Nimechoka kupendwa!!!

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,550
Mpaka muda huu naandika huu uzi, bado sijajua kwanini mabinti wengi wananipenda hadi inafikia hatua ya kugombaniwa mbele ya mkadamnasi. Labda nianze kwa kukri kwamba mimi sina uwezo wa kiuchumi wwte ule maana mpaka sasa nakula, naoga, nalala nyumbani.

Labda sababu familia yetu ipo vzri, mmmh bado nakataa maana home maisha ya kubangaiza tu hata chuo sikumaliza kwa sababu ya kukosa ada.

Labda mimi ni handsome,...Ila napenyewe nakataa. Mi wa kawaida sana japokuwa ni mrefu, mwembamba na pua kama ya kitusi, na mweusi kama mkaa. Mavazi yangu mitumba, chakula changu ugali kwa miguu na ngozi ya kuku.

Cha ajabu kuna mabinti warembo, wasomi wanaotoka familia za "VIP" hapa mtaani kwetu wananikubali vibaya. Wapo ambao wamekataa kuolewa na watoto wa madon wanakuja kwangu.

Mathalani, kuna binti ( Faith) anafatiliwa na mtoto wa don mkoa mzima amemkataa mbele yangu. Na jamaa ameniomba nimsaidie atanipa mtaji wa 10m. Sikuamini....nikasema Mungu akunyimi vyote.

Basi imebidi nimwambie Faith ili suala....we kumbe nilikosea...maana binti aliwaka sana akampigia simu jamaa na kumtukana sana.

Sasa nimejenga uadui na vijana wengi mtaani. Imagine, hadi wazee baadhi hawanipendi. Juzi namsalimia pastor wangu haitikii..imeniuma sana.

Labda niwatie moyo vijana wenzangu, demu akikutema shukuru Mungu. Huwezi jua anakuepusha na nini mbeleni.

Na pia ni vizuri....

Samahanini mb zinakata muda si mrefu...Ila msijali Faith atanitumia ntaendelea.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo hiyo ni nyota
Nyota nzuri sana
Nyota ya kupakwa wese
 
Tunashukuru kwa tangazo ... watakuja inbox wenye akili ndogo kama zako


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…