Nimeingia choo cha kike .... part 8 (Mwishooo, nipeni pole!) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kike .... part 8 (Mwishooo, nipeni pole!)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Mar 28, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Inaendelea toka part 7

  "Sikuachi ng'oo, hata ufanye nini" Meseji ilisomeka hivyo. Sikumbuki nini kilinipata baada ya kuisoma. Tulikutana kazini tena, lakini hali yangu ni wazi ilidhoofu. Rafiki yangu Katunzi alikuwa akipita mara kwa mara na kunifariji huku akikisisitiza ni lazima kumpiga chini yule binti. Kimawazo sikupenda kufanya hivyo ila kwa shinikizo la Katunzi na matatizo ya kiafya ya huyu dada kwa sehemu ndogo sana nilianza kutekewa na mawazo ya rafiki yangu.

  Baada ya kama wiki hivi, nilipita nyumbani kumjulia hali. Nilimkuta amechangamka mno na tuliongea mengi sana. Alikumbushia mpango wa kufunga naye ndoa. Nilijikaza na nilimwambia kuwa anipe muda wa kujipanga. Ingawa mawazo ya Katunzi yaliniteka, niliona muda ule haukuwa sahihi sana kumweleza ukweli kuwa wazo lile nimelipiga chini.

  Jioni tuliagana vzr na kuondoka kurudi nyumbani. Nilipofika nyumbani tu, sms iliingia. Nilipoisoma ni Angel, alilisitiza kuwa lazima nimpe jibu siku hiyo hiyo. Kwa uchungu nilijikaza na kuamua kumpigia kuogopa ushahidi wa meseji. "Angel, hbr za muda?" "Nzuri, umepata sms yangu?" "Ndiyo, na ndiyo maana nimekupigia" Nilimjibu. "Angel unanipenda?" Nilimuuliza kwa utani. "Ohhh sana wewe tena!" Alinijibu. "Nikikuomba kitu unaweza kunikubalia?" "Wewe tena, chochote nitakuapatia, ili mradi kiwe ndani ya uwezo wangu" Alijibu. "Ok asante, naomba tusifunge ndoa …!" Nilimwambia huku moyo ukinidunda. Nilisikia simu imekatika, na nilipojaribu kumpigia tena haikuwa hewani kabisa.
  Baada ya masaa matano, ningali nikiwaza , simu iliita kwa namba nisizozijua. "HorsePower?" "Nikusaidie nini?" Nilijibu. "Naitwa Monica, Angel amelazwa, Marie Stopes, Amekunywa sumu, na aliacha ujumbe ulioandikwa namba yako ya simu" "Mwee sauti ilinitoka, NIMEINGIA CHOO CHA KIKE , ninakwenda jela hivi hivi najiona!" Ghafla nikaanguka na kuzimia"

  Nilipozinduka nilijikuta niko na Angel mwenyewe. Sijukufahamu alifikaje nyumbani kwangu. Ila Angel, aliniangalia kwa huruma sana, akaniinamia. "Pole sana, HP" Aliniambia kwa Upole. "Majibu yako, yalinifanya nikose tumaini la kuishi duniani" "Kimbilio langu na tegemeo langu lilikuwa ni kwako" Aliongeza. "Kama unavyofahamu mimi ni yatima, niliyezaliwa pekee yangu. Wazazi wangu walifariki kwa ajali ya gari siku chache baada ya kurudi toka Uingereza nilikokuwa nasoma" "Sikuwa na ndugu wa karibu, kunifariji. Maisha yangu yamekuwa ni ya upweke sana ingawa niliachiwa magari na nyumba kadhaa hapa mjini. Kabla ya kifo chake, mama yangu alinisihi niwe mwangalifu nikiona wakati wa kuolewa umefika. Wanaume wengi hawana upendo wa kweli. Huwatumia wanawake na vile walivyonavyo kwa maslahi yao binafsi. Hivyo mimi ilinilazimu kuchukua njia ngumu kupima pendo lako kwangu. Sina HIV wala UKIMWI na wala sijawahi kuwa na boy friend, lilikuwa changa la macho tu kupima level ya upendo wako kwangu. Na kwa taarifa yako sikunywa sumu, nilikufanyia kamchezo nikiwa nyumba jirani karibu na kwako na ndo maana baada ya kuzimia, nikakuwahi kukuokoa. Kwa kifupi, nakupenda sana, na najua unanipenda sana na pia nilipenda niwe mkeo. Lakini nimegundua mambo mengi, Kwanza HorsePower una upendo wa dhati, lakini hujiamini, Pili una moyo wa huruma lakini ni mtu unayeyumbishwa na marafiki. Kwa hivyo nimeshindwa mimi. Ila napenda uendelee kuwa kaka yangu wa karibu. Asante kwa kampani yako na pole kukupotezea muda wako kwa kipindi chote hicho. Asante na kwa heri." Aliingia kwenye gari yake, akawasha na kuondoka. Kwa mbali niliona mwanga hafifu wa indicator za gari yake akiomba kuingia main road na kutoweka machoni pangu.

