Habari wana MMU? Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulikuwa tunapendana sana na tulipanga Mungu akijaalia tufunge ndoa mwaka huu mwishoni. Sasa leo ameniandikia meseji akiniambia Mama yake amemwambia hawezi kunioa mimi kwa sababu sio wa kabila lake, na yeye kasema hawezi kuacha kumtii mama yake.
Ameniomba tuachane na hivi sasa mama yake amemuunganishia kwa msichana mwingine ambaye ni kabila lao. Hapa nawaza na kuwazua hivi naanza mahusiano na nani? Wanaume wote sio kanisani, ofisini walikuwa wanafahamu mahusiano yetu na waliyaheshimu. Leo hii naanzaje kusema niko single? Ndoto ya kuolewa naona imepaa.
Naombeni ushauri wenu wana MMU, haya mambo yamenichanganya sana.