Nimebaki kushangaa tu

Nimebaki kushangaa tu

milimo

Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
61
Reaction score
32
1. Nashangaa na kutaka kujua ni nani aliyewafanya baadhi ya wana ccm kuwa na maneno ya kihuni? Kwa mfano; nimejaribu kutafakari kuhusu maneno ya "Musukuma" (Mwenyekiti wa ccm mkao wa Geita) nashindwa kuelewa kama kweli huyo ni kiongozi mkubwa wa chama na mgombea ubunge! Nimejaribu kuuliza watu kama Wasukuma na Wamasai ni watani, nikambiwa sivyo (hata utani wa makabila unazungumzia vitu/tabia za asili za jamii husika sio matusi kwa mtu mmoja mmoja). Japokuwa nampongeza Mh. Lowasa na UKAWA kwa ujumla kutojibu yale maneno ya kifedhuli ya kijana "Musukuma", lakini ni muhimu tukemee vitendo hivyo. Nionavyo mimi mpaka sasa bado hatujampata raisi wa nchi kwa maana hiyo anaweza akashinda yeyote kati ya Mh. Lowasa au Mh. Magufuli, hivyo hata kama tunataka vyama vyetu vishinde ili kupata maslahi fulani binafsi ni vizuri tutumie maneno yasiyo ya kifedhuli tunapokua majukwaani. Matusi hayo yanadakwa na vyombo vya habari vya nje hivyo kudhalilisha utu wetu. Hivi ccm ni nani kawafundisha matusi, maana asilimia kubwa ya wapiga debe wa ccm wapandapo jukwaani badala ya kuzunguzia sera huwa ni kumtukana Mh. Lowasa tu. Pamoja na kasoro za hapa na pale nampongeza sana Mh. Magufuli amejitahidi sana kukwepa kuongea matusi akiwa jukwaani, wakati mwingine natamani hata wangemwachia peke yake ndio aongee jukwaani. Lakini mshangao unapungua kwa sababu hata mtu aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa wa chama (katibu mkuu) alipokua anamnadi Mh. Magufuli mjini Morogoro aliporomosha matusi na shutuma tu kwa Mh. Lowasa bila kusema nini kama chama walikifanya ili kuwapa Imani wananchi kuhusu mwenendo wa chama hicho na serikari yake.

2. Nashangaa tena kuhusu mikakati ya Mh. Magufuli kwamba akishinda uraisi atanzisha mahakama ya Mafisadi. Nashangaa kwa sababu ni wazi kwamba hakuna fisadi kijana ambaye anafanya ufisadi wa kutisha (labda wale waliobebwa mgongoni na wazazi wao au ndugu zao). Mafisadi wengi ni wale ambao walitakiwa kuwa wamestaafu lakini bado wanang'ang'ania madaraka kwa sababu hawawezi kufanya biashara nzuri ya kujilimbikizaia mali wakiwa nje ya mfumo wa serikali. Hivi Mh. Magufuli anatuambia kwamba hao wanaompeleka Ikulu ndio atawaundia mahakama ya mafisadi? Nijuavyo ufisadi una sura kuu mbili; moja ni kufanya ufisadi wenyewe na pili ni kunyamazia bila kuwachukulia hatua wale wanaofanya ufisadi (ndio maana watu wanafungwa kwa kutowajibika vizuri). Labda mahakama hiyo itakua kwa ajili ya Mh. Lowasa kama ccm wanavyotuaminisha kwamba ndiye fisadi pekee nchini na ndio maana wanasema kuondoka kwa Lowasa ccm chama kimekua safiii!

