Nimeathirika kisaikolojia,Nahitaji msaada wenu..

Nimeathirika kisaikolojia,Nahitaji msaada wenu..

Mmmmmh napata shida nikushaurije kama matatizo ya utotoni unayo hadi leo. Point note; kaa na mamako kwa kuwa yeye hajui kama humpendi na umwonyeshe upendo wa dhati. Pia mshukuru sana kwa malezi yake maana huenda asingekupa vichapo hivyo leo ungekuwa mauti au jela kabisa.
 
100℅ya maisha yangu nimelelewa na bimkubwa may be kidogo na dada wa nyumbani...ila nakiri na najua adhabu za mama ndizo zilizonifanya hadi leo kidogo nimekuwa na future ktk maisha yangu.nilikuwaga mkorofi na kiburi kila siku nilikuwa napigwa na niliona naonewa but sasa nimekuwa mtu mzima nimeshajua umuhimu wa zile adhabu.crew yote tuliokuwa tunafanya ujinga ujinga sasa wengine wanakunywa viroba mmoja yupo jela kwa robbery.mkuu mshukuru sana mama yako,hapo sasa ivi unatype sometime kama sio adhabu zake usingefika hapo ungeishia darasa la tatu
 
Nenda Kwa Washahuri wakushauri,maana matatizo ya kisakolojia hayaishi kwa ushahuri wa siku moja.

Unahitaji matibabu Kama ugonjwa mwingine,utapangiwa dozi kulingana na maelezo yako na jinsi utakavyo kuwa Wakati wa maongezi yenu.
 
MAMA NI MAMA TU....pole sana ndugu yangu. ..usijali Mwenye Enzi Mungu atakuongoza Yeye Mwenyewe na atarudisha pendo lako na la mama tena...stay blessed my friend
 
I Am telling you bro

You're gonna miss her when she's gone....
hata mimi nilikuwa kama wewe japo wewe umezidi, tokea nilipoanza kujitegemea nilikuwa mvivu sana kupiga simu au kwenda home hata kusalimia mpaka inafika wakati ananipigia simu anamwaga lawama kibao binafsi nachukulia poa tu

Ila baada ya yeye kufariki (R.I.P) ndipo nilianza kujua neno kumiss lina maana gani,

Mkuu, hakuna mwanadamu mkamilifu, mpende na kumjali mama yako hakuna mbadala wa mama
 
PTSD hiyo! Tafuta psychologists wakusaidie, la sivyo inaweza kukusababishia terminal illnesses kama schizophrenia.
 
MAMA NI MAMA TU....pole sana ndugu yangu. ..usijali Mwenye Enzi Mungu atakuongoza Yeye Mwenyewe na atarudisha pendo lako na la mama tena...stay blessed my friend
Asante sana mkuu..
 
I Am telling you bro

You're gonna miss her when she's gone....
hata mimi nilikuwa kama wewe japo wewe umezidi, tokea nilipoanza kujitegemea nilikuwa mvivu sana kupiga simu au kwenda home hata kusalimia mpaka inafika mda mpaka ananipigia simu anamwaga lawama kibao binafsi nachukulia poa tu

Ila baada ya yeye kufariki (R.I.P) ndipo nilianza kujua neno kumiss lina maana gani,

Mkuu, hakuna mwanadamu mkamilifu, mpende na kumjali mama yako hakuna mbadala wa mama
Nimekupata mkuu,nashukuru kwa ushauri..god bless you..
 
Dogo utakuwa na laana! Kuna post yako humu umeomba ushauri dada yako anakutaka kimapenzi, nyingine inadai mpenzi wako ukimpa elfu 10 kesho anakudai elfu 10x2,
Leo umekuja na chuki na mama yako.

