Nimeangamiza jeshi la Kunguni kimasihara

mtumbagrade1

Member
Joined
Sep 10, 2020
Posts
71
Reaction score
67
Hawa wazee waliweka kambi chumbani kwangu, aisee sio watu wazuri yaani wanagawa dozi kwa ushirikiano alafu wana masaa ya kazi, wanapishana mida ya usiku yaani ukiamka manundu mwili mzima.

Yaani nilikuwa sina muda wa kuweka alarm maana huwezi pitiwa na usingizi ukiwa na hawa wadudu ndani kwako, ukifika saa kumi utaamka kitandani utakaa kwenye kochi kupumzika kwanza.

20200922_180318.jpg

Sasa siku nikawaamulia baada ya kusikia kuwa sumu inawafanya wanasinzia hawafi, nikaazima bonge la sufuria la kupikia pilau lile kwa mama ntilie hapa home, nikachemsha maji hadi yakachemka then nikayamwaga kila sehem iliyokuwa na makazi yao kuanzia chaga za kitanda hadi kitanda chenyewe mpaka godoro.

Kwa sasa mwezi huu sioni hata kitoto cha kunguni
 
Ungetumia mafuta ya taa mkuu yaani unatafuta zile chupa za kusprey unayajaza humo halafu unatoa vitu vyako nje kuanzia chaga+godoro+mito nk then unapulizia itakusumbua hiyo harufu kwa muda lkn ndo dawa komesha kwa wadudu hata wadudu+wanyama wakali kama nyoka+na wadudu wengine kama viroboto+utitiri+mbu+mende (piga kwenye chemba za choo),umeharibu kuni/gesi bure
 
Hawa wazee waliweka kambi chumbani kwangu, aisee sio watu wazuri yaani wanagawa dozi kwa ushirikiano alafu wana masaa ya kazi, wanapishana mida ya usiku yaani ukiamka manundu mwili mzima.

Yaani nilikuwa sina muda wa kuweka alarm maana huwezi pitiwa na usingizi ukiwa na hawa wadudu ndani kwako, ukifika saa kumi utaamka kitandani utakaa kwenye kochi kupumzika kwanza.

View attachment 1591388

Sasa siku nikawaamulia baada ya kusikia kuwa sumu inawafanya wanasinzia hawafi, nikaazima bonge la sufuria la kupikia pilau lile kwa mama ntilie hapa home, nikachemsha maji hadi yakachemka then nikayamwaga kila sehem iliyokuwa na makazi yao kuanzia chaga za kitanda hadi kitanda chenyewe mpaka godoro.

Kwa sasa mwezi huu sioni hata kitoto cha kunguni
Mkuu mimi ilikuwa ikifika usiku nalichukia geto, nilikuwa nalala na tracksuti, soksi miguuni na sweta lenye kofia yaan kama ninja. Nilitumia dawa nikashindwa niliama geto nikauza samani zote kwa ninja mwingine.
 
Back
Top Bottom