Nakumbuka nilikuwa na Biashara na rafiki yangu, mimi ndio niliyevumbua ile Biashara nikamshirikisha na yeye, tukawa tunafanya pamoja, Mzigo tunapeleka wote, pesa ikitoka napokea mimi tunagawana sawa bin sawia, siku moja nilimuagizia yeye achukue ile pesa, kilichotokea !!? alitia ndani pesa yooote, niliamua kuiua ile Biashara na hatukuongea kwa mwaka 1, japo tulikuwa ofisi moja, Sikutaka Boss wetu ajue, lakini alihisi kuna kitu kinaendelea kati yetu, japo kulikuwa na maneno yakiendelea kwa kuwa mwanamke ambaye niliachana naye yeye akawa naye hivyo wengine walihisi hicho ndio chanzo cha ugomvi wetu, hii ilikuwa zamani kidogo.
Hii story inafanana sana na yangu. Mimi alifika kwangu mtu niliyemsimamia ndoa yake akaomba nimpe hela. Sasa nikawa sina za haraka muda ule na nilikuwa mbali kidogo. Tena alikuwa kwa njia ya kukopa. Sasa kulikuwa na mtumishi mwenzangu alikuwa anakopesha hivyo nikamtaka kama yuko tayari akope nitamdhamini. Nilimdhamini mwaka 2008 2,500,000 na akaahidi atarejesha ndani ya miezi mitatu. Hakurudisha ule mkopo, na simu akawa hapokei. Sasa ninataka nimweke hapa jamvini kwa kuwa ni msomi wa Chuo Kikuu alimaliza degree ya Uchumi mwaka 1996. Siku moja nikakutana naye ghafla maeneo ya bank alishtuka sana, na akaomba ohhh mara vile ngoja jumatatu ya pasaka nitafika. Na hajaonekana hadi leo. Deni sasa limefika zaidi ya 10m. Hawa ndiyo binadamu. Sasa kama anasoma humu, ninataka nimtoe hapa na picha yake na part ya mkataba ili wengine wapate adhabu. Na waajiri waliowaajiri waone jinsi walivyofuga majizi.
achana nae huyu, life will tell nakuambia!!!!!
Hii dhambi itamsumbua miaka yake yote
mkuu unanikumbusha miezi michache tu iliyopita mtu tuliyehusiana naye kama huyo mtu wako!!
Mke wake alikuwa anajifungua akaniomba nimkopeshe kiasi kadhaa cha fedha ambacho angerejesha wiki ambayo ingefuata,.
Yeye kama rafiki, jirani na kaka yangu isitoshe tumekulia wote kijijini bila hiyana nikampatia kiasi alichoniomba na kwa sababu mimi nilikuwa na shida pia ila nikampa yeye kipaumbele kwanza nikamuambia kwamba hizo hela nimeazima hivyo arejeshe mapema nimrudishie mwenyewe!!
Kila wakati ananipiga tarehe tuu,..
Mpaka leo hii takriban miezi sita imeshapita hapokei simu yangu wala
kujibu meseji!!
Kiukweli nasema wakati mwingine kuliko kumkopesha mtu bora umwambie hauna ili kuepuka usumbufu wa aina hii..
...ukiona manyoya ujue keshaliwa. mleta mada tuna RB? umeshakwenda ofisini kwa mwajiri wake? weka picha hapa tukusaidie kumtafuta. Vinginevyo tulia tu.
Sana tu. Kuna mtu alinizima 8m chaajabu nikampigia sim kumwambia kuwa nimemsamehe deni na nimemwachia mungu. Kwa woga wake akakimbilia polisi na kunishtaki kuwa nimemtishia maisha. Baada ya kukosa ushahidi akafuta kesi. Lakini hii leo anasota sana na sio mimi tu alinidhulumu, kumbe ni wengi na hicho ndo kinachommaliza. Jasho la mtu haliliwi bure bana.
Naunga mkono hoja lakini ukweli ni kwamba mazingira ya huyo jamaa ni ya kitapeli na nashauri wenzangu tuwe makini sana na marafiki wanaotaka kukukopa fedha nyingi kwa wakati mmoja kwa minajili ya madeal.