3. Nashangaa pia kuwa sijui imetokeaje kwamba wagombea hawa wawili maarufu yaani Mh. Magufuli na Mh. Lowasa nawalinganisha kwa vitu viwili. Moja, wote wawili wanapenda sana kufanya maamuzi kwa kupigiwa makofi (Kiswahili cha mtaani tunasema wanapenda masifa). Hivyo ni vizuri wakashauriwa kupunguza hiyo tabia. Kwa hapa tulipofikia hatuhitaji kiongozi wa kupenda kupigiwa makofi kwa ajili ya umaaru wa kijinga. Tunataka mtu ambaye anamtazamo wa mbele na mpana kwa maslahi ya nchi kiasi kwamba hata akituambia tunafunga mikanda amaanishe hivyo na kila mtu ajifunge mkanda wake akiwemo mwenyewe. Wanasiasa kupenda kupigiwa makofi ndio kumetufikisha hapa na kuwa Taifa la wababaishaji. Nakumbaka Mh. Clean wakati anaingia madarakani ndani ya miaka mitano ya awamu yake ya kwanza alifanya kazi bila kupenda kupigiwa makofi na kazi yake ilonekana. Lakini baadaye naye akabadilika na kuanza kupenda kupigiwa makofi na kupenda kusifiwa ndio matokeo yake tuliyaona mwishoni mwa kipindi chake cha uraisi.

Hawa watu wawili pia wanafanana kwa kufanya maamuzi magumu. Natoa mfano mmoja mmoja kwa kila mtu. Nakumbuka Mh. Magufuli akijua fika kwamba biashara ya Molori yanayoharibu barabara ni ya watu wazito au wanamahusiano na viongozi wazito; akatoa amri ya kupunguza uzito wa mizigo inayoyobebwe na malori hayo kwa ajili ya kunusuri uharibifu wa barabara zetu. Wote tunajua kilichotokea kuhusu wakubwa wake kumwamrisha asitishe hilo zoezi. Japokuwa uamuzi wake haukuzingitia mazingira ya kutokuwa na njia mmbadala na fanisi (kama reli) ya kusafirisha mizigo kwenda mikoani na nchi jirani, lakini nilimpongeza kwa kufanya maamuzi magumu. Wataalamu wanasema ni bora kufanya maamuzi kwa nia njema yenye matokea mabaya kuliko kutofanya maamuzi kabisa (maana yake ni kwamba utakua na mahali pa kuanzia ili kurekebisha mambo). Nije kwa Mh. Lowasa; pamoja na maamuzi mengine magumu aliyofanya, kubwa kuliko yote ni kuhama ccm na kijiunga na Chadema/UKAWA. Haya ni maamuzi magumu sana ukizingitia jinsi dude linaloitwa ccm kujijengea mfumo wa kuogopesha walio ndani kutoka. Kabla ya ccm kumkata kwenye mchakato wao, watu wengi nikiwemo mimi niliona salama ya Mh. Lowasa hata kama atakatwa ni kubaki ndani ya ccm (kutokana na kashfa zilizokua zinamwandama). Nisema ukweli kwamba nilikua miongoni wa watu ambao walikua hawampendi Mh. Lowasa, lakini baada ya kufanya maamuzi hayo magumu sana ghafla nikatokea kumkubali kwa kuamini kwamba ni mtu ambaye anafaa kuwa raisi kwa kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ambapo alikubali kukorofishana na marafiki zake wengi wa muda mrefu kwa uamuzi wake huo. Watu watasema alihama kwa sababu anapenda madara; inawezekana ni kweli lakini tujiulize kama kuna mwanasiasa ambaye hapendi madaraka. Kwa nchi za kwetu mtu yeyote anayeingia kwenye siasa anatafuta madaraka, hivyo ukiwa mwanasiasa lazima ulenge kuwa kiongozi wa ngazi yoyote. Wengi wanapenda madaraka lakini sio jasiri. Ukitaka kujua kuwa kwa uamuzi huo Mh. Lowasa ni jasiri jaribu kumuuliza Mh. Sitta nini alifanya (alingia mitini) wakati ametendwa ndani ya ccm hivyo Chadema walimuomba afanye maamuzi magumu. Wengine watasema mbona hata Mh. Mrema alifanya hivyo; ni kweli alifanya hivyo lakini mazingira ni tofauti sana. Kwanza hakuwa na kashfa zinazomzunguka (zinaweza kuwa na kweli au uzushi) hivyo hakutegemaea kupigwa mawe sana na chama chake cha zamani, pia kulikua na tetesi (za kweli au uongo) kwamba ilikua ni mbinu ya ccm kudhoofisha vyama vya upinzani (hasa Chedema) ili kuvuruga mfumo wa upinzani ulioanza kujengeka wakati ule.

