Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,611
Lakini mwendazake si CCM huyo huyo? Hapo tofauti ni kwamba ndani ya CCM kutakuwa na itikadi tofauti... ila chama ni hicho hicho kimoja.Sio kweli, mbona mwendazake aliipangua na kuweka watu waka na sera zake kama alivyotaka
Subiri uone mikutano miwili tu ya Hadhara watajuta kuruhusu mikutano ya siasa.Ukitembea kwa walala hoi mikoa mbali mbali, huwaambii kitu kuhusu CCM ....
Ukomunisti ndo una tabia ya kukita mizizi kila kona.. kwenye idara zote za elimu, ulinzi, sanaa... nk.Pamoja na kuwa CCM imenikuza, Pamoja na kuwa CCM imeniangusha. Hata siku moja-au Kamwe siwezi kuiita ya Kikomunisti.
Na ukipata mda ...please Define Ukomonisti.
Hiyo ni lugha ya Ukimbari, Ni lugha inayotumika kuwahadaa Vijana wa Ulaya na Magharibi yake.
Haina mshiko tena katika korido za Kimataifa na ni za wale wa Mlengo wa Kulia- Kulia (Far-Right) Yaani wale wanaohusishwa na Ushetani. Msitumezeshe sumu zenu.
Ni Propaganda Hasi.
Utaeleweka.
Ushauri wangu ni bora tusiwe na vyama vya upinzani... maana gharama za uchaguzi ni kubwa sana, hizo pesa zingepelekwa kusaidia maendeleo..Una ushauri gani kwa vya upinzani.
vifutwe au wafanya nini kushika dola mkuu.
Hiyo mikutano ineruhusiwa na nani???... tukubali tukatae.. ukiona mpaka mikutano ambayo ipo kisheria inaamuliwa na matakwa ya CCM, wewe mpinzani utasemaje kwamba una ndoto za kuitoa CCM madarakani?Subiri uone mikutano miwili tu ya Hadhara watajuta kuruhusu mikutano ya siasa.
Hapa Tanzania CCM ilishakataliwa.
Acha kuandika hisia.
Sahihi kabisa....Pamoja na kuwa CCM imenikuza, Pamoja na kuwa CCM imeniangusha. Hata siku moja-au Kamwe siwezi kuiita ya Kikomunisti.
Ccm ni chama kujifichia makucha ya ufisadi ,Kama nadanganya fuatilia wote wajifanyao ccm kindakindaki ,utashangaaHii ni baada ya kuzunguka kwenye taasisi kubwa za kielimu hapa nchini na kubaini kwamba asilimia kubwa ya hawa tunawaita wasomi wa ngazi za juu ni wana CCM kindakindaki na bado wana imani kubwa na dola iliyopo.
Ukitembea kwa walala hoi mikoa mbali mbali, huwaambii kitu kuhusu CCM.
Ukija kwenye hivi vinajiita vyama vya upinzani ukivichambua haswaaa na ukavichimba, unakuja kuona kwamba ni wale wale tu CCM. Maana wanatembea mule mule kwenye njia za CCM.
Yaani hivi vinajiita vyama vya upinzani wanachogombea ni viti vya ubunge wapate ruzuku maisha yaende, ukichunguza sana bado unaona hamna chama cha upinzani ambacho kipo tayari kuunda serikali.
Na hiki ni chama ambacho kimetawala nchi miaka inaenda sitini sasa.
Hujapita kwenye taasisi za ulinzi na uasalama, nako huko kumejaa wenye mapenzi na CCM kindaki ndaki.
Ndo mana nasema, CCM imejichimbia mizizi kama chama cha kikomunisti cha China. Wamewezaje kufanya hivo, sijui.
Ila ifike mahala sasa wananchi, tuwaombe CCM wawe wanatuletea viongozi wenye akili, na kama ikibidi hata system ihusike, kuhakikisha taifa linapata viongozi wenye akili ya ku drive growth ya nchi.
Iwe kama tu chama cha kikomunisti cha China, system inahakikisha nchi inatawaliwa na watu wenye bongo na sio hawa utopolo ambao wanatembelea brand ya CCM kwa kujua kwamba itatawala milele.
I wish mpinzani ninayemkubali mimi 'Tundu Antiphas Lissu' angekuwa tu ni mwana CCM, maana nimegundua huko upinzani ni watu wachumia tumbo tu na watu hopeless.
Najua ntapokea matusi yote, lakini najaribu kuwa realistic, huwezi kupambana kwenye hakuna.
N.Mushi
Sawa Mkuu,Ukomunisti ndo una tabia ya kukita mizizi kila kona.. kwenye idara zote za elimu, ulinzi, sanaa... nk.
We hujiulizi... wasanii asilimia 98% ni CCM, walimu wa vyuoni, vyombo vya usalama, halafu unasema nisikiiete kwamba ni chama cha kikomunisti?
Proved,Sahihi kabisa....
Ccm ni mabepari uchwara japo walianzia kwenye ujamaa.
Kuna kitu tunaita kwa kimombo 'Non-partisan' ni maarufu sana kwenye siasa za magharibu, ikiwa na maana kwenye vyombo kama vya ulinzi na usalama, vinatakiwa viwe na hii principle ya kutoegemea upande mmoja...Sawa Mkuu,
Hakika najiuliza Wasanii gani? Manake kudai Wasanii karibu wote 98% naona kuna ukinzani hapo....
Vilevile uwepo wa Wanachama wa CCM katika sekta tofauti za Kiserekali, kwangu sioni kama hiyo hoja inaqualify Kuwaita CCM wakomunisti....
Define Komunisti unavyoelewa basi....
Halafu jibu hili....Au nionyeshe au uniambie ni Nchi gani zaidi ya China ambayo Haina Wanachama katika sekta hizo ulizozitaja
Unataka kusema kuwa hakuna Wanachama wa vyama vingine katika hizo sehemu ulizotaja?
Tuendelee
Je kujificha makucha kunakufanya uwe Mkomunisti?Ccm ni chama kujifichia makucha ya ufisadi ,Kama nadanganya fuatilia wote wajifanyao ccm kindakindaki ,utashangaa
Hilo swali lako mbona jepesi sana? Sikutegemea kuulizwa na wewe mtalaamHiyo mikutano ineruhusiwa na nani???... tukubali tukatae.. ukiona mpaka mikutano ambayo ipo kisheria inaamuliwa na matakwa ya CCM, wewe mpinzani utasemaje kwamba una ndoto za kuitoa CCM madarakani?
Hiyo mikutano ya kisiasa nanialiizuia? Na nani anairuhusu??..
Nijibu