Nimeingia choo cha kike ...... (2) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kike ...... (2)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Feb 17, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sifa zake za utulivu na tabia njema zilizagaa kwenye shirika letu hili lisilo la kiserikali. Nilishawahi kusikia vijana wenzangu mara kadhaa wakimsimulia binti huyu kwa jinsi alivyo na misimamo thabiti ya kimaisha na kuonyesha tabia njema. Ingawa mimi binafsi si mtu wa kuendekeza wanawake na si mpenzi wa kampani za wanawake, lakini kwa urembo wa huyu binti dalili zote zilionyesha kuwa naelekea kuvunja msimamo wangu.

  “Angel, pliz naomba unisubiri!” Niliropoka bila kujifahamu. Hakuniskiliza wala kunijali, alionyesha kuvuta hatua ndefu na za uhakika kulielekea gari lake alilolipaki pembezoni ya ukuta wa ofisi yetu. Huwezi amini, sikukata tamaa, niliamua kumfuata nyuma kama fisi anavyofuata mfupa mpaka pale kwenye gari lake!

  Kitendo cha kumfuata nyuma kilinifanya niweze kuuona uzuri wake katika angle tofauti tofauti. Alikuwa binti mrefu, maji ya kunde, sura ya kuvutia na mwenye umbo la namba sita. Kwa haraka sana niligundua kuwa alikuwa na kifua cha wastani kilichoshiba nanihii vizuri. Pia alikuwa na kiuno maridadi na chini yake kidogo sehemu ya nyuma mweee siwezi kusema zaidi, nilihisi mapigo ya moyo yakiongezeka! Nilishusha macho chini na kukutana na miguu ya bia iliyoshiba vizuri, hatua zake za uhakika ziliuteketeza kabisa moyo wangu, nilijihisi nimehama hii dunia kwa ghafla, na kuhisi aliyeko mbele yangu ni malaika wa ajabu! Kumfuata kwa hizo dakika sekunde chache tu tayari nilikuwa nimeburudika vya kutosha.

  “Nikusaide nini HP?” Aliuliza huku akiwasha RAV4 yake short chases. “Nahitaji kuongea na wewe” nilizungumza kwa kujiamini. “ Wewe umechanganyikiwa nini, hebu acha utani wako tuko kazini, bwana!” Aling’aka. Kwa kifupi HP ni king’ang’anizi sana na huwa hakubali kushindwa kirahisi. “Nakuhitaji Angel wewe ni malaika hivi hujioni?” Niliropoka. Sielewi mdomo wangu alikuwa na nini siku ile! “Ok at the moment naelekea PPF Tower kuna document napeleka, ila kwa kukuheshimu nifuate naenda kukusubiri Sweet easy, Masaki karibu na Coco Beach” Alinong’ona. “Sawa” Nilijibu. Hakupoteza muda aliweka “Drive” akachia breki gari ikaondoka.
  HorsePower Kufakunoga ndiyo jina langu halisi. Wafanyakazi wenzangu wengi hunitafsiri kama kijana mpole, nisiye na maneno mengi na mtulivu. Kwa umbo ni mrefu, mweusi, na si mwembamba, ila najiamini sana. Mara nyingi hupenda kuongea na watu, lakini kwa uangilifu sana, sifa ambayo iliwafanya wafanyakazi wenzangu wengi wapende kuja kuomba ushauri kwa mambo mbali mbali yanayowatatiza mara kwa mara. Miongoni mwa hao ni huyu binti, ambaye kwa leo nimejikuta nikimuona kwa utofauti sana, kama malaika au kiumbe ambacho hakika kilistahili kuishi katika nchi hii ya maskini yenye mafisadi wa kila aina.

  Aliponiambia nimfuate, sikuhitaji kupoteza hata sekunde moja kwa nafasi hii adhimu niliyoipata. Nami kwa mwendo wa haraka, niliingia kwenye Toyota Verossa kana kwamba nafukuzwa! Nilichomeka funguo, nikajaribu kuwasha gari kwa haraka!
  Kanyinyi nyi nyiiiiiiiinyiii ni mlio uliotoka toka kwenye injini ya gari yangu bila kuonyesha dalali zozote za kuwaka. Nilijaribu kama mara tatu bila mafanikio. Walinzi walikuja mbio na kunizunguka, “Boss pole sana, unajuwa tuliosha gari yako mpaka kwenye injini, inawezekana maji yameingia kwenye ….” Acheni ujinga nyie, niliropoka kwa jazba. Nani aliwambia muoshe mpaka huko?” Katika kipindi hiko nilisahau kabisa kuwa mimi ndiyo niliwapa maelezo ya kuwa wanaosha gari nzima mpaka kwenye injini kila wanapoona kuwa gari ni chafu. “Lakini Boss si ulitupa maelekezo wewe mw …” aliitikia mmoja “Nyamaza nilimkatiza kwa hasira ….” Mpaka hapo nilihisi kuwa ndege wangu tayari ameshaota mabawa!

  Ghafla message iliingia kwenye simu yangu. Nilipojaribu kuifungua shabaaashiiii …… Ni Angel, hofu ilinipanda! Ilisomeka: “HorseNguvu nimefika tayari, I hope within 5 minutes utakuwa hapa, ninaharaka sana na nimekuheshimu kukubali wito wako na I hope utaheshimu na kuuthamini muda wangu pia. Angel”. Presha ilipanda, nikaisikia pia ikishuka na kwa mara ya kwanza nilijihisi kumkosea huyu binti kwa kutoweza kufika ndani ya dk 5, na kuhisi kupoteza nafasi ya wazi!

  **** naingia kwenye kikao mara moja halafu nakuja kuwamalizia hii stori nikitoka. Samahani kwa usumbufu! ******
   
 2. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  So far riwaya yetu inazidi kuamsha udadisi.Good umepangilia vizuri.
   
 3. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  haya HP verossa imehalibu pozi lol
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  mmh! Malaika anapepea hivi hivi naona...nasubiria part 3, stori imetulia!
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ungeenda Plan B hapo kijana...
   
 6. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Sasa HP unasubiri nini kuomba nafac kwny magazeti ya udaku uwe unatunga hizi riwaya pendwa,fanya fasta uwacliane na Shigongo ujipatie ulaji maana una kipaji cha kutunga riwaya za mapenzi.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Na ulivyo bahili huwezi kuita taxi! "Stood up" is a very bad beginning douwg!
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  tatizo lako una haraka sana, subiri usiwe na papara utajuwa nini kilitokea!
   
 9. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Dah HP unazidi kutufurahisha asee, vipi kitabu lini?
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nasubiri..
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Aiseee, ngoja niangalie uwezekano wa kupiga collabo na Shigongo huenda nikaambulia chochote!
   
 12. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  loh! hadithi tamu ss unavyoirigishia mmh!
  haya twasubirii!
   
Loading...