4. Nashangaa pia kuwa Wazee wa ccm wameng'ang'ania madaraka (hawataki kung'atuka) nadhani bado hawajawamini vijana kama wanaweza kuongoza. Na hawa wazee watakaposhindwa kufanya kazi kwa sababu ya uzee ni wazi kwamba chama kitakufa kifo cha mende. Hivi kuna kijana gani ameshika madaraka makubwa? Ni wachache sana ambao miongoni mwao ni wachache sana wanaojitambua, wengi ndio hao waendesha propaganda, watukanaji na waongolea kashfa za Lowasa tu. Wengine watasema kuna mashirika mengi ya umma au mamlaka za umma zinaongozwa na vijana. Je unafahamu wenyeviti wa Bodi na wajumbe wao ambao ndio watunga sera wa mashirika hayo au mamlaka hizo ni wa namna gani? Tunataka vijana wapewe nafasi ya kuongoza baadhi ya mashirika ya umma au mamlaka za umma kuanzia ukurugenzi mpaka wenyeviti wa Bodi na pawepo na mzee mmoja au wawili wa kutoa ushauri tu

5. Nashangaa kuona tuna matatizo makubwa ya elimu ya uraia hata kwa wenye elimu ya darasani. Ili kudhihirisha hilo natoa mifano miwili mifupi. Moja ni kwamba watu wengi wanashindwa kutofautisha serikali na chama, hii inasabisha watumishi wengi wa umma kudhani kwamba ccm isiposhinda na wao watakua hawana kazi. Hata uwambie vipi kwamba mtumishi wa umma anatakiwa kuwa tayari kutumikia serikali yoyote itakayokuwa madarakani (mbali na nafasi za kisiasa) hivyo anatakiwa apige kura kuchagua serikali ambayo anaona itasaidia utendaji wake wa kazi kuwa na ufanisi, kakini walio wengi bado wanakua na wasiwasi na hawaelewi. Pili, utakuta mtu msomi anakua na mawazo ya ajabu ajabu ati vyama vyote vinafanana hivyo hata chama kingine kikichukua madaraka mambo yatakua yaleyale. Maneno hayo ni sawa na kusema mchezaji fulani akikosa penati basi mashabiki wanasema hata angepewa mcezaji mwingine penati hiyo pia angekosa. Watanzania tumekua watu wa kuishi kwa kudhania tu, hata kama tuna elimu zetu bado hazitusaidii. Mfano, kocha mzuri ni yule anayempa nafasi ya kucheza yule anayechonga sana ili akishindwa kucheza vizuri asiweze kuchonga tena. Mpe mtu nafasi, akishindwa ndio upate nafasi ya kumshusha daraja.

