Nimeamini kuna watu wana akili ya ajabu

Nimeamini kuna watu wana akili ya ajabu

josephwaara

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2016
Posts
304
Reaction score
640
Inawezekana vipi mtu mwenye upeo mzuri wa kuwaza kusafirishwa kutoka mkoani kwa fedha zako, uuze mali zako au za mzazi wako, mkalundikwe chumba kimoja watu zaidi ya 20 huko Dar eti kwa ahadi ya kufanikiwa kibiashara.

Kweli kijana mzima wa miaka zaidi ya 24 unalipa milioni 5 hewani kwa mmiliki wa kampuni hewa na hujawahi kumwona na unaamini ipo siku utatoboa huku ukilala chooni?

Hili jambo limeniwazisha sana, wakuu nilifuatlia kipindi cha ripoti maalumu cha ITV ni mambo ya kustaajabisha mno.

Kipindi kipo youtube kwa jina la Ripoti maalumu!
 
Tema mate chini... Mshukuru Mungu hayakukuta..! Hakuna mjanja kwenye kupigwa kama maafisa wa serikali na nafasi na vipato vyao wanapigwa ... Usishangae mhitaji wa ajira kupigwa.. Na wajinga kamwe hawaishi
 
Jambo la kusikitisha ni kwamba wapo wengi sana vijana wa aina ile.

Andaa tu jambo lako ambalo limekaa kwa muonekano wa kupata matokeo kwa haraka utawapata wengi sana.

Watanzania wenye uwezo wa kuhoji jambo kiundani ni wachache sana.

Exposure hatuna, kusoma vitabu ili kuuelewa ulimwengu unaenda vipi pia hatutaki... Na tunajitia kujua kila kitu ilihali tupo watupu.

Safari ni ndefu sana.

Anyway, Duniani usipowahi unawahiwa.
 
Kwamba kwa wachache wale umehitimisha ni watanzania wengi mna low iq?
Hili liko ulimwenguni kote na wajinga hawataisha
Mkuu hizi discussions mbona zipo muda mrefu sana? Kuna nyingne tafiti kabisa ziliwahi kusema wengi wetu ni vichaa, nyingne zikasema hatuna furaha n.k, mimi nimeamua kuhamia upande tu km alivyofanya Haji Manara.
 
Mkuu nkisikiliza wale vijana wanavyojibu maswali ya mwandishi, kwanza napata aibu, pili napata hasira, tatu naishia kusikitika. Ni aibu kwa taifa, wasomi wale vijana!
Ile video inasikitisha na inauma sana mkuu basi tu. Ukombozi wa kifikra tunauhitaji sana Tanzania.
 
Hao vijana wa Q net,wengi ni wahitimu wa vyuo vikuu vya hapa Dar,wengi ni kutoka UDSM na DUCE.

Vijana hao wakishamaliza vyuo bas hujiunga na taasis hizi huku wakiamini watakuwa matajiri

Salamu zao ni "Habari Bilionea"
 
Nakubaliana na wewe.

Tumepigwa kwenye madini na wazungu.

Epa, Richmond, Escrow na matrilion ya jiwe, tulipigwa na waafrika wenzetu.

Sasa hivi mwarabu naye anatulia timing atupe za uso hapo ngorongoro.

Cha ajabu nini Q net wakiwachapa vijana?
 
Inawezekana vipi mtu mwenye upeo mzuri wa kuwaza kusafirishwa kutoka mkoani kwa fedha zako, uuze mali zako au za mzazi wako, mkalundikwe chumba kimoja watu zaidi ya 20 huko Dar eti kwa ahadi ya kufanikiwa kibiashara.

Kweli kijana mzima wa miaka zaidi ya 24 unalipa milioni 5 hewani kwa mmiliki wa kampuni hewa na hujawahi kumwona na unaamini ipo siku utatoboa huku ukilala chooni?

Hili jambo limeniwazisha sana, wakuu nilifuatlia kipindi cha ripoti maalumu cha ITV ni mambo ya kustaajabisha mno.

Kipindi kipo youtube kwa jina la Ripoti maalumu!
Sijui ni upumbavu au ni ujinga wa aina gani huu, au wakifika wanarogwa?
 
Inawezekana vipi mtu mwenye upeo mzuri wa kuwaza kusafirishwa kutoka mkoani kwa fedha zako, uuze mali zako au za mzazi wako, mkalundikwe chumba kimoja watu zaidi ya 20 huko Dar eti kwa ahadi ya kufanikiwa kibiashara.

Kweli kijana mzima wa miaka zaidi ya 24 unalipa milioni 5 hewani kwa mmiliki wa kampuni hewa na hujawahi kumwona na unaamini ipo siku utatoboa huku ukilala chooni?

Hili jambo limeniwazisha sana, wakuu nilifuatlia kipindi cha ripoti maalumu cha ITV ni mambo ya kustaajabisha mno.

Kipindi kipo youtube kwa jina la Ripoti maalumu!
Hapo waliopigwa hela ni wachache sana wengi wao ni kanyaboya ili kuwapumbaza wengine.Ila Kuna wengine hapo ni mwendo wa kuliwa mbususu kama hako kadogo kanaonekana kameliwa wiki nzima kwa mapigo ya kukunja
 
Back
Top Bottom