Nimeamini wanaume ni wabinafsi

Nimeamini wanaume ni wabinafsi

Nimetoka kumaliza kesi na mpnz wangu ila roho imeniuma sina namna

Mpnz wangu ni wale watu ambao wanapenda sana kujua habari za ex nishaletaga mada hapa alivyoninunia kumsimulia juu ya ex

Kusema ukweli sijawah kumwambia ule ukweli kabisa kuhsu ex huwa namdanganya danganya

Basi bhn katika kukagua picha zangu kwenye simu yangu akakuta picha za ex wangu yeye hamjui… mimi huwa sina kawaida ya kufuta picha kiasi kwamba nina picha zaidi ya elfu 3 kwenye simu yangu na simu ni ya muda kidogo…

Ubaya kuna baadhi ya picha za ex zilikuwa hide kwa file nyingine ni picha sensitive sio za uchi sema ni zile ambazo zimepigwa marufuku kuonekana hivyo kipindi ananitumia alikuwa akisema niwe nazo makini so nikawa naziweka kwenye hidden file….

Sasa mpnz alipoziona hizo picha akaniuliza huyu ni nani nikasema ni rafiki yangu kumbe yeye tayari alishajua maana zilikuwa Picha kama 10 hivi na ubaya zaidi alikuta na zingine kwenye hidden file so akajua moja kwa moja namdanganya…

Akauliza anafanya kazi gani nikamdanganya kumbe tayari alijua kukazuka ugomvi mimi muongo ikabidi kuombana msamaha nikamweleza ukweli yakaisha


Kinachofanya niseme wanaume ni wabinafsi ni hili

Wakati anakagua simu yangu na yeye alinipa yake nikawa natazama alifutaa mauchafu yake ili nisione ila alisahau kwenye account zake za Facebook na Instagram

Wakuu niliingia messenger na DM yake aisee ni makubwa yaani mpnz wangu anakazi ya kutongoza wadada wa huko na kuwatumia namba zake wamtafutee… anawasifia wanawake sijui waremboo [emoji849][emoji849]

Sms ilioniuma alimwambia mdada amebadilika siku hzi sijui kammis waonane yule dada akamjibu kwamba kuna siku alimwita kusema kammiss kumbe alitaka alambee tu asepee [emoji1787]

Ukweli nimeumiaa ila sikumwambiaa kama nimeonaa upuuzi wake… daaaah


Wanaume acheni ubinafsiii

NB… mwanaume wangu nampendaaa sanaa hata kwa hili pia simuachii [emoji38]
Okey, sawa
 
IMG_2942.jpg
 
Tangu dunia iundwe, mwanamke ni mbinafsi kuliko kiumbe kingine chochote ulimwengu huu... Huyo ni vile tu mmefanana tabia
 
Back
Top Bottom