6. Nashangaa kuona watu hawatambui kwamba Mh. Lowasa wa ccm sio Lowasa wa Chadema/UKAWA. Ni wazi kwamba uraisi ni tasisi wala sio mtu mmoja. Uraisi ni timu (team work) ambapo maamuzi makubwa hayafanywi na mtu mmoja. Ikitokea Mh. Lowasa ameshinda uraisi halafu uendeshaji wake wa serikali ukawa ni vile vile alivyokua ccm, kwa upande wangu sitamlaumu Lowasa ila nitawalaumu UKAWA kuwa ndio dhaifu. Nina Imani Mh. Lowasa alivyohamia Chadema/Ukawa lazima afuate misingi na matakwa ya vyama hivyo. Tutakapoona mambo yaleyale yaliyokua yanafanyika kwenye chama cha zamani yakaendeleakufanyika ndani ya UKAWA basi hatutasita kuirejesha tena madarakani ccm, na ccm ikirudi madaraka haitakua ile ya zamani maana lazima watakua wamejipanga vizuri na kujirekebisha. Kwa wale wapenzi wa mpira wa miguu niwape mifano miwili inayoakisi namna ambavyo mazingira yanayomzunguka mtu yanamfanya awe mzuri au sio mzuri; moja ni mchezaji Andriy Shevchenko alipokua AC Milan alikua mchezaji wa kutumainiwa lakini alipokwenda Chelsea (sijui Morinho alimfanya nini) akawa butu. Kwa upande mwingine, mfano wa pili ni Arjen Robben, alipokuwa Chelsea alikua mchezaji wa kawaida sana lakini sasa yupo B. Munich ni mchezaji wa kutegemewa, hivyo mazingiza na watu wanaokuzunguka wanakufanya uwe mzuri au wa hovyo.

7. Nashangaa kuona kwamba tusipokua makini uchaguzi huu utatuacha na vidonda vya ukabila. Wanaojua mambo nadhani wamenielewa

Mwenyezi Mungu tunaomba ibariki Tanzania, utuongoze tufanya uchaguzi kwa Amani na utulivu na haki ikatendeke.
 
Ccm hawana sera,,sera yao ni kumtukana Lowasa... Halafu hao watukanaji ndio washauri wa Magufuli ajabu
 
1. Nashangaa na kutaka kujua ni nani aliyewafanya baadhi ya wana ccm kuwa na maneno ya kihuni? Kwa mfano; niimejaribu kutafakari kuhusu maneno ya “Musukuma” (Mwenyekiti wa ccm mkao wa Geita) nashindwa kuelewa kama kweli huyo ni kiongozi mkubwa wa chama na mgombea ubunge! Nimejaribu kuuliza watu kama Wasukuma na Wamasai ni watani, nikambiwa sivyo (hata utani wa makibila unazungumzia vitu/tabia za asili za jamii husikika sio matusi kwa mtu mmoja mmoja). Japokuwa nampongeza Mh. Lowasa na UKAWA kwa ujumla kutojibu yale maneno ya kifedhuli ya kijana “Musukuma”, lakini ni muhimu tukemee vitendo hivyo. Nionavyo mimi mpaka sasa bado hatujampata raisi wa nchi kwa maana hiyo anaweza akashinda yeyote kati ya Mh. Lowasa au Mh. Magufuli, hivyo hata kama tunataka vyama vyetu vishinde ili kupata maslahi fulani binafsi ni vizuri tutumie maneno yasiyo ya kifedhuli tunapokua majukwaani. Matusi hayo yanadakwa na vyombo vya habari vya nje hivyo kudhalilisha utu wetu. Hivi ccm ni nani kawafundisha matusi, maana asilimia kubwa ya wapiga debe wa ccm wapandapo jukwaani badala ya kuzunguzia sera huwa ni kumtukana Mh. Lowasa tu. Pamoja na kasoro za hapa na pale nampongeza sana Mh. Magufuli amejitahidi sana kukwepa kuongea matusi akiwa jukwaani, wakati mwingine natamani hata wangemwachia peke yake ndio aongee jukwaani. Lakini mshangao unapungua kwa sababu hata mtu aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa wa chama (katibu mkuu) alipokua anamnadi Mh. Magufuli mjini Morogoro aliporomosha matusi na shutuma tu kwa Mh. Lowasa bila kusema nini kama chama walikifanya ili kuwapa Imani wananchi kuhusu mwenendo wa chama hicho na serikari yake.

