Nimefungua insurance agency wadau

Nimefungua insurance agency wadau

ngawia

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
834
Reaction score
858
Baada kufanya kazi ya sales na kampuni za bima nimeamua kufungua insurance agency yangu ofisi zipo magomeni kagera na banana Ukonga top guide insurance agency mimi agent wa jubilee insurance ltd kwa wadau mliopo kwenye sector naomba tupeane mazoefu zaidi kuhusu masoko then mdau yeyote anetaka tufanye nae biashara au mwenye biashara anakaribishwa ani pm namba yake ya sim nitampigia tuongee.

Tunatoa bima za moto kwa nyumba,biashara waliopanga kwenye frem,bima za magari, bajaj, elimu, afya, bima za mazao kama mahindi, ufuta, shahiri, mtama, etc. Bima ya green house kwa wale wakulima wanaoanza kilimo na umeweka mtaji wako wote hapo. Ni muhimu ukaweka bima usije ukapotea, bima ya kuku wa mayai na wa nyama kwa wafugaji wa kuku wale vifaranga unawekea bima in case wakifa ugonjwa au wakiibiwa bima incoposate gharama ulizotumia mpaka pale walipokuwa wamekufa.

Nitaendelelea kutoa maelezo zaidi namna bima hizi mpya za wanyama na kilimo zinavyokuwa kwa sababu ni product mpya inayoingia sokoni kwa mjasiriamali kijana kwenye kilimo ni muhimu kuweka bima ili kufanya kilimo chako kwa uhakika. Bima itakopasate incase kumetokea ukame, mafuriko,mazao yameharibiwa na wadudu au wanyama na tetemeko la ardhi. Uzuri wa kutumia agency ni kwamba atakusaidia kufatilia kwenye kampuni pindi panapotokea claims ili ulipwe kwa wakati
Karibuni wadau
 
Ahsante mkuu nashukuru sana kama utajali naomba unipm no.yako ili nipate experience ya hapo manyara toka kabla sijafika hapo

mkuu nnami nataka kuingia kwenye biashara hiyo naomba mbinu za kuniwezesha.
 
Nataka kujua hiyo bima ya mazao inafanyaje kazi.
Nilima mahindi ekari 20 ukaja ugonjwa ukaniliza mbaya.
Vipi ningekua na bima ningeponea?
 
ngawia ....

bima ya mazao ipo kwa kifupi utajaza form maalumu itaotaka kujua ni heka ngapi, umelima wapi na kama ni kampuni ama mtu binafsi aina zao una wafanyakaz wangapi shambani, mbegu umenunua kias gani,umelima kwa sh ngapi, pia utatakiwa kujaza jina la mtalam wako wa kilimo, anayekushauri hasa kwenye dawa za magonjwa ya hilo zao utategemea kupata kiasi gani ukivuna na utauza kwa kiasi gani....then jumla hyo pesa utakatwa pre 4% ndio utalipa kama bima
 
Back
Top Bottom