Nimeamua kuachana na CHADEMA

Eboo nimekwambia sina chama wala sikuwa na chama,nilipenda na kukubali walichokuwa wakipigania CHADEMA.
Hapo kwenye msisitizo - kwani sasa walichokuwa wanapigania kimebadilika?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wamekuelewa mkuu...
 
Hapo kwenye msisitizo - kwani sasa walichokuwa wanapigania kimebadilika?

Walitakiwa kukipigania hata kama ni kumwaga damu hawakutakwa kurejea nyuma.
 
Eboo nimekwambia sina chama wala sikuwa na chama,nilipenda na kukubali walichokuwa wakipigania CHADEMA.
Umeanzia kuisapoti kwenye UKUTA? Au ulikuwa mwanaCHADEMA tangu zamani?
 
Umehama chadema kama katika soka ulivyotuhama arsenal??

Hakuna namna ukiona jambo linakukera unasepa watu wanawaacha wanawake tena kwa viapo itakujakuwa chama !.
 
Walitakiwa kukipigania hata kama ni kumwaga damu hawakutakwa kurejea nyuma.
Sababu walizotoa kuahirisha nadhani zina mashiko lakini ishu ya mustakabali wa wale walio mahabusu ndio wanatakiwa washikie bango waachiwe.!
 
Hakuna namna ukiona jambo linakukera unasepa watu wanawaacha wanawake tena kwa viapo itakujakuwa chama !.
Kadi yao usisahau kurudisha.....oooh sorry umesema hukuwa mwanachama wao Bali uliwaunga tu mkono.!
 
Kina Mbowe wenyewe wanagombea kila uchaguzi kwa sababu wanaujua utamu wa maisha mazuri. Nani haogopi kufa?
 
Kamanda Ngongo hasira hasara.

Chama cha siasa ni mbinu. UKUTA umefanikiwa kwa 80%. Wote tumeona reaction ya serikali na vyombo vya dola; hii inaonyesha nguvu ya CHADEMA Tanzania. Hata hivyo operesheni UKUTA haijafutwa bali imesogezwa mbele kwa ushauri wa viongozi wa dini.
Aluta continua!
 
Kama unaona CHADEMA wamefanya kosa kuhahiirisha maandamano na Kama unaona yanafaida hakuna asiyependa faida wala CHADEMA hawajakukata miguu tarehe 1 ikifika komaa beba unachoona kinafaa ingia barabarani andamana mkuu.
 
Eboo nimekwambia sina chama wala sikuwa na chama,nilipenda na kukubali walichokuwa wakipigania CHADEMA.
chama chetu sikivu kimewasikia viongozi wetu wa dini natunawaheshimu si kama yule anaye omba kuombewa lakini ni mkaidi akiitwa na viongozi hao
 
Kaboa kweli lakin mi nampenda Tu Lowassa
 
Umeanzia kuisapoti kwenye UKUTA? Au ulikuwa mwanaCHADEMA tangu zamani?

Nimekwambia sina chama ila naunga mkono mambo ya maana yawe yamefanywa na chama chochote.Mfano niliunga mkono wazo la serekali ya CCM ya kufufua shirika letu la ndege,majuzi wameleta ndege mpya si mtumba toka Canada.Naunga mkono uhakiki wa wafanyakazi hewa,naunga mkono suala la kumaliza uhaba wa madawati,naunga mkono ujenzi wa reli Dar to Rwanda & Burundi lakini napinga ujenzi wa uwanja wa ndege CHATO,napinga matamshi ya Makonda wakati wa kuaga miili ya askari waliouwawa (ningekuwa mimi ni Rais ningetengua uteuzi wake mara moja)Nalaani matumizi mabovu ya jeshi la polisi hasa katika masuala ya kisiasa upooo ndugu yangu.
 
CDM wamefaniliwa sawa kwa sababu lengo la maandamano ni kutoa attention kwa watu ili wajue nini kitakwenda zungumzwa mwisho wa hayo maandamano sasa kwamuda wote huo cavarage waliyoipata ni zaidi ya hayo maandamano kwa kuwa walichotaka kukisema kimesemwa na kila kada kuanzia kijiji mpaka taifa kuna makundi yamefanya maandalizi ya vitendo hadharani namna ya kuzuia sasa ki kawaida ukiona unajiandaa sana maana yake unajua umahiri wa mpinzani wako
 
Huyu Anakwenda Kule Kwa Ng'Ombe Waliokatika Mikia Machungani Unadhani
Chadema Ni Chama Kidogo
Huko Chadema Kuna Viongozi Wenye Mbinu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…