Nimeipenda na kuitamani katiba ya Guinea

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Juzi kwenye taarifa ya habari DW saa 12 jioni walisema Mkuu wa Tume ya Uchaguzi wa Guinea amefariki dunia lakini alikwisha hukumiwa kwenda jela mwaka mmoja baada ya kuchakachua (kubadilisha) matokeo ya uchaguzi uliofanyika Juni 2010, na uchaguzi huo huko mbioni kurudiwa (pia: Mwananchi 15/09/2010, uk 13)

Hii katiba ni nzuri sana kwenye demokrasia ya kweli, pia inaonesha jinsi gani Guinea kuna uhuru wa mahakama. Ya kwetu inaminya demokrasia na kuhalalisha wizi, uchakachuaji, rushwa, umasikini, ufisadi nchini kwa kusema NEC wakitangaza tu matokeo ya mshindi wa Urais basi hakuna mahakama yeyote nchini ambayo itasikiliza malalamiko dhidi ya matokeo hayo. Jamani tumpe Dr. Slaa ili tupate katiba safi!!
 
Back
Top Bottom