kokudo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 2,546
- 1,662
Siku tisini (90) baada ya kufungua Biashara.
Habari wana JamiiForums, leo nimekuja kwenu kupata maoni kuhusu mwenendo wa biashara yangu hii niliyoianza siku 90 zilizopita.
Nilifikiria kuanza biashara hii baada ya kazi niliyokuwa naifanya kufa. Wakati nafikiria kufungua biashara nilikuwa sina mtaji na sikujua nitaupata wapi lakini niliamua kutafuta wapi wanauza bidhaa hizo kwa jumla ili nikifanikisha kupata pesa nisiangaike kutafuta mzigo unapopatikana.
Badaye niliamua kuuza kiwanja changu kwa shilingi 2,000,000/= baada ya makato ya dalali na wakili (wakili tulichangia na mnunuzi) nikabakiwa na 1.9 ku-cut story short, nilikwenda kununua mzigo baada ya kulipia chumba, nauli, nilifanikiwa kuanza na mzigo wa 900,000+
Baada ya kufungua biashara nilianza kwa taabu maana wanasema mwanzo mgumu, lakini nilipambana nikawa kila shilingi ninayouza naagiza mzigo Dar, hivyo hivyo baada ya siku kadhaa mahitaji ya wateja (wanaoulizia) bidhaa fulani ikawa kubwa ikabidi nitafute sehemu nikope pesa niongezee mtaji nikapata 800,000 nikaongeza mtaji dukani.
Ikumbukwe kwamba hapa dukani sitoi matumizi zaidi ya matumizi ya kulihudumia duka kama umeme, mlinzi nk.
Hivyo mpaka leo siku tisini nimeingiza faida ya 1,092,600/= .
Swali langu kwenu: Je, ninakwenda vizuri na biashara hii au napiga mark time tu?