Mnyenz
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 2,042
- 6,292
Pata picha ni muda wa usiku kuna sehemu unaenda kuna shida muhimu sana[ mida kama ya saa sita usiku] ili uweze kwenda huko ni lazima ukodi boda boda ya kukupeleka, basi unaenda mpaka kituo cha boda boda unapofika wanakuchangamkia lakini unapotaja sehemu unapotaka kupelekwa wote kwa pamoja wanasita na kukwambia kwa mida hiyo kwenda maeneo ya huko ni hatari kuna wakabaji.
kwa kuwa una shida sana ya kufika huko unalazimika kumshawishi mmoja wao na kumbembeleza sana, unaamua na kumuongezea hela ili tu akupeleke, hatimae kijana wa watu tamaa inamuingia anaamua kukupeleka, unampa chake safari inaanza......
Mkiwa katikati ya safari kwenye kamsitu kadogo wanatokea watu wakiwa na silaha za jadi, wanawazuia na kuanza kumpa kipigo dereva kwa kuwa yeye anaonesha ubishi,{ wewe wamekupiga mtama wako umetulia zako chini tuliiii.....}
baada ya kumpa kipigo dereva wa boda boda wanawasha piki piki hiyo na kutokomea zao{ wanaiiba} hivyo hapo chini unabaki wewe na huyo dereva, anatoa simu yake mfukoni na kuwapigia wenzake kwamba ameibiwa piki piki, wanamuuliza jamaa aliekukodi yupo anajibu yupo, basi wanasema wanakuja.
Je, kama wewe ndio huyo abiria utachukua hatua gani? utaamua kujikongoja ukimbie ukichechemea kutokomea gizani? ama utasubiri msaada wa boda boda wenzake?????
...................... usiku mwema....................