UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 3,101
- 14,248
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!
Binafsi kuanzia Leo Mimi UMUGHAKA WA BHAGHAKA
Nimejivua rasmi uanachama wa klabu ya Young Africans almaarufu kama Yanga!
Nimekuwa shabiki wa hii timu ningali bado niko shule ya msingi,nimekuwa mpenzi wa hii timu ningali bado kinda,nimekuwa mkereketwa wa hii klabu ningali bado kijana wa makamu,pia nimekuwa mwanachama wa klabu hii tangu mwaka 2003.
Hivyo kuanzia Leo nimeamua kubwanga manyanga rasmi!
NIMEAMUA YAFUATAYO :-
1.Kuchoma kadi zangu zote za Uanachama nilizowahi kumiliki
2.Kugawa Jezi Kwa jamaa mmoja ambaye ni shabiki wa Yanga hadi hivi Sasa (Nilitaka kuzichoma lakini nikaona kuchoma nguo si jambo jema)
SABABU ZA MIMI KUAMUA RASMI KUACHANA NA KUJIVUA UANACHAMA
1.Nimechukizwa mno na kitendo Cha Rais wa Yanga kuhudhuria kwenye Harambee ya Chama Cha Mapinduzi na kutoa mchango Kwa niaba ya timu ya Yanga!
Ieleweke kwamba,binafsi sichukii Hersi Kuwa mwanachama wa CCM,huo ni uhuru wake binafsi ambao umetajwa kwenye katiba ya nchi,kilichonikera na kuniudhi I kuitumia nembo ya Yanga kwenye masuala ambayo ni Binafsi,Klabu ya Yanga inaendeshwa Kwa mujibu wa katiba ya klabu,pia Bajeti zote zinazohusiana na klabu hupitishwa na mkutano mkuu!
Mkutano mkuu wa mwisho ulioketi mnamo 9.6.2024 hakukuwa na Ajenda ya kuchangia Vyama vya siasa,Sasa hiyo Pesa iliyotolewa na Rais Hersi Kwa niaba ya klabu ya Yanga kwenda Kwa CCM ilipitishwa kwenye Bajeti ipi na ilikuwa mkutano mkuu ulioketi mwaka gani?
Yes,yawezekana isiwe pesa ya klabu,sawa nakubali,Je kwanini chapa/nembo ya klabu ya Yanga ihusishwe?
Sababu nyingine hazina uzito sana na ningeweza kuzivumilia,hii ya kutumia nembo ya Yanga kwenye masuala ya kisiasa imenisikitisha sana!
Rasmi Sasa narudi England Kwa washika manati niendelee kukonda Kwa mawazo!