2. Nashangaa tena kuhusu mikakati ya Mh. Magufuli kwamba akishinda uraisi atanzisha mahakama ya Mafisadi. Nashangaa kwa sababu ni wazi kwamba hakuna fisadi kijana ambaye anafanya ufisadi wa kutisha (labda wale waliobebwa mgongoni na wazazi wao au ndugu zao). Mafisadi wengi ni wale ambao walitakiwa kuwa wamestaafu lakini bado wanang’ang’ania madaraka kwa sababu hawaezi kufanya biashara nzuri ya kujilimbikizaia mali wakiwa nje ya ya mfumo wa serikali. Hivi Mh. Magufuli anatuambia kwamba hao wanaompeleka Ikulu ndio atawaundia mahakama ya mafisadi? Nijuavyo ufisadi una sura kuu mbili; moja ni kufanya ufisadi wenyewe na pili ni kunyamazia bila kuwachukulia hatua wale wanaofanya ufisadi (ndio maana watu wanafungwa kwa kutowajibika vizuri). Labda mahakama hiyo itakua kwa ajili ya Mh. Lowasa kama ccm wanavyotuaminisha kwamba ndiye fisadi pekee nchini na ndio maana wanasema kuondoka kwa Lowasa ccm chama kimekua safiii!

3. Nashanga pia kuwa sijui imetokeaje kwamba wagombea hawa wawili maarufu yaani Mh. Magufuli na Mh. Lowasa nawalinganisha kwa vitu viwili. Moja, wote wawili wanapenda sana kufanya maamuzi kwa kupigiwa makofi (Kiswahili cha mtaani tunasema wanapenda masifa). Hivyo ni vizuri wakashauriwa kupunguza hiyo tabia. Kwa hapa tulipofikia hatuhitaji kiongozi wa kupenda kupigiwa makofi kwa ajili ya umaaru wa kijinga. Tunataka mtu ambaye anamtazamo wa mbele na mpana kwa maslahi ya nchi kiasi kwamba hata akituambia tunafunga mikanda amaanishe hivyo na kila mtu ajifunge mkanda wake akiwemo mwenyewe. Wanasiasa kupenda kupigiwa makofi ndio kumetufikisha hapa na kuwa Taifa la wababaishaji. Nakumbaka Mh. Clean wakati anaingia madarakani ndani ya miaka mitano ya awamu yake ya kwanza alifanya kazi bila kupenda kupigiwa makofi na kazi yake ilonekana. Lakini baadaye naye akabadilika na kuanza kupenda kupigiwa makofi na kupenda kusifiwa ndio matokeo yake tuliyaona mwishoni mwa kipindi chake cha uraisi.

