Nimeipenda hii, sijui imeshafika huku?

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
173
Yuko wapi aliyemsafi CCM?


9c516874b7367b90471604f9fbda1a9b

Na Hilal K. Sued - Imechapwa 13 October 2010

VIONGOZI wasafi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanapatikana kwa nadra sana. Sisemi hawapo, la hasha! Wapo lakini ama hutengwa kwa kile kinachoitwa, “Huyu si mwenzetu” au huamua kujiweka mbali kwa kuogopa kuchafuliwa.
Kwa ujumla baada ya takriban miaka 50 ya kuwepo kwake, CCM imepoteza sifa ya kuwa na viongozi bora ambao misingi yake ilijengwa tangu nchi ilipojiondoa katika mikono ya wakoloni.
Utando huo wa viongozi umeshindwa kurutubishwa. Kilichobakia sasa, ni majigambo kwamba CCM ni chama bora, wakati machoni mwa wengi kinaonekana kimekumbatia mafisadi.
Hata tukikubali na kauli ya mgombea wake urais, Jakaya Kikwete kwamba “nchi haihitaji chama cha kuongoza kwa majaribio,” basi chenyewe ndicho kinachotakiwa kuondoka kwa kushindwa kutimiza majaribio ya kuongoza.
Kwa miongo mitano sasa, CCM imeshindwa kuzalisha viongozi, badala yake inaongozwa na kikundi cha watu ambao wengi wao “si wasafi.”
Baadhi yao wanabeba tuhuma kadhaa za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Wengine wanafahamika hata kwa majina. Lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
Kutoweka kwa viongozi waadilifu katika uongozi wa juu wa CCM kumesababisha mmomonyoko wa maadili nchini na kasi yake inaweza kuwa ni ya kushangaza.
Kwa jinsi hali hii ya kulea ufisadi ilivyo, karibu taifa hili linakaribia nchi kama ya Zimbabwe ambayo inaongoza kwa uporaji wa rasilimali za taifa.
Ripoti ya utafiti iliyotolewa na taasisi ya Marekani ijulikanayo kama National Intelligence Council (NIC) inasema kutakuwepo nchi nyingi za aina ya Somalia – zitakazoshindana kujiendesha.
Ripoti hiyo inataja nchi kadha katika Afrika na Asia ya Kusini kwamba zinaweza kutwaliwa na mitandao ya kihalifu.
Dalili hizi zinaanza kujitokeza nchini kutokana na utamaduni mpya ambao CCM wameanza kuulea. Utamaduni wa kulindana ndani ya chama hicho ndiko kunazidi siku hadi siku.
Chukulia mfano wa tuhuma za uwindaji katika mbuga ya Loliondo, mkoani Arusha; kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi ndani ya Benki Kuu ya Taifa (BoT), viwanda na mashamba. Lakini nani aliyewagusa?
Baadhi yao wameteuliwa kugombea uongozi, ikiwamo ubunge, jambo ambalo linawapa fursa ya kuwa mawaziri.
Wako wapi wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo ilikubuhu kwa wizi? Yuko wapi aliyejipatia mlungula wa rada?
Ni ukweli usiopingika kwamba ufisadi ni mojawapo ya masuala ya kampeni zinazoendelea ingawa chama tawala kimekuwa kikijitahidi kulisukuma nje ya kampeni kwa kutumia visingizio mbali mbali.
Wanajaribu kuwazuia wananchi na vyama vya siasa kuzungumzia ufisadi katika kampeni kwa madai kwamba kufanya hivyo ni “uchochezi.”
Kinachobakia ni “usemaji wa hovyo,” usiyo na mashiko. Yumkini hakuna hatua zinazochukuliwa sasa wala baadaye.
Hata walengwa wa “uongo huo,” wanaamini kuwa wananchi ni mbumbumbu. Wanakubali kila wanachoambiwa na viongozi wa chama tawala. Hili ni kosa kubwa ambalo CCM wanalifanya.
Kwa mfano, angalia suala la ukodishwaji wa ndege za serikali kwa mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
Viongozi wakuu wa CCM wamejaribu kulifunika suala hili kwa kuonyesha stakabadhi za malipo ya ukodishaji. Hata hivyo, kila mwenye akili timamu anajua kuwa stakabadhi hizi zina utata.
Ndiyo maana, haikupita muda vyombo vya habari viliripoti kuwa hati hizo zilikuwa za kughushi. Walisema hati za Salma hazionyeshi malipo halisi, ikiwamo nambari ya kasma.
Hadi leo waliotoa hati zile, Mwenyekiti wa kamati ya kampeni, Abulrahaman Kinana hakurudi kwa waandishi wa habari kufafanua kasoro hizo.
Bila shaka hakuwa na hoja ya msingi ya kufanya hivyo. Hadi sasa, hakuna afisa wa mamlaka yoyote ya serikali aliyechunguza hati za Mama Salma. Je, nani mwenye ubavu? Atautoa wapi wakati chama chenyewe kimetopea katika ufisadi?
Angekuwa ni Profesa Mwesiga Baregu, mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndiyo ametoa hati hizo za kughushi, kabla hata ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari, serikali tayari ingepeleka afisa wake kuchunguza suala hilo.
Lakini ni kutokana na kile mtu anaweza kuita unafiki wa hali ya juu ndicho kilimsukuma Kinana kutoa kauli ya kupinga matokeo hayo ya REDET, akidai kwamba yamempunja mgombea wao – kwani angestahili kupata asilimia 88.
 
Kaka mi mwili wote umekufa ganzi kwa kuyasikia hayo, najua iko siku ambayo haina jina Mimi na wewe tutakuwa huru na zaidi ya yote kwa Mkono wa Mungu tutashinda.
 
Back
Top Bottom