Nimeambiwa tutaishi South Sudan baada ya ndoa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,777
Habari za leo wapendwa,

Niliota na kuwaza siku nitakayosema 'I do', hayawi hayawi yamemkua, nimepata mchumba na ndoa ni baada ya Kwaresma. Tatizo ni kuwa huyu jamaa tumekutana Bongo akiwa anaishi Mbezi. Nilivyokuwa ninahesabu siku za kusogea kutoka huku kwetu Kwamtogole niende Mbezi.

Sasa bwana usiku wa jana, jamaa ananifahamisha kuwa amepata kazi South Sudan, ndoa ninaitamani lakini kwenda kuishi Sudan ni kitu ambacho sijawahi kukiwaza. Ninachance ya kughairi kabla sijasema 'I do'. Nikishakuwa mke sitakuwa na maamuzi tena.

Ushauri tafadhali.
 
Kama hukutusi wenzio wakati wa kampeni all the best, ila kama uliporomosha matusi hayatoki bure, we love u...we love ur marriage
 
Jua kwanza shughuli inayompeleka huko,neno kazi lina maana nyingi.

Shirikisha wazazi wajue kwanza mahari watakayopokea itawagharimu aje kwa wewe kupelekwa sudan
Ni mfanyakazi katika shirika ambalo lina ofisi Sudan. Nimekwisha kutana na wa-Sudan kadhaa pale ofisini kwao, kwakweli mbele yao mimi ni 'snow white' ingawa ndugu zangu huku Kwamtogole wananiita cheusi dawa.
 
Kwamtogole kunalipa vizuri. Sudan mwambie aende mwenyewe.

Habari za leo wapendwa,

Niliota na kuwaza siku nitakayosema 'I do', hayawi hayawi yamemkua, nimepata mchuma na ndoa ni baada ya Kwaresma. Tatizo ni kuwa huyu jamaa tumekutana Bongo akiwa anaishi Mbezi. Nilivyokuwa ninahesabu siku za kusogea kutoka huku kwetu Kwamtogole niende Mbezi.

Sasa bwana usiku wa jana, jamaa ananifahamisha kuwa amepata kazi South Sudan, ndoa ninaitamani lakini kwenda kuishi Sudan ni kitu ambacho sijawahi kukiwaza. Ninachance ya kughairi kabla sijasema 'I do'. Nikishakuwa mke sitakuwa na maamuzi tena. Ushauri tafadhali.
 
Njoo mie nikuoe maana naishi Masaki..
wp_ss_20170216_0048.png
wp_ss_20170216_0023.png
wp_ss_20170216_0035.png
 
mkuu mwenye jukumu la kuamua utaishi nae wapi ni mume,we nenda tu ni salama kabisa,si ni mke kwani tatizo liko wapi,punguza kuwa selective sana,huyo ndo chaguo lako
 
mkuu mwenye jukumu la kuamua utaishi nae wapi ni mume,we nenda tu ni salama kabisa,si ni mke kwani tatizo liko wapi,punguza kuwa selective sana,huyo ndo chaguo lako
Isije kuwa mnaniaga kwa buriani, maana story nilizopata kule wakifanya ride ni kijiji kizima kinachukuliwa.
 
Habari za leo wapendwa,

Niliota na kuwaza siku nitakayosema 'I do', hayawi hayawi yamemkua, nimepata mchuma na ndoa ni baada ya Kwaresma. Tatizo ni kuwa huyu jamaa tumekutana Bongo akiwa anaishi Mbezi. Nilivyokuwa ninahesabu siku za kusogea kutoka huku kwetu Kwamtogole niende Mbezi.

Sasa bwana usiku wa jana, jamaa ananifahamisha kuwa amepata kazi South Sudan, ndoa ninaitamani lakini kwenda kuishi Sudan ni kitu ambacho sijawahi kukiwaza. Ninachance ya kughairi kabla sijasema 'I do'. Nikishakuwa mke sitakuwa na maamuzi tena. Ushauri tafadhali.

Kwanza oaneni mengine baadae.
 
Isije kuwa mnaniaga kwa buriani, maana story nilizopata kule wakifanya ride ni kijiji kizima kinachukuliwa.
hahaha usiogope,after all mnaweza kimbilia north,mambo mengine huwa ni story tuu si unajua Sudani ilivyo kubwa ni kama congo,kila leo kinawaka ila kuna maeneo watu wanakula bata kama kawaida tuu hakuna complication,au ni sawa Tarime kwa hii bongo yetu
 
Hali ya usalama wa kule ndiyo tatizo na mimi nikiwa mgeni kwenye nchi ndani ya ndoa change.
Duuh! Fuatilia anaenda kwa kazi gani na kwa mda gani. Na mjulishe unavyojisikia kuhusu hiyo sehemu.
Sioni kama hiyo ni sababu ya kusitisha ndoa mkuu... Ni mambo ya kuongea tu na mwenzako.
 
Back
Top Bottom