Hawa watu wawili pia wanafanana kwa kufanya maamuzi magumu. Natoa mfano mmoja mmoja kwa kila mtu. Nakumbuka Mh. Magufuli akijua fika kwamba biashara ya Molori yanayoharibu barabara ni ya watu wazito au wanamahusiano na viongozi wazito; akatoa amri ya kupunguza uzito wa mizigo inayoyobebwe na malori hayo kwa ajili ya kunusuri uharibifu wa barabara zetu. Wote tunajua kilichotokea kuhusu wakubwa wake kumwamrisha asitishe hilo zoezi. Japokuwa uamuzi wake haukuzingitia mazingira ya kutokuwa na njia mmbadala na fanisi (kama reli) ya kusafirisha mizigo kwenda mikoani na nchi jirani, lakini nilimpongeza kwa kufanya maamuzi magumu. Wataalamu wanasema ni bora kufanya maamuzi kwa nia njema yenye matokea mabaya kuliko kutofanya maamuzi kabisa (maana yake ni kwamba utakua na mahali pa kuanzia ili kurekebisha mambo). Nije kwa Mh. Lowasa; pamoja na maamuzi mengine magumu aliyofanya, kubwa kuliko yote ni kuhama ccm na kijiunga na Chadema/UKAWA. Haya ni maamuzi magumu sana ukizingitia jinsi dude linaloitwa ccm kujijengea mfumo wa kuogopesha walio ndani kutoka. Kabla ya ccm kumkata kwenye mchakato wao, watu wengi nikiwemo mimi niliona salama ya Mh. Lowasa hata kama atakatwa ni kubaki ndani ya ccm (kutokana na kashfa zilizokua zinamwandama). Nisema ukweli kwamba nilikua miongoni wa watu ambao walikua hawampendi Mh. Lowasa, lakini baada ya kufanya maamuzi hayo magumu sana ghafla nikatokea kumkubali kwa kuamini kwamba ni mtu ambaye anafaa kuwa raisi kwa kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ambapo alikubali kukorofishana na marafiki zake wengi wa muda mrefu kwa uamuzi wake huo. Watu watasema alihama kwa sababu anapenda madara; inawezekana ni kweli lakini tujiulize kama kuna mwanasiasa ambaye hapendi madaraka. Kwa nchi za kwetu mtu yeyote anayeingia kwenye siasa anatafuta madaraka, hivyo ukiwa mwanasiasa lazima ulenge kuwa kiongozi wa ngazi yoyote. Wengi wanapenda madaraka lakini sio jasiri. Ukitaka kujua kuwa kwa uamuzi huo Mh. Lowasa ni jasiri jaribu kumuuliza Mh. Sitta nini alifanya (alingia mitini) wakati ametendwa ndani ya ccm hivyo Chadema walimuomba afanye maamuzi magumu. Wengine watasema mbona hata Mh. Mrema alifanya hivyo; ni kweli alifanya hivyo lakini mazingira ni tofauti sana. Kwanza hakuwa na kashfa zinazomzunguka (zinaweza kuwa na kweli au uzushi) hivyo hakutegemaea kupigwa mawe sana na chama chake cha zamani, pia kulikua na tetesi (za kweli au uongo) kwamba ilikua ni mbinu ya ccm kudhoofisha vyama vya upinzani (hasa Chedema) ili kuvuruga mfumo wa upinzani ulioanza kujengeka wakati ule.

4. Nashangaa pia kuwa Wazee wa ccm wameng’ang’ania madaraka (hawataki kung’atuka) nadhani bado hawajawamini vijana kama wanaweza kuongoza. Na hawa wazee watakaposhindwa kufanya kazi kwa sababu ya uzee ni wazi kwamba chama kitakufa kifo cha mende. Hivi kuna kijana gani ameshika madaraka makubwa? Ni wachache sana ambao miongoni mwao ni wachache sana wanaojitambua, wengi ndio hao waendesha propaganda, watukanaji na waongolea kashfa za Lowasa tu. Wengine watasema kuna mashirika mengi ya umma au mamlaka za umma zinaongozwa na vijana. Je unafahamu wenyeviti wa Bodi na wajumbe wao ambao ndio watunga sera wa mashirika hayo au mamlaka hizo ni wa namna gani? Tunataka vijana wapewe nafasi ya kuongoza baadhi ya mashirika ya umma au mamlaka za umma kuanzia ukurugenzi mpaka wenyeviti wa Bodi na pawepo na mzee mmoja au wawili wa kutoa ushauri tu

