Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,520
2,000
Siku tisini (90) baada ya kufungua Biashara.

Habari wana JamiiForums, leo nimekuja kwenu kupata maoni kuhusu mwenendo wa biashara yangu hii niliyoianza siku 90 zilizopita.

Nilifikiria kuanza biashara hii baada ya kazi niliyokuwa naifanya kufa. Wakati nafikiria kufungua biashara nilikuwa sina mtaji na sikujua nitaupata wapi lakini niliamua kutafuta wapi wanauza bidhaa hizo kwa jumla ili nikifanikisha kupata pesa nisiangaike kutafuta mzigo unapopatikana.

Badaye niliamua kuuza kiwanja changu kwa shilingi 2,000,000/= baada ya makato ya dalali na wakili (wakili tulichangia na mnunuzi) nikabakiwa na 1.9 ku-cut story short, nilikwenda kununua mzigo baada ya kulipia chumba, nauli, nilifanikiwa kuanza na mzigo wa 900,000+

Baada ya kufungua biashara nilianza kwa taabu maana wanasema mwanzo mgumu, lakini nilipambana nikawa kila shilingi ninayouza naagiza mzigo Dar, hivyo hivyo baada ya siku kadhaa mahitaji ya wateja (wanaoulizia) bidhaa fulani ikawa kubwa ikabidi nitafute sehemu nikope pesa niongezee mtaji nikapata 800,000 nikaongeza mtaji dukani.

Ikumbukwe kwamba hapa dukani sitoi matumizi zaidi ya matumizi ya kulihudumia duka kama umeme, mlinzi nk.

Hivyo mpaka leo siku tisini nimeingiza faida ya 1,092,600/= .

Swali langu kwenu: Je, ninakwenda vizuri na biashara hii au napiga mark time tu?
 

The Salt

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
210
500
Ni biashara gani mkuu?! Maana hapa umetaja jinsi ulivyoanza biashara na ulivyoingiza faida, ila hujataja ni Biashara gani, umeifanyia mkoa gani.

Ili hata wadau wanaotaka kujifunza kitu hapa waondoke na chochote ama wafanye kama wewe. Kama hutojali mkuu toa maelezo in details. Asante
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,404
2,000
Naomba nikupongeze kwa kukubaliana na hali ya kuishiwa kazi/ajira.
Na mtazamo wangu ni kwamba hiyo biashara ina faida na pengine nahisi inaendelea kukuwa.

Ikiwa umeweza kuingiza faida ya laki tatu kwa mwezi kwenye mtaji usio zaidi ya 1.5 million, nadhani unaendelea vizuri.

Pia nakuona ukiwa mwenye nidhamu sana na pesa, na hii itakufikisha mbali na ufanikiwe zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,520
2,000
Naomba nikupongeze kwa kukubaliana na hali ya kuishiwa kazi/ajira.
Na mtazamo wangu ni kwamba hiyo biashara inafaida na pengine nahisi inaendelea kukuwa. Ikiwa umeweza kuingiza faida ya laki tatu kwa mwezi kwenye mtaji usio zaidi ya 1.5 million, nadhani unaendelea vizuri.
Pia nakuona ukiwa mwenye nidhamu sana na pesa, na hii itakufikisha mbali na ufanikiwe zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana Mkuu kuna wakati Nilidhani nafanya mchezo tu lakini kumbe ninapiga hatua ipo hivi

Nilikua nafanya kazi ofisi moja kwa mwezi nilikua nalipwa laki moja tu imagine japo kulikua na deals za hapa na pale lakini ilikua hailipi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom