Nimeamua kuachana na CHADEMA

Nimeamua kuachana na CHADEMA

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,186
Reaction score
37,496
Heshima kwenu wanajamvi,

Leo tarehe 31/08/2016 nimeamua kuachana na CHADEMA na kujishuhulisha na masuala ya michezo tu hasa mpira wa miguu.

Nilikuwa shabiki wa siasa bila kuunga mkono chama chochote cha siasa,kama mtanzania hata kama si mpenzi wa vyama bado nilikuwa na wajibu wa kuunga mkono jambo ninaloliona lina manufaaa kwa taifa.Tamko la viongozi wa CHADEMA la kututaka tuandamane nilikubaliana nalo kwa asilimia 100%, kwasababu madhumuni yake yalikuwa kupigania utawala wa sheria,kulinda uhuru wa kupasha habari,uhuru wa kusikia maoni kutoka vyama vyote si chama kimoja tu uku vingine vikizuiliwa hii ni hatari sana.

Viongozi wa CHADEMA walitangaza rasmi tarehe 01/09/2016 yangefanyika maandamano na mikutano nchi nzima.Makamanda walitumwa sehemu mbali mbali za jamhuri ya Tanganyika (Zanzibar ni nchi nyingine hainihusu) Ngongo na wapigania demokrasia hawakuhitaji kuhamasishwa na makamanda toka makao makuu tayari tulishafanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia kilometa kumi kila siku asubuhi ili kuuweka mwili katika hali ya utayari kukabilia na nginja nginja ya Polisi.

Tulishanunua mafuta (sina uhakika kama yangesaidia) kwaajili ya kuilinda ngozi dhidi ya maji ya washawasha,tulisha nunua miwani isiyopitisha hewa kwaajili ya kujilinda na mabomu ya machozi (sina hakika kama zingesaidia) kwa ujumla maandali yalikuwa yamefikia 95% ghafla bini vuuu Kamanda anahairisha maandamano ?

Hii haikubaliki nasema haikubaliki kabisaa lazima viongozi watambue wajibu wao katika kila matamko yao si unatamka leo hivi kesho unatenda vingine.

Mwezi mmoja aliotoa kamanda wetu Mbowe hauna maana makamanda wameswekwa rumanda, wanachama na wapenzi wamejiandaa vya kutosha hatuna uhakika na hizo siku 30.



Up date 1

Heshima kwenu wanajamvi,

Leo asubuhi nimepata simu kadhaa toka kwa viongozi wa vyama viwili CCM & CHADEMA sijui number yangu ya simu waliipata vipi nasema sijui (hili nawaachia wataalamu wa IT wanaweza kunijuza)

Viongozi wa CCM walikuwa wakifurahia uamuzi wangu wa kuachana na SIASA za vyama lakini wakanisihi sana nijiunge na chama chao kwasababu wameona ninaweza nika add value katika chama chao.Nikawauliza maswali kadhaa pengine majibu yake yangeweza kunishawishi kujiunga na chama hicho kikongwe kusini mwa jangwa la Sahara na bara la Afrika kwa ujumla wake.

a. CCM kama chama cha siasa kipo tayari kuacha demokrasia kuchukua mkondo wake
i,Kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa bila vikwazo.
ii,Kupinga hoja za vyama vya upinzani kwa hoja na si kutumia vyombo vya dola.
iii,Kurekebisha sheria za mitandao na kuhakikisha uhuru wa kupashana habari unalindwa.

b. CCM na viongozi wake kuhakikisha wanafuata sheria za nchi.
i,Kwakuwa KATIBA ndio sheria mama na Rais alipokabidhiwa madaraka yupo tayari kulinda.
ii,Serekali ya CCM kuhakikisha bunge linaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zake.
iii,Wale wote waliohusika kumshauri RAIS vibaya wanawajibika.

Majibu niliyopewa yalikuwa ya hovyo kabisa nikawaambia huko siji kamwe mtanisamehe sana siwezi kufanya kazi za Prof Lipumba ingawa mimi ni darasa la sita A lakini nina akili kuliko Prof wa uchumi.

Maongezi na viongozi wa CHADEMA ayalikuwa mazuri yenye ushawishi ni kwanini wamesitisha UKUTA.Sina hakika kama ni kweli lakini wamedai eti viongozi wa dini waliwasihi sana wasitishe maandamano (Nitalifanyia kazi mwenyewe nitakutana na viongozi wangu wa dini wanijuze kama ni kweli kazi ya kuhudumia kondo ni pana kiasi hicho).

Swali moja tu niliwauliza viongozi wa CHADEMA lakini nilikosa majibu yanayokidhi viwango vyangu vya ufikiri.

Mlipotangaza UKUTA tarehe 01/09/2016 Mlifahamu uzito wake au mlitangaza tu.Mlitarajia serekali ya JPM ingelala usingizi,mlitarajia mgeitwa IKULU kunywa juice au mlitarajia nini ?.Majibu niliyopewa yalikuwa mengi lakini yote hayakukidhi viwango vya kamati kuu (wanasiasa ambao wengine walishashika wadhifaa wa waziri mkuu....)

Bado uamuzi wangu wa kususa upo pale pale.Ingawa nimepenyezewa habari kwamba Mama wa Taifa (Mke wa Mwl Nyerere) alihusika kushawishi CHADEMA kusitisha maandamano sina hakika kama ni kweli ngoja nimwite mtoto wa Mwl Yericko Nyerere labda akithibitisha naweza kurejesha moyo na kuwasamehe viongozi wa CHADEMA dhambi ya kubadili gear angani.
 
Vuta pumzi mkuu , rudi nyuma na jitafakari , kuahirisha si kuacha au kushindwa , mimi binafsi nimepata hasara ya karibu hela ya madafu 2.7 mil kwa ajili ya maandalizi .
 
Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
 
Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
Leo jina lake sio Padre Slaa?
 
Kuna msemo heri lawama kuliko fedhea... Mbowe alishasoma fedhea inayokuja, imagine unaingia mtaani na watu kumi wanaokuunga mkono wengine wapo pembeni wanashangaa na kuchukua picha za kurusha insta na fb... Kiukweli Chadema ya leo sio Chadema ya Dr Slaa.. Kuna siku mtakuja kumkumbuka Slaa japo leo mnamtusi matusi yote ila kile kichwa kilishafanya calculations na kuona yote haya wakati nyie mnawaza kura za ulipo tupo.
Nakupinga vibaya sana , nadhani kuna kitu hukijui kuhusu chadema ndio maana umeingiza Dr Slaa ambaye hayupo wala hakushiriki UKUTA .
 
HAHAHAAHAHAHA,CHADEMA kama Lipumba,hawajui wanataka nini?hawana muongozo,hawapimi impacts za maamuzi yao,kiukweli kuwa mfuasi wa hawa watu ni hatari. Wamewaimbisha ukuta kwa mwezi sasa,at the end wanabadili gia angani,
 
Mkuu ka una uchungu na nia ya dhati siuandamane tu kwanini usubirie wengine. Ji sacrifice tu
 
HAHAHAAHAHAHA,CHADEMA kama Lipumba,hawajui wanataka nini?hawana muongozo,hawapimi impacts za maamuzi yao,kiukweli kuwa mfuasi wa hawa watu inabidi uwe na akili mfu/finyu.Wamewaimbisha ukuta kwa mwezi sasa,at the end wanabadili gia angani,
Kubadili gia angani ni sera rasmi ya CDM. Usiamini wanachosema hadi kifanyike kweli! !
 
..lengo la maandamano ni kufikisha ujumbe wa kupinga udikteta kwa wananchi.

..naamini ujumbe umefika pamoja na kwamba maandamano hayajafanyika.

..mikutano na maandamano yangefanyika bila shaka Polisi wangeingilia na kuumiza waandamanaji.

..uamuzi wa Kamati Kuu umewanyima Polisi nafasi ya kutekeleza uovu wao dhidi ya wanachama wa CDM.
 
Mbowe naona kafanya vizuri, na nadhani ni bora akajifunza namna nzuri ya kufanya siasa badala ya kutunishiana msuli na watu wenye kiburi kama Magufuli, ni bora wakawa wanatoa elimu kupitia media zao na mitandao kuliko hii staili ya maandamano, ambayo hayataungwa mkono kwa kuwa bado watanzania wengi ni waoga, na pia mzuka wao kwa magufuli haujapoa, wangesubiri angalau miaka miwili ipite kisha waanze kukinukisha kw mikutano kwa kuwa hata Magufuli wengi watakuwa wameshamchoka na maandamano yatapata wengi
Kuunga mkono CCM kisa CHADEMA wamefanya mis calculation ndogo nadhani ni wrong, sababu CCM wao hawana challenge yoyote bungeni , wala mawazo mapya ya kuikwamua Tanzania hapa ilipo, ni kupiga makofi tu bungeni bila kuhoji chochote
Chadema japo wanafanya error nyingi, wana afadhali kuliko CCM
ACT nilikuwa na matumaini nao lakini naona wamepoa sana, CUF ni chama cha wahafidhina tu hakina tofauti sana na CCM
 
Back
Top Bottom