Nimeamua kumpotezea rafiki yangu

Madam vivian original

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
503
990
Wakuu nilipata rafiki wa kiume, yeye ameoa na mimi nimeolewa ila familia zetu wote wapo mbali tumekutana mkoa mmoja, tukaanza urafiki mpaka ile stage ya kubebishana mara pika nije kula na kudekezana.

Nikaanza kuona hapa nikileta ujinga tutaingia kwenye mahusiano, na mtu mwenyewe jamaa anaonekana ana mambo mengi. Basi leo tukachuniana tangu asubuhi, jioni hii nikamwambia I miss you, akaajibu thanx madam.

Eeh pozi likaniishia nikasema any way acha nimchane, nikamwambia naomba urafiki wetu uishie na maneno mazuri mazuri ya kumtia moyo, nikajaza paragraph mwisho nikamwambia ntakumiss bye.

Jibu alilonipa sasa Good luck

Mimi kuona hivyo nikamtia block na kufuta namba zake juu.

Sasa hivi nimekaa hapa tayari nishamiss, najua na yeye pia atakua kanimiss lakini najua ujeuri wa wanaume anaweza akamute kimya.

Wakuu, Je nimekosea kumpotezea huyu rafiki yangu?
 
Hujakosea 😀😀

Mihemko yako ndo ilifamya uone kama anakutaka… umejiskia vibaya kuona ye hayuko mawazo yako yalipo

Ukajipa moyo umuache as if mlikua kwenye mahusiano.

Mwenzako hana shida we ndo unatapatapa sasa

In short akirudi atakukula na urafiki hautaendelea utaumia kuliko sasa

Ila polee😉
 
Hujakosea

Mihemko yako ndo ilifamya uone kama anakutaka… umejiskia vibaya kuona ye hayuko mawazo yako yalipo

Ukajipa moyo umuache as if mlikua kwenye mahusiano
Mwenzako hana shida we ndo unatapatapa sasa

In short akirudi atakukula na urafiki hautaendelea utaumia kuliko sasa

Ila polee
Ila nayeye atakua kaumia mkuu, hembu nitie moyo bas
 
Back
Top Bottom