5. Nashangaa kuona tuna matatizo makubwa ya elimu ya uraia hata kwa wenye elimu ya darasani. Ili kudhihirisha hilo natoa mifano miwili mifupi. Moja ni kwamba watu wengi wanashindwa kutofautisha serikali na chama, hii inasabisha watumishi wengi wa umma kudhani kwamba ccm isiposhinda na wao watakua hawana kazi. Hata uwambie vipi kwamba mtumishi wa umma anatakiwa kuwa tayari kutumikia serikali yoyote itakayokuwa madarakani (mbali na nafasi za kisiasa) hivyo anatakiwa apige kura kuchagua serikali ambayo anaona itasaidia utendaji wake wa kazi kuwa na ufanisi, kakini walio wengi bado wanakua na wasiwasi na hawaelewi. Pili, utakuta mtu msomi anakua na mawazo ya ajabu ajabu ati vyama vyote vinafanana hivyo hata chama kingine kikichukua madaraka mambo yatakua yaleyale. Maneno hayo ni sawa na kusema mchezaji fulani akikosa penati basi mashabiki wanasema hata angepewa mcezaji mwingine penati hiyo pia angekosa. Watanzania tumekua watu wa kuishi kwa kudhania tu, hata kama tuna elimu zetu bado hazitusaidii. Mfano, kocha mzuri ni yule anayempa nafasi ya kucheza yule anayechonga sana ili akishindwa kucheza vizuri asiweze kuchonga tena. Mpe mtu nafasi, akishindwa ndio upate nafasi ya kumshusha daraja.

6. Nashangaa kuona watu hawatambui kwamba Mh. Lowasa wa ccm sio Lowasa wa Chadema/UKAWA. Ni wazi kwamba uraisi ni tasisi wala sio mtu mmoja. Uraisi ni timu (team work) ambapo maamuzi makubwa hayafanywi na mtu mmoja. Ikitokea Mh. Lowasa ameshinda uraisi halafu uendeshaji wake wa serikali ukawa ni vile vile alivyokua ccm, kwa upande wangu sitamlaumu Lowasa ila nitawalaumu UKAWA kuwa ndio dhaifu. Nina Imani Mh. Lowasa alivyohamia Chadema/Ukawa lazima afuate misingi na matakwa ya vyama hivyo. Tutakapoona mambo yaleyale yaliyokua yanafanyika kwenye chama cha zamani yakaendeleakufanyika ndani ya UKAWA basi hatutasita kuirejesha tena madarakani ccm, na ccm ikirudi madaraka haitakua ile ya zamani maana lazima watakua wamejipanga vizuri na kujirekebisha. Kwa wale wapenzi wa mpira wa miguu niwape mifano miwili inayoakisi namna ambavyo mazingira yanayomzunguka mtu yanamfanya awe mzuri au sio mzuri; moja ni mchezaji Andriy Shevchenko alipokua AC Milan alikua mchezaji wa kutumainiwa lakini alipokwenda Chelsea (sijui Morinho alimfanya nini) akawa butu. Kwa upande mwingine, mfano wa pili ni Arjen Robben, alipokuwa Chelsea alikua mchezaji wa kawaida sana lakini sasa yupo B. Munich ni mchezaji wa kutegemewa, hivyo mazingiza na watu wanaokuzunguka wanakufanya uwe mzuri au wa hovyo.

7. Nashangaa kuona kwamba tusipokua makini uchaguzi huu utatuacha na vidonda vya ukabila. Wanaojua mambo nadhani wamenielewa

Mwenyezi Mungu tunaomba ibariki Tanzania, utuongoze tufanya uchaguzi kwa Amani na utulivu na haki ikatendeke.
Msukuma ni kijana wa mitaani tu hata shule hana! Kazi yake ni kutumwa na matajiri wa mwanza kuwachungia ng'ombe,kichwani hamna kitu! Niko hapa Geita kwa sasa yaani watu wa rika zote wamemdharau sana na ubunge ataangukia pua! Wamesema watakula hela zake anazokopa kwa matajiri wa mwanza ila kura kwa Rogers.
 
