ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,356
- 4,626
Ninaona mwanga mkali huku maeneo mengine yakiwa ya mejaa kiza.Kwa kuwa sijui nilipo tumaini langu pekee ni kufuata mwanga ule niuonao.Natembea taratibu huku nikiwa na wasiwasi mkuu.Najiwa na kumbu kumbu ya mambo mengi niliyoyaona duniani.Kumbu za watu waliokufa,waliokuwa wakiteswa,waliokuwa wakipata taabu kwa sababu mbalimbali.
Nakumbuka sana na kwa sasa kumbukumbu zinanijia kama vile ni jambo linalotokea sasa hivi.Napata msukumo wa kutaka kufanya jambo ili kuondoa hali ile katika dunia.Najiamini sana na kwa mara ya kwanza naona kabisa kuwa nina uwezo wa kuwasaidia waliokuwa wanateseka, ninaona kuwa nina uwezo wa kuwaokoa waliokuwa wanateseka. Ninajiona mwenye mamlaka na nguvu nyingi. Nisiyeogopa hatari yoyote.
Niko tayari kwa lolote vyovyote kuifanya dunia kuwa bora zaidi.Ninapata kumbukumbu wa nyakati za majaribu.Nyakatia ambazo alitakiwa kusimama mtu na kutetea watu waliokuwa wanaonewa na kunyanyasika.Ninajiona kuwa mimi ndiye ninayepaswa kufanya hivyo na nina kiu kubwa ya kuchukua hatua.
Nikiwa na mawazo haya naendelea na safari yangu kuufuata mwanga.Naona maandishi yameandikwa JEHANAM, ninashtuka sana kwa hofu ninaona watu wanalia na kuteseka na ninaona kadiri ninavyojaribu kusita kwenda ndio ninavozidi kwenda karibu na lango lile lakini ghafla napitiliza na kutokea katika upande mwingine huku bado nikiona kiza kila upande naendelea na safari kwa taratibu huku nikipata ahuene kwamba sijaingia jehanam.
Naona mwanga kwa mbali na maandishi kama yale yameandikwa JEHANAMU YA WATAKATIFU.Ninashtuka lakini kwakuwa ile ya kwanza ilinipita najipa moyo kuwa sasa pia nitapita.
Jehanam hii ina mateso makali kupita ile ya kwanza vilio nilivyoviona na mateso niliyoyaona ni zaidi ya ile jehanamu ya kwanza.Kiukweli ningepaswa kuchagua ningechagua ile ya kwanza.Kwa kuwa ya kwanza sikuingia najipa moyo kuwa hata hii sitaingizwa.
Kwa mshangao najikuta nikiwa katika eneo la uwazi huku hakimu mkuu akiwa katika kiti cha enzi.
Chini yake pameandikwa ENEO HILI LIMETENGWA KWA AJILI YA WATU AMBAO KATIKA NYAKATI ZA MAJARIBU NA MATESO AMBAPO WALITAKIWA KUONYESHA MSIMAMO WAO WALICHAGUA KUWA VUGUVUGU.Kwa kizungu.THIS AREA IS RESERVED FOR THOSE PEOPLE WHO IN THE TIMES OF TRIALS AND PERSECUTION CHOSE TO BE NEUTRAL.
Maneno haya yalikuwa katika lugha zote za ulimwengu na niliona watu wengi sana walioishi maisha mema duniani.
Niliambiwa hapa ndipo panaponifaa kwa sababu sikushiriki katika kuleta mabadiliko na kuonyesha msimamo wangu bali nilijikomba na kutaka kuonekana mwema ili nipate changu huku nikiacha wengi wateseke.