Anatafuta kick hana lolote... Watu kama hawa una wa bulokuu kutafuta sifa za kijinga tu
 
Explain it hii imekaaje?
Kuna post yake humu inadai ameathirika kisaikojia kisa kaoa mwanamke ila anadai pesa. Eg leo akipa laki kesho anamdai lakix2! Keshokutwa laki2x2! Hawa ndo great thinkers wa kizazi cha nyoka.
 
100℅ya maisha yangu nimelelewa na bimkubwa may be kidogo na dada wa nyumbani...ila nakiri na najua adhabu za mama ndizo zilizonifanya hadi leo kidogo nimekuwa na future ktk maisha yangu.nilikuwaga mkorofi na kiburi kila siku nilikuwa napigwa na niliona naonewa but sasa nimekuwa mtu mzima nimeshajua umuhimu wa zile adhabu.crew yote tuliokuwa tunafanya ujinga ujinga sasa wengine wanakunywa viroba mmoja yupo jela kwa robbery.mkuu mshukuru sana mama yako,hapo sasa ivi unatype sometime kama sio adhabu zake usingefika hapo ungeishia darasa la tatu
Ila inategemea sometime wazazi wanakuwaga na maneno makali sana,yani kosa kidogo la bahati mbaya ambalo hukukusudia ila maneno atakayotamka utabaki unashangaa k yatoa wapi au alikuwa amekuhifadhia anasubiri ukosee hapo ukikumbuka kimtokacho mtu ndicho kiujazacho moyo wake un baki unashangaa yale ambayo anakuwaziaga.

Imagine mzazi hatunzi privacy zako,atawambia rafiki zake au hata rafiki yako kitu ambacho hukutaka ajue coz hata akijua labda haimuhusu yani anamsimulia tu bila reason ya msingi na kukusengenya juu,jamani kuwa mzazi ni kuwa mungu wa pili kwa mtoto wako,mfanye mwanao akupende,akuamini akutumaini sio kisa mama ndio iwe ticket ya kumnyanyasa mtoto vile unavyotaka mara umchagulie mchumba kwa nguvu zote eti kisa tu mama,au unamtukana hadharani mtoto above 18 na utegemee mtoto atakupenda maneno hayapoteagi kirahisi unaweza mtukana mtu kwa dk1 ila akaumia miaka 10.
 
Potea nyumbani mapema sana nenda kaanze maisha yako wewe na mkeo....tena mikoa ya mbali sana funga mawasiliano kwa miaka miwili na yeye....siku ukijamtafuta asipokuambia amekumiss ni sikio la kufa huyo.....
 
Baba ni kama rafiki..
Pole sana jitahidi kuondoa ghadhabu hizo kwani paradise under the feet of Mother.

Msaidie sana hata kama ana uwezo, kama zawadi ndogo ndogo.
Kwani anajuwa yaliyomsibu mpaka akawa mkali kiasi hicho.
 
kaka uwa natamani nami niandike kama ww yanayokusibu kuhusu mama yako, uwa nashindwa naona watu watanipa ushauri negative
hata mm nilikuwa mtundu balaa, ikitokea nyumbani ugomvi kati yangu na kaka yangu au wadogo zangu basi nitapigwa mm hata kama sina kosa.
ilifika kipind nilimchapa mdogo wangu wa kike fimbo, mama alitoka huko na kunikoromea akaniambia ningejua ningekupa sumu ufe toka ukiwa mdogo kipindi hicho naingia A'level akasema pia na tuone kama uendako utafaulu, ila mungu mkubwa nilifaulu.
mpaka nyakati hizi mama uwa anisemi kwa mambo mazuri, mara nyingi ananitolea mifano negative.
uwa nashangaa huo upendo kwa mama wengine wanaosifia uwa nahisi kama ni vitu vya kufikirika pia stor na mama sina kabisa
nami pia nisaidien hii kitu inanisumbua sana,naweza kukaa hata miez kadhaa sijawasiliana na mama na ninahisi poa hata yy anitafuti.
 
Back
Top Bottom