Nimegandwa kama rubba

Nimegandwa kama rubba

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,487
Reaction score
6,517
Huyu ni mpenz wangu hasa tulianza mahusiano kama masihara tu eti siku moja alinialika nikaftari yeye ni daktari by profession wanaka nyumba za hospitali pamoja na wenzake asubuhi wanaingia job.

Siku hiyo baada ya kumaliza kuftari aliniharakishia niende msikitini kwa ajili ya sala ya Tarwehe kama kawaida nikaenda nilipomaliza nikarudi lakini moyoni najiambia huyu amenialika kuja kuftari halafu nilale hapa na kwenye hiyi nyumba lengo hasa ni nini?

Tukawa tumekaa pale ukumbini na madakari wenzake kike kwa kiume tunatia stori stori baadae kama saa 5 usiku ivi wakaeka chakula kwa ajili ya daku nikapiga daku then tulipomaliza kuna daktari 1 wa kiume nafkiri walishaongea na huyu ant kwamba baadae ukienda kulala mchukue mgeni wangu mukalale uko upande wa wanaolala madaktari wa kiume.

Jamaa gafla akaniambia twendezetu tukalale nikuonyeshe room yako, nikasema ok nikatoka kwenda kuonyeshwa room mzee nikaingia room kwa ajili ya kulala. Moyoni nikawa nafkiri mbona huyu ant hatujaongea chochote au ndio ni ftari tu basi. mara nikajikuta nimetoka mle ndani nikarudi kule kule nikagonga akafungua nikamkuta anamalizia kula kwenye meza na mimi nikakaa nikaanzae ndogo ndogo, akanambia yeye uhusiano hataki kabisa na mwaname mana aliwahi kutendwa hivyo hawezi kuumwa na nyoka mara mbili basi nikarudi zangu chumbani kwang kulala.

Lakini kule chumbani kulinipa hope kitanda kilitandikwa babkubwa then kapuliza perfume ile ya kimahabaa kwa mbali inanukia ikawa nalala lakini ukweli sijui lengo hasa la yule ant. amini usiamini siku ile karibu na alfajiri nilijipiga bao la nguvu nikachafua shuka.

Asubuhi kumekucha nina swaumu ant akanisindikiza barabarani nikapanda gari nikarud zangu.

Sasa kutoka siku hii ikawa nawasiliana naye namtongoza pole pole mpaka akaingia katikati akanipa moyo wake.

Sasa kuna siku nilimuuliza kwanini aliachana na huyo alokuwa mpenz wake akaniambia niliachana naye kwa sababu yeye alianza ishara za kutaka kunifanya mapenz hakuwa na nia nzuri na mimi sikutaka alinishika mkono wang siku moja nikauvuta kwa nguvu toka siku hiyo nikaachana naye nikajua hakuwa na nia ya dhati na mimi asingenishika mkono wang na kujaribu kutaka kunichezea.

Dah, baada ya kunipa kisa hichi nikajiambia inamaana bas hata mimi siwez shika shika mahali popote otherwise nitaachwa? nikajiambia sawa wacha twende pole pole tuone.

Unajuwa sisi wanaume kwenye haya mambo yetu tunatofautiana huyu dem nimeenda naye pole pole nikamkoleza kwenye mapenz mpaka ikawa twaogeleana sio kushikana twaogeleana ananikumbatia busu kama kawaida ingawa kula tunda hataki abadan.

Sasa mapenz yetu yalinawiri sana kwa kweli kuna siku huyu dem aliomba kusoma Nje ya nchi akapata kule kwenda kufanya degree miaka 4 sasa hapo katikati ikawa twasiliana kwa simu lakini mimi familia haikuniruhusu tena kusubiri miaka 4 ndio nishike ndoa.

Na hawa dada zetu wa siku hizi ukimgusia kumuoa kama ni msomi msomi wanakuwa hawataki mpaka eti wamalize kusoma nikamwambia sawa maliza kusoma.

Mimi akatokea mchumba mwengine katikati yake mambo yakanawiri na home wakanitaka lazima nilifanye hili jambo kwa sababu sikua na sababu tena kuendelea kusubiri kila kitu kilikuwa sawa nyumba na kaz Alhamdullah.

Nikaoa, na ukweli nampenda mke wangu.

Sasa huyu bibie kurudi akapata hizi taarifa za mimi kuoa akakasirika sana sana, unajua sana akawa analia namuonea huruma ukweli alichanganyikiwa lakini chakushangaza ni kwamba bado ameniganda kama ruba na sasa wake 2 si mudu kabisa kutokana na hali.

Naleta kwenu kwa ushauri.
 
Yaani katika vitu ambavyo vimenishinda nikuvumilia kuwa,katika mahusiano na, chick then niishie kumnawa tu..then papuchi asinipe
 
Mimi nikupongeze tu kwa kuoa mkuu hayo mengine maliza mwenyewe
 
Nakupongeza kwa kuongeza mke mwingine mkuu, ila usisahau vumbi la lubumbashi pembeni ya kitanda, maana wake wawili siyo mchezo brow.
 
Mwana umeandika refu ila point umeiweka mwishoni kabsa.

Sema fresh leo umenkuta niko na mood ya kusoma,nmeisoma yote

ila chakufanya hapo kabla hatujakushauri "fata ushauri wa moyo wako"

Mapenzi hayashauriwi Jombaa,ingekua biashara hapo sawa,we hapo sikiliza

moyo wako wazungu wanasema "listen your heart"
 
Msome kwanza akili yake.
Kama anaweza kuwa mke wa pili ongeza mke mkuu.
Na akili yako itachangamka.
Mke mmoja analaza akili mkuu.
Unajikuta akili yako inaishia kutafuta ada za watoto wawili tu.
Na ndio mwisho wako
 
Kwa namna ulivyoeleza ni wazi hauna mpango wa kuwa na wanawake wawili au zaidi, hivyo usilazimishe.

Na pia kwa imani yenu, mke wa pili na kuendelea sio kuwa ruksa hutoka kwa bi mkubwa?
 
Kuna bwana mmoja alikuwa na mke mmoja,kula anapambana sana ndio milo mi3 ikae mezani.Akamfuata mtume Muhammad (S.A.W)Mtume Muhammad akamuambia ongeza mke,Jamaa akaongeza mke.Maisha yakabana zaidi milo ikawa miwili tena kwa taabu.Yule bwana akaona Mtume Muhammad amemzingua akamfuata tena akamuambia shida zimeongezeka ya Rasullulahi,mtume akamuambia ongeza mke mwingine.Jamaa kwa shingo upande akaongeza mke,Hakuchukua round vyuma vikabana sana mlo mmoja tena wa taabu muda mwingine unakosekana kabisa,Akamuendea mtume akamuambia mtume maisha yamenishinda inabidi niache hawa wanawake nawatesa bure siwezi kuwahudumia.Mtume akamuambia ongeza mke,Jamaa akaongeza mke.Mkuu hupangi Riziki,mshauri umuoe mke wa pili,akikubali na wewe ukiridhia ongeza mke shekhe wangu,anayepanga riziki ni Allah S.W
 
Back
Top Bottom