illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Nimepotelewa na cheti cha kifo cha mzee wangu nikaelekezwa niende RITA, nakumbuka mara ya mwisho walikuwa pale Muhimbili kufika pale nikaambiwa wamehamia katikati ya mji karibu na ilipo kuwa Bilicanas nikaenda kufika pale nikakuta jengo kubwa zuri linabendera ya taifa na ile ya Africa mashariki, kilicho nishangaza nikakuta akina mama wengi wamekaa nje chini wengi wana watoto wadogo nikaenda kwa mlinzi kueleza shida yangu akaniambia niandike kwenye kitabu cha wageni kisha niende ghorofa ya kwanza kufika ghorofa ya kwanza hakuna pa kukanyaga watu ni wengi naamini wote wamefuata huduma.
Hakuna wa kumuuliza yaani watu wengi pale kwenye dawati lililoandikwa maulizo kuna watu wako bize na shughuli zingine wamezungukwa na watu utafikiri wakimbizi wanagombania chakula nikamuuliza mlinzi akaniambia nipange foleni nimekaa kwenye foleni dakika hamsini ilipofika zamu yangu nikaambiwa hii foleni ni ya watu wa mikoani kapange foleni pale ndio ilala na kama ni Kinondoni nenda wilayani pale Magomeni.
Kuna umuhimu wa kufanya settings za ofisi naamini mamlaka husika itatafuta namna bora zaidi ya kuhudumia wananchi nikikumbuka ilivyokuwa TRA miaka ile tuna kwenda kukata road license siku mbili mpaka tatu lakini siku hizi imekuwa zoezi la dakika kadhaa tu, siku hizi tunaandika kwa mujibu wa sheria mpya ya vyombo vya habari kueupuka "uchochezi"