Nimehamishiwa Arusha, nitegemee kuona tofauti gani?

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
508
962
Wanajf!!

Nimepata uhamisho wa kikazi kutoka jiji la Dar kwenda Arusha Jiji, na niweke wazi kuwa sijawahi kufika Arusha (hivyo sijui kabisa maisha ya Arusha)

Nitegemee kuona (Experience) tofauti gani kati ya miji hii miwili?

Tofauti zozote zile katika nyanja zote za maisha ya binadamu.
 
Sijawahi ishi Arusha, mara nyingi huwa napitapita.

Naweza lala siku moja au mbili au tatu kisha nduki.

Kwa ninavyowauliza wenyeji wanasema maisha Arusha yapo juu sana ukilinganisha na Dar-es-Salaam
 
arusha na dar tofauti yake kubwa ni hali ya hewa, labda na lafudhi, pia kuna unywaji mkubwa sana wa pombe na kutafuna mirungi, kuvuta sigara na bangi
arusha kila duka linauza viroba na wanapanga hadi mezani barabarani kuuza viroba na big G

wameru pia ni wagomvi
 
Kuna vumbi pia
 
Hali ya hewa ni kinyume kamili cha unakotoka. Nyumba za kupanga ni expensive sana. Katika Kila vijana watano unaokuta wamekaa sehemu mmoja ama wawili utaona anatafuna mirungi. Rafudhi ni kama za kikenya kiswahill Chao kinataka kufanana na cha Nairobi. Mara nyingi utapewa jina la "chaliii angu". Utafaidi nyama choma ni wataalamu sana was kuchoma nyama na nyama yao mara nyingi ni nzuri sana. Kuna ujambazi sana. Vibaka was kukuvamia nyumbani wakitaka Mali zako ni wengi. Hali ya hewa utaipenda ni nzuri sana kwani hakuna siku utajiskia kulala barazani. Maisha yako juu kuliko Dar. Vyakula bei ghali.
 
1.Arusha gharama za maisha zipo juu ukilinganisha na Dar,
2.Arusha ipo baridi mno ukilinganisha na Dar,
3.Arusha hakuna foleni kuuubwa barabarani ukilinganisha na Dar,
4.Arusha kila mtu m-babe na hutembea na silaha kama si Bastola basi pisipisi ama kisu.
5.Arusha hakuna panya road kwa hiyo na hatawakitokea hawatakimbiwa watapigwa tu.
6.Arusha kuna mamilionea wengi sana na huwezi mdhania ukikutana nao road so heshimu kila mtu.
7. Arusha hakuna discipline barabarani ukiwa una-drive so unabidi na wewe ukomae nao.
8.Ntarudi tena....
 
Labda jiandae kuona mabilionea sasa, maana nasikia kila mwenye kausafiri ni bilionea huko. Wakati hapa Dar ni ya mkopo!!
 
Arusha sio lelemama,sisi ambao tunaishi huku ndio tunajua. Kila mtu ni mbabe hata mtoto ila utambue kuwa maisha yako juu tofauti na dar. Hali ya hewa sio mbaya sana kuna msimu wa baridi June mpaka October,halafu joto lenye nyuzi 25° lakini pia mjini sio mkubwa kama dar yaani mjini ni nusu saa umemaliza. Ukitaka kujua zaidi utanifuata private
 
Wanajf!!

Nimepata uhamisho wa kikazi kutoka jiji la Dar kwenda Arusha Jiji, na niweke wazi kuwa sijawahi kufika Arusha (hivyo sijui kabisa maisha ya Arusha)

Nitegemee kuona (Experience) tofauti gani kati ya miji hii miwili?

Tofauti zozote zile katika nyanja zote za maisha ya binadamu.
Tegemea kuona watu wakila bangi na mirungi mbele ya polisi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom