahindi! Tulisimama na Mdogo wangu kuangalia kituko hicho! Ilichukua kama dakika tano hivi,kikatoweka na kurejea giza! Tukaendelea na safari huku tukiwa kimya kabisa!
Umbali tena kama wa km1 hivi,tukaona treni ikiwa na mabehewa 23,ikiwa imejaza abiria inatokomea mlimani!
Kumbuka sehemu hiyo hapakuwa hata na reli! Tulisimama kama nusu saa kutafakari tukio hilo!
Hali ya kawaida ikarudia tukaendelea na safari!
Tulifika nyumbani kwenye saa 10 alfajiri! Tulipoingia chumbani nikamuuliza Mdogo wangu kama anakumbuka yote yaliyotupata njiani,akasema anakumbuka!
1)Kuvunjika baiskeli;
2)Eneo lenye umchana wakati nilikuwa ni usiku;
3)Treni ikiwa na abiria inatembea bila reli!
Toka siku hiyo utundu vijijini nilishaapa kutokurudia tena!