Tatigha
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 1,957
- 2,022
Wakuu niliweka malengo ya kwamba, ikifikia mwezi wa nne mwaka huu niwe na mil 6, kwa ajili ya kuanza biashara ya kuuza vyakula vya majumbani kama vile nafaka za aina mbalimbali, mafuta ya kupikia, sukari, mikate na vitu mbali mbali na nimepanga kutafuta frem pande za tabata kwa sababu kule Kuna wakazi wengi naamini mambo yataenda sawa.
Sasa mimi shida yangu sijui chochote kuhusu hii biashara, kwa wale wazoefu naomba msaada wenu juu ya
1.ni nini kinahitajika ili kuweza kupata leseni ya biashara?
2.nasikia lazima uende tra wakufanyie makadirio ya kodi, napo ni vitu gani wanahitaji?
3.kuna ulazima wa kununua Efd machine kwa ajili ya risiti juu ya hii biashara ambayo ni ya Kawaida tu?
4.T-number inapatikana wapi? Na ili upate unapaswa kuwa na vitu gani?
5.kama Kuna kitu kinahitajika alafu sijakitaja naombeni muongezee wazoefu wa biashara
6.kama Kuna biashara yoyote tofauti na hiyo ya yangu ni ruksa kunishauri na ukizingatia mdogo enu niko chuo, nimeona Kuna ulazima wa kujipanga mapema kabla sijamaliza chuo, mambo yakuzunguka na bahasha sitoyaweza kwa kweli, kwa hiyo nikaona haka kamkopo changu nilichobahatika kupata pamoja na akiba zangu za nyuma nichanganye niweze kufanya kitu cha maana.
Karibuni wakubwa kwa wadogo