GE2025 Nimecheka sana Baada ya Kuona CCM wamekuja na Tone Tone

GE2025 Nimecheka sana Baada ya Kuona CCM wamekuja na Tone Tone

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
36,228
Reaction score
60,546
Hahahaha......Ndugu zangu siasa zimegeuza ubao. Leo ccm wanakuja na tone tone?

Wana wanachama takribani 13M kwa mujibu wa taarifa zao, kama ni za kweli au la sijui lakini Mwanachama mmoja mmoja tu akitoa elfu 10 ni mabilioni ya hela. Je wameshindwa kutumia fursa hiyo?

Baadhi ya wadau wamehoji kwanini CCM imekopy mbinu na taratibu za Chadema mkakati ulioanzishwa na Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika na Godbless Lema.

Wengine wamesema ni siasa tu kujaribu kuamsha ari za uchaguzi na kwamba pesa wanazo ila tu wanazuga.

Lakini kama kweli kuna ukata ndani ya Chama ama la hilo lina baki kuwa siri yao.

Kiichonichekesha ni kuja na Tone tone ambayo waliibeza.

Chadema siku zote iko mbele ya muda na muda ni mwalimu mzuri
 
Tajiri akitaka kuendelea kukutawala kwa hila ni lazima ajifanye na yeye ni maskini mwenzako kumbe anakunyonya.
Yaani mtu ana HAZINA ya nchi, ana kila anachotaka leo hii anataka watu maskini achukue tena walichonacho... hii ni mbayaaa!!
 
Majina kama

1. Mtoto wa mkulima
2. Mtoto wa maskini
3. Rais wa Wanyonge
.yoote haya ni zuga tu na janjajanja
 
Back
Top Bottom