Lowasa aliondoka serikalini miaka 8 iliyopita. Sumaye aliondika serikalini miaka 10 iliyopita. Sasa tujiulize maswali yafuatayo-
Hivi kweli kwa takribani miaka nane hakuna ufisadi uliotokea? Zaidi ya richmond? Mbona majukwaa ya kampeni za ccm hawayataji hayo?
CCM ime divert na kuwaduwaza watanzania na kusahau ESCROW, TOKOMEZA, Mabehewa ya train mabovu , rada etc, wanachozungumza ni Lowasa na richmond tuu. Ama kweli nimeamini watanzania ni NYUMBU
 
Siasa sio uadui kiasi hicho! Haiwezekani mwenzio alikua rafiki yako kipenzi tena amekutoa matongotongo na amekufundisha siasa eti Leo hii unamtukana matusi ya nguoni.Hii ni fedheha na laana itakayomrafuna Msukuma hata baada ya uchaguzi. Mkuu.
 
Tena ni kama watoto wanatukana baba zao. Siasa inapukutisha weledi
 
Hivi kweli tuache ushabiki wa kijinga. Kwa kuondoka Lowasa CCM ndio imekua safi? Mbona aliondoka serikalini miaka nane iliyopita. Je serikali ya CCM inachembe ya usafi hata moja?
 
Tatizo si CCM kuwa safi ila tatizo ni namna watu wa chama Fulani walituaminisha mtu huyu mmoja ndiye FISADI MKUU.
Hivyo nivigumu kwa wananchi wanaoelewa kuamini hii dhana ya kutuaminisha kuwa huyu huyu diye atakuja kutukomboa.
Hata kudiriki kusema ni vema nchi tukampa MWIZI MZOEFU kuliko kumpa MWIZI ANAYEJIFUNZA.
Sentensi kama hizi zinapotoka majkwaani ndiyo tatizo. Sasa mtu nachafuliwa na anaendelea kuchafuliwa huku watu wakidhani kuwa wananesha msisitizo
Kwa mtindo huu tulikotoka na tunako kwenda hakuna dira
 
Muheshimiwa aliendelea kusakamwa kwa miaka yote hata asipate kwa kupumua.
Watu bado na wanaendelea kuhoji kuhamia upande uliyokudhihaki ndiyo kukufanya kuwa msafi.
Tanzania bado siasa ni za kutumia majina ya watu.
Tuende mbaili kuonesha namna gani jambo Fulani utalitekeleza na watu wakaelewa hapo ndipo mabadiliko ya kweli yatatokea. Watu utawaona kwa umoja wao na kimya kimya wakibadilisha nchi na watu wengine wakistajabu.
 
Mbona unashangaa ya ccm Tu lakini ya chadema hayakushangazi!

1. Nashangaa kuona chadema wametoka kwenye msitari baada ya kumpokea lowassa.

2. Nashangaa kuona mbowe amemuuzia fisadi namba moja chama kwa bilioni kumi.

3. Nashangaa kuona fedha zimewagawa viongozi Wa ukawa. Slaa, lipumba, seif, mbatia na mbowe.

4. Nashangaa kuona ukawa suala LA afya ya lowassa haliwagusi. Mzee hafai kugombea urais kana kweli tunaipenda Tanzania.

5. Nashangaa kuona ukawa licha ya kutokua na kashfa ya magufuli wamengangania kumuunga mkono lowassa
 
Mijitu bado inashabikia upuuzi, upuuzi wa kupiga pushap jukwaani, upuuzi wa kusema watu maneno machafu ambayo yanakera na kufedhehesha. Naamini mungu anasikia udharirishaji huu. Watu hawajui kabla hujafa hujaumbika. Kwa imani kauli hiyo chafu itamrudia msukuma katika maisha yake.
 
Endelea tu kushangaa mkuu hapo tutakapo muapisha rais MAGUFULI utazimia kabisa
 
Unamsema sana Lowasa, huku ukijua kuwa wewe sio Mungu, na wala ugonjwa wake hauujui. Kwahiyo kuisemea nafsi ya mwenzio ni dhambi, na dhambi anafanyiwa Mungu ndio maana nitakushtakia kwake, ili akuhukumu.
 
Back
Top Bottom