Hii akili ya Mungu atanilipia ndiyo maana hatuendelei. Yaani wewe mtu unamfahamu kakulia mkwanja wako wa maana halafu umwache tu?!!!!!achana nae huyu, life will tell nakuambia!!!!!
Hii dhambi itamsumbua miaka yake yote
Tumezaliwa kijiji kimoja, nimekuwa naye kijijini na nimesoma naye shule ya msingi, tuliachana tukiwa tunakwenda Secondary mpaka tunamaliza vyuo vikuu ambavyo tumesoma vyuo tofauti, tulikuwa tukionana pale kijijini mara chache sana wakati wa likizo mpaka tulipomaliza chuo.
Baada ya kumaliza chuo tulionana Dar katika mihangaiko ya kutafuta kazi, tulibahatika kupata kazi katika Taasisi mbili tofauti, yeye alipangiwa mkoani mimi nilipata nafasi hapa hapa Dar, ni zaidi ya miaka sita hatukuwahi kuonana face to face zaidi ya kuwasiliana kwa simu na kuchart kwenye mitandao.
Mwaka 2012 alihamishiwa kikazi hapa makao makuu ya Taasisi yao, kutokana na ukweli kwamba hapa mjini mambo ni mengi hivyo imekuwa ngumu sana kuonana mara kwa mara kwa masaa ya kutosha kiasi kwamba tunaweza tukastukiana kama kuna mabadiriko makubwa ya tabia baina yetu, tumekuwa tukionana mara chache sana tena sehemu za Starehe.
Mwezi July2012 alinishirikisha deal moja zuri sana lilikuwa la maslahi ya kutosha lakini, ilitakiwa nichangie kama Million15 ndani ya wiki moja, kutokana na hali yangu kifedha nilipigana sana ndani ya wiki hiyo ikaniwia ngumu kuikamata M15 hivyo nikalikosa lile deal nilisikitika sana.
Mwezi April 2013 miezi saba iliyopita ilikuwa ni jioni siku ya jumapili alinipigia simu kwamba yupo Mlimani City kuna transaction ya 2,500,000 anataka kuifanya amefanikiwa kutoa 800,000 lakini kadi imezama itabidi aifuate kesho yake asubuhi, akaniambia anahitaji hard Cash 1,700,000 za haraka haraka kama itawezekana vinginevyo atapata hasara kubwa, kiukweli ishu aliyoniambia ilikuwa ni lazima niamini, isitoshe ni mshkaji.
Kutokana na ukweli kwamba huwa ananisifia kwamba mimi ni 'ALWATANI' hapa mjini nililazimika kupambana ili ipatikane hiyo 1,700,000 nisimuangushe jioni hiyo hiyo japo mimi nilikuwa na 900,000 kwenye Akaunti yangu nikaongezea na 700,000 kutoka kwa mshkaji wangu aliye na duka pale Mwenge, then nikamkabizia.
Kesho yake asubuhi ya saa4 alinipigia simu kwamba wamepatwa na msiba wamefiwa na mfanyakazi mwenzao Ofisini yeye kateuliwa kuwa mmoja wa watu waliotakiwa kwenda Kilimanjaro kupeleka Maiti/Msiba, hivyo akadai akipata time atachomoka mara moja aende Benki arekebishe ule mzigo, siku hiyo hakufanya hivyo sikutaka kumsumbua sana nikasubiri arudi ila nikajitahidi kumalizana na mshikaji wangu wa dukani kwa kuhamishia deni kwa mtu mwingine, aliporudi toka Kilimanjaro akanishirikisha tatizo lingine, amekuwa akifanya hivyo kila ninapompigia huku akiniomba nimvumilie.
Siku zimekwenda miezi inakatika mpaka sasa nikimpigia simpati nahisi kani-Block, nikimpigia kwa simu nyingine anapokea lakini akistukia ni mimi ananikatia simu, hiki kitu kimekuwa kinanikera sana hakuna kitu kinachokera kama kukatiwa simu na mtu ambaye wewe unadhania ni rafiki yako.
Wadau nishaurini nimfanyeje huyu jamaa, ikumbukwe kwamba sina ushahidi kwamba kanidhulumu na kanisababishia usumbufu.
wa kujuta ni mbongo!!? Kwanza hapo anaona km jamaa mnoko wkt mali ya kwake..