  Wakati ananiambia mambo yote hayo sikuweza kujibu hata moja. Niliishia kupigwa na butwaa na kushangaa huku nikishuhudia ndege wangu akipeperuka mikononi mwangu. Sikuelewa kwa nini aliamua kunipima kwa njia ngumu kiasi hiki. Nilijiuliza, ni kwa nini alitumia udhalimu kunipima? Kipimo gani hiki unaweza kukitumia kupima upendo wa mtu? Mbona amenitenda kwa kipimo kisicho sahihi? Kwa nini hakufungua moyo wangu na kuuchungulia badala ya kutumia kipimo cha nadharia? Niliona wazi wazi hali yangu ya upweke ikinirudia tena. Kwa takribani miaka mitano nilikuwa sina mahusiano na mwanamke yeyote baada ya niliyekuwa naye kunitenda mabaya. Na sasa huyu naye niliyempenda sana, akanipenda, baadaye kushindwa kuprove upendo wangu kwake, ananiacha nilirudi kwenye mateso yale yale ya zamani. Nachukia kupenda mimi. Sina Bahati mimi! Siwapendi wasichana, wananitenda mabaya. Nakiri udhaifu. Nakiri kutokupendwa na wadada. Nakiri kutokuwa na mvuto kwa wadada. Nakiri kushindwa kuwaelewa wadada. Ni dada gani tena atakayejitokeza kumpenda HorsePower? Wadada wa MMU msinisahau, naomba faraja yenu. Hali yangu ya upweke, naomba inirudie tena. Niendelee kuwa Senior Lonely Bachelor. JF sintawaacha kwenye hali ya kuwashauri ktk mahusiano, sipendi yaliyonikuta yawakute na nyie pia. Nawapenda sana! MMU wote, Wish me lucky ktk ukurasa wangu mpya wa maisha ya Upweke. Msinionee huruma, niacheni hivi hivi!

  Na log off ….

  Ni mimi HorsePower Kufakunoga,
  Katika dimbwi la Upweke,
  TRUE STORY-March 2012
   
 2. LEARNED BROTHER

  LEARNED BROTHER JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 322
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Thanks Hp for your good story, I like it..
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Thanks ...
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  i see.......................
   
 5. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  HP,brilliant if it is fiction but if it is based on true story of yours,am sorry for what happened to you.Leaving you citing that that you were not strong enough as one of the reasons was a mistake.Hakuna mtu perfect bana,udhaifu wako ulikuwa mdogo sana kulinganisha na majority ya mtu anemtaka yeye.

  Kama nihivyo hujaingia choo cha kike kwani huna sababu ya kuwachukia wanawake unless labda kwa yule wa kwanza ambae hatujui alikutenda nini.

  Kama nilivyosema kama ni fiction,ni story nzuri sana kuandika na kuisoma lakini kama yalikukuta kweli nakupa pole sana.Lakini tusichukiane,wanaume kwa wanawake kwayale mabaya tunayotendeana,inauma kweli kutendwa,ila tusamehe baada ya makovu ya kutendwa kupona.

  Umetufundisha mambo fulani katika story yako,lakini mawili makuu ni kuwa na upendo wa kweli na pili tunachaguaje watu wa kuwa nao katika maisha yetu(kuoa/kuolewa) ili kupunguza yale ambayo yanatukuta kila siku ndoa kuvujika nyingine kabla ya hata kufungwa.
  Niliweka thread moja hapa ya kipande cha maisha yangu kabla ya kuoa na regrets nilizokuwa nazo na ilikuwa na maswali kadha yanayoshabiana na hii story yako lakini haikupata michango ya maoni ya watu wengi.Ulichangia kitu fulani katika hiyo thread nakumbuka,inaitwa .....she wasn't a girl........she was not yet a woman.Inahusika sana katika hii story .

  Asante sana tena HP,mungu akubariki.
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole sana..........!
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145

  Thanks kikungu.
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,727
  Likes Received: 8,292
  Trophy Points: 280
  mh..TRUE STORY??! kaka inabidi ukaoge maji ya bahari...yule...huyu..ila huyu naye msanii sana...anafanyia maigizo kwenye maisha yako, inabidi ukamdai malipo...
   
 9. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  mkuu umekubalije yaishe kirahisi hivyo ? hakyamama ingekuta ni mimi nisingekubali kirahisi. embu ni pm namba yake na mimi nikatupe karata yangu.
   
 10. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nani aliyekwambia kuwa mapenzi yanalazimishwa? Kumbuka asiyekubali kushindwa, si mshindani!
   
 11. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  pole bana.
   
 12. R

  Raia Safi Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 13. R

  Raia Safi Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fanya ibada kaka utapata mafundisho mema,una jini mahaba dawa pekee ni kuwa mchamungu! Pole sana kwa yalokusibu
   
 14. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade HorsePower nimewahi kusoma visa vingi sana lakini hiki kisa chako kimeniongezea uwanja mpana zaidi wa kujua mambo asante sana Comrade kwa ajili yetu na wengine usiache kuwa jirani nasi tena wana jf tena na tena thanx comrade.
   
 15. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Jini mahaba ni kitu gani na anaingiaje hapa? Sina taratibu za kuamini na kushiriki ktk mambo ya majini
   
 16. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 818
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  nigukua na uwazo ningekupatia tuzo ya msimulizi bora MMU
   
 17. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145

  Mkuu tuzo kama ipo unaweza kutoa tu, hata kwa VodaPesa au airtel money!
   
 18. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nice story. . but kama ni kweli! usikate tamaa mfuatilie tena. .
   
 19. G

  GENDAEKA Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nn imeisha hivo?w endelea kutujuza,isiwe mwisho tujue nn kitaendelea hasa namna wasichana wanavyo wapima wanaume
   
 20. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  HP

  What a Good story

  Inafundisha sana

  Nilitamani kuuona mwisho wa hadithi, Kumbe ulimpeperusha ndege wako kwa kuogopa ukimwi

  Labda nikukumbushe Tu kwamba Kina cha maji hakipimwi kwa Macho

  USHAURI; Rudi kwa umpendaye na umwangukie kisha UBADIRIKE, BE YOUR OWN

  Big UP, It is a Good Story, I like it
   
Loading...