Nimeibiwa kwenye account yangu ya benki?

kussy

JF-Expert Member
Jun 15, 2010
400
121
Jumamosi nimetoa pesa kny ACC yangu kupitia ATM NBC kwa kutumia TEMBOCARD VISA yangu, jana nataka tena kutoa pesa kwenye Akaunti ATM ikasema sina hela kwenye ACCOUNT wakati nina hela za kutosha, leo nimedamkia kwenye tawi langu la CRDB, Counter wanadai hiyo hela iliyopotea imetolewa kupitia Bank ya EXIM, wanadai itakuwa imeibiwa wakaniambia nijaze Claim form alafu nifuatilie, but hawajui kama nitalipwa. Jamani hii imekaaje?
 
pole sana ndugu ..... hela inatolewaje kwenye account yako bila idhini yako .... au ulijisahau na password yako mtu anaijua
 
NMB ni wezi haijapata kutokea? Ukitumia ATM Machine umekwisha. Na hao watu wa claim wana majibu ya kunya haijawahi kutokea.
 
Pole sana Mkuu,hiyo inabidi utoe taarifa polisi pamoja na maelezo uliyopewa bank.Polisi kuna kitengo kinachoshughulika na wizi wa pesa kwa njia ya mtandao watakusaidia.
 
Pole sana Mkuu,hiyo inabidi utoe taarifa polisi pamoja na maelezo uliyopewa bank.Polisi kuna kitengo kinachoshughulika na wizi wa pesa kwa njia ya mtandao watakusaidia.

Polisi gani hii hii ya afande Mwema? wewe kama unataka kupoteza hela yako zaidi nenda!!!:wave::wave:
 
pole sana. je umejiunga na sim/ internet banking?????????????? na kama jibu lako ni ndio, then probably kuna mtu ameijua password yako then akaitoa thru cyberspace. ukiangalia vizuri terms za sim/ internet banking utakuta clause inayosema kuwa ukiibiwa sio liability ya CRDB kwa hiyo wao kukulipa is very unlikely.

what we need nowadays is cyber auditors and cyber PIs, watu watakaoweza kufuatilia trail of money electronically from a source to the final destination. wenzetu majuu wanafanya sana haya mambo. once you join the internet banking services, money transfers can be made by simply clicking on a mouse or via a handset so it is very crucial to keep your passwords complex and well protected.
 
wafanyakazi wa bank wanatuibia sana kule songea NMB kuna mfanyakazi ameingia mitini baada ya kubainika kuchota pesa kwenye acc za wateja hasa wenye pesa nyingi.
 
mkuu muone branch meneja fasta! Customer care zetu ovyo, utapoteza muda mwingi na hela hutaipata kama huja muona meneja! Ila Tembo card ni nbc kweli? Sio crdb?
 
Tembo card ni za crdb lakini unaweza kutolea atm za nbc zenye visa.

mkuu muone branch meneja fasta! Customer care zetu ovyo, utapoteza muda mwingi na hela hutaipata kama huja muona meneja! Ila Tembo card ni nbc kweli? Sio crdb?
 
usikubali benki wana namna ya kujua nani ametoa hata kama imetolewa kupitia exim mtu aliyetoa anajulikana mwone meneja wa benki waexpose kwenye vyombo vya habari ili watu wote wajue hiyo benki haiaminiki tena kutunza pesa za wateja hakikisha unafatilia hadi mwisho lazima pesa yako irudi
 
Acha kuzngua kijana..from bank point of view,there is no such a think...itakua mtu wa karibu yako ambae he/she knows your password alitumia kadin yako kutoa pesa and nothing else
 
Crdb sio benk kabisa sikuhizi...mimi nilitumiwa pesa kutoka nje ya nchi, ikawa imekosewa namba moja ya akaunt ila information nyingine zote sana, huwezi amini ile hela ilikaa takriban wiki moja wameihold, sasa sijui waliiweka akaunt gani manake kwangu haikuingia na wala hawaku irudisha ilipotoka yaaan mpaka kuna mtu namfahamu kitengo kimoja ndio akanisaidia.....swalli linakuja, je kkama aliyekuwa anatumiwa hizo pesa anamawasiliano na watumaji si inaamaana wafanyakazi wahusika wanazikamua?????kwahiyo ndugu yangu nenda kwa manager na kama vipi toa kwenye vyombo vya habari....
 
Mbona tuhuma za CRDB zinazidi kuwa nyingi, inawezekana kuna sehemu wamezembea, wanataka tuhame?
 
Apart from ma experience ni kwamba, hiyo fedha fanya kama umetoa sadaka, kwa sababu hiyo claim waliyokuambia uandike utafutailia hata miaka minne na hupati fedha. Nilitoa fedha kwa kutumia visa card ya CRDB kwenye atm ya NBC pale Dodoma mwaka 2008, lakini nilipokuja kuangalia salio niliporudi Bongo nikakuta kama laki 2 hazipo, then nikafuatilia, da! ebwana enhee, nikafunga na akaunti yangu kwa hasira, maana kila siku wanakuambia njoo kesho!
 
Acha kuzngua kijana..from bank point of view,there is no such a think...itakua mtu wa karibu yako ambae he/she knows your password alitumia kadin yako kutoa pesa and nothing else

Aisee sizingui mtu, nafikiria kufunga Account kabisa sasa
 
Una accouny CRDB --> umetoa hela kupitia ATM ya NBC --> then umeambiwa hela iloibiwa imetolewa Exim Bank --> then wanakuvunja moyo kwa kukwambia kuwa hawajui kama utalipwa!!! SUE THEM!!! Hawa CRDB customer care yao ni mbovu kupita kiasi, wanamajibu ya kunya, wanajiskia, hawajui kuhudumia wateja kabisa, ni wajeuri, siku nikiwa kazini akija mfanya kazi wa CRDB akitaka huduma nampuuza na kumpa majibu ya kunya kuliko ya kwake!
 
usikubali benki wana namna ya kujua nani ametoa hata kama imetolewa kupitia exim mtu aliyetoa anajulikana mwone meneja wa benki waexpose kwenye vyombo vya habari ili watu wote wajue hiyo benki haiaminiki tena kutunza pesa za wateja hakikisha unafatilia hadi mwisho lazima pesa yako irudi

Kwa hlo usitegemee,ma benki ni wateja wa vyombo vya habari that means banks pay a lot thru ads on these media so hawatatoa hyo hbar kwenye vyombo vyao.
 
Jumamosi nimetoa pesa kny ACC yangu kupitia ATM NBC kwa kutumia TEMBOCARD VISA yangu, jana nataka tena kutoa pesa kwenye Akaunti ATM ikasema sina hela kwenye ACCOUNT wakati nina hela za kutosha, leo nimedamkia kwenye tawi langu la CRDB, Counter wanadai hiyo hela iliyopotea imetolewa kupitia Bank ya EXIM, wanadai itakuwa imeibiwa wakaniambia nijaze Claim form alafu nifuatilie, but hawajui kama nitalipwa. Jamani hii imekaaje?
Fuatilia hela yako kwa kuweka kumbukumbu za maandishi, hizi ndiyo kesi ambazo tunazisubiri sisi wanasheria ili kuziwajibisha benki mahakamani...wakiendelea kukuzingua wasiliana na wakili yeyote aliyejirani akusaidie kufungua kesi ya madai watakulipa na usumbufu woote, pesa ikiibiwa kwenye akaunti aliyeibiwa ni benki wala sio mteja.
 
Back
Top Bottom