Nimeathirika kisaikolojia,Nahitaji msaada wenu..

Jiraniyetu

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
350
Reaction score
333
Kwanza habari zenu wadau,,kiukweli mi nahisi saikolojia yangu imevurugika,..Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtundu sana,sasa mama alikuwa akinipa dozi ya kichapo kama mbwa mwizi,,ilifikia hatua akawa ananiwekea kisu shingoni kama anataka kunichinja,,nilikuwa nakung'utwa soli za viatu mpaka basi,,amekuwa akinitamkia maneno makali sana hata nikikosea kitu kidogo tangu nikiwa mdogo hadi nikiwa mkubwa,, sasa nimekuwa bila amani na mamaangu,,na kadri siku zinavyozidi kwenda ndo nazidi kukosa aman na ule upendo wa kutoka moyoni haupo tena kisana kwa mama angu kiasi hata kummisi inakuwa ngumu sana,,,najua hakuna kama mama,najitahidi niishinde hiyo hali lakini nashindwa,,naombeni mnishauri njia ya kuurejesha moyo wangu kwenye hali ya kawaida..[HASHTAG]#Nishaurini[/HASHTAG]..
 
Pole, umeacha utundu lakinii?? Halafu nina wasiwasi na ile asilimia 49, labda ndo maana mama anatembeza kichapo kikuu
 
Hiyo 49 angekuwa baba hapo sawa. Mama tena [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Ngumu hiyo mh, yeye mwenyewe anajua una feel hivyo? Umeshawahi kumwambia?
 
Tatizo watu wengi huwa tunataka kuwatazama wazazi kama 'watu perfect'

kumbe mzazi wako anaweza kabisa kuwa 'mgonjwa wa akili'

jifunze kuwatazama watu na mapungufu yao utajikuta huwalaumu

soma sana vitabu
hasa vya saikolojia
 
Kwanza habari zenu wadau,,kiukweli mi nahisi saikolojia yangu imevurugika,..Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtundu sana,sasa mama alikuwa akinipa dozi ya kichapo kama mbwa mwizi,,ilifikia hatua akawa ananiwekea kisu shingoni kama anataka kunichinja,,nilikuwa nakung'utwa soli za viatu mpaka basi,,amekuwa akinitamkia maneno makali sana hata nikikosea kitu kidogo tangu nikiwa mdogo hadi nikiwa mkubwa,, sasa nimekuwa bila amani na mamaangu,,na kadri siku zinavyozidi kwenda ndo nazidi kukosa aman na ule upendo wa kutoka moyoni haupo tena kisana kwa mama angu kiasi hata kummisi inakuwa ngumu sana,,,najua hakuna kama mama,najitahidi niishinde hiyo hali lakini nashindwa,,naombeni mnishauri njia ya kuurejesha moyo wangu kwenye hali ya kawaida..[HASHTAG]#Nishaurini[/HASHTAG]..
Dogo utakuwa na laana! Kuna post yako humu umeomba ushauri dada yako anakutaka kimapenzi, nyingine inadai mpenzi wako ukimpa elfu 10 kesho anakudai elfu 10x2,
Leo umekuja na chuki na mama yako.
 
Uyo mama hatari asee
Hadi kisu shingoni!

Nenda kanisani mkuu(kama ni christian), shiriki zile seminar seminar zitakujenga kiroho, upendo unaweza ukarudi ukisamehe

Kutokuwa na maelewano na mzazi sio poa kabisa

Pole mkuu
 
Tatizo watu wengi huwa tunataka kuwatazama wazazi kama 'watu perfect'

kumbe mzazi wako anaweza kabisa kuwa 'mgonjwa wa akili'

jifunze kuwatazama watu na mapungufu yao utajikuta huwalaumu

soma sana vitabu
hasa vya saikolojia

Ushauri mzuri mkuu, nmejifunza kitu na mm...............................
 
Kama mama hakupendi kiasi hicho na umejitahidi kumwonyesha unamuheshimu na kumjali lakini bado anakuwa katili (iwe kwa maneno makali au kwa namna yoyote ile) hauna sababu wewe kujali tena lolote linalomuhusu. Jambo muhimu kwako fucus nini unakipenda zaidi katika maisha yako. Maisha mafupi sana kuishi katika wasiwasi namna hiyo

Mkuu unatakiwa uwe IMARA mwonyeshe mama UNAMPENDA lakini pia muonyeshe wewe si "jinga" kisa tu yeye ni mama sasa anatumia mwanya huo kukutesa.

Maximum respect and honor bredren.
 
Back
Top Bottom