Nimeanza Tena Kuangalia Taarifa Ya Habari Ya ITV

Nimeanza Tena Kuangalia Taarifa Ya Habari Ya ITV

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu,

Kwa muda sasa nimekuwa niki-tune TBC1 kwa ajili ya taarifa ya habari na zaidi ile ya saa mbili usiku.
Jana nili-tune televisheni ya ITV.

Nilijikuta nikibaki kwenye kiti karibu kwa muda wote wa taarifa hiyo. Ama hakika, niliona tofauti. ITV wameonyesha kujitahidi sana katika kuandaa taarifa ya habari yao. Ilikuwa ya mchanganyiko wa habari.

Ilipofika kwenye kuripoti kampeni za Uchaguzi wa Arumeru Mashariki, vyama viwili vikubwa vinavyopambana huko vilipata coverage inayolingana kwa kiasi kikubwa. Hata CUF walipata coverage kubwa kwenye mkutano wao kule Unguja.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http.//mjengwablog.com
 
Maggid hiyo habari ya siku moja tu una conclude? Ungeendelea kufanya utafiti alafu ndio uje kutoa analysis hapa! This is too low kwa level zako mkuu wangu!
 
Mkuu ni kweli taarifa ya jana na juzi wamejitahidi sana. coverage haikuwa na upande. Naona wamerekebisha tangu tuwaweke hapa jamvini mambo yao na safi siku hizi
 
TBC1 wanapenda usanii wanataka wagombea kama yule wa Igunga aliyekuwa kituko ndiyo wampe coverage ya kutosha lengo ni kudhalilisha upinzani. Lakini upinzani ukidondosha nondo za ukweli hawaonyeshi hata kwa dawa.
 
Habari yao nzuri lakini ikifika wakati wa habari ya CCM Arumeru wanachakachua sana, wanweka picha za siku ya uzinduzi badala ya kutuonyesha uhalisia wa mambo.
 
Kwa habari za kitaifa hakuna kituo kinachowafikia ITV, ukitaka porojo za habari wafi TBC1
 
Naunga mkono hoja yako. TBC baada ya Tido Mhando kuondoka inazidi kushuka kila siku + kupendelea ccm.
 
kweli itv walionesha kubadilika kidogo na chombo cha habari kinatakiwa kuwa vile sio kupenda ushabiki tu
 
itv sasa safiii ila nipashe naona kama wame-base upande mmoja
 
Ndugu zangu,

Kwa muda sasa nimekuwa niki-tune TBC1 kwa ajili ya taarifa ya habari na zaidi ile ya saa mbili usiku.
Jana nili-tune televisheni ya ITV.

Nilijikuta nikibaki kwenye kiti karibu kwa muda wote wa taarifa hiyo. Ama hakika, niliona tofauti. ITV wameonyesha kujitahidi sana katika kuandaa taarifa ya habari yao. Ilikuwa ya mchanganyiko wa habari.

Ilipofika kwenye kuripoti kampeni za Uchaguzi wa Arumeru Mashariki, vyama viwili vikubwa vinavyopambana huko vilipata coverage inayolingana kwa kiasi kikubwa. Hata CUF walipata coverage kubwa kwenye mkutano wao kule Unguja.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http.//mjengwablog.com
hebu imagine watu kama huyu ndio ma prominent news analysts wetu wa kibongo!
 
Maggid ulichokinena umekimaanisha kwa uhalisia, mie ni mfuatiliaji mzuri wa taarifa za habari usiku, naanza na channel ten, inafuat mlimani tv then najitahidi kuangalia ITV & TBC1, Taarifa ya TBC1 hasa habari za kitaifa hakika inakerehesha hasa tangu Clemence Mshana, yule kada wa chama cha magamba apewe u-CEO, Tbc1 imekuwa sawa na radio uhuru fm! Inaendeshwa very bias na habari zake ni za kiccm.
PENDEKEZO: Tupendekeze ibadili jina iache kuitwa Tbc1 iwe CCMbc1 na isiendeshwe kwa ruzuku itokanayo na kodi yetu, bajeti yake itoke kwenye ruzuku ya chama cha magamba.
 
Back
Top Bottom