Nimeambiwa ni Jinamizi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeambiwa ni Jinamizi!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Columbus, Oct 30, 2012.

 1. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna dhana kwamba ukiwa umelala usiku ukakajikuta umekabwa na kushindwa kabisa kujisogeza ni kutokana na jinamizi, hili jinamizi ni nini au kuna sababu za kiafya zinazosababisha hali hiyo? je kuna namna yoyote ya kujiepusha au kuna dawa ya kutibu hali hiyo isikutokee? msaada wetu tafadhali.
   
 2. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heart Failure mkuu hiyo. Hakuna jina mizi wala nini. Ukiona hivyo nenda hospital na utapata matibabu mazuri na kujikuta upo ok mkuu.
   
 3. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jinamizi, ni neno linalotumika kwa waginjwa au watu fulani kutaka kueleza jinsi anavyo "kabwa" wakati akilala usiku!!

  Neno la kiingereza huitwa Breathlessness na lile la kitaalamu huitwa "Paroxysmal Nocturnal Dyspnea" (PND)

  Hii hutokea pale kunapokuwa hakuna uwiano sawa kati ya damu inayozunguka mwili hasa itokayo na kwenda katika mapafu( Pulmonary Circulation) na Upumuaji wa hewa ya Oxygen..

  Mkandamizo/Shinikizo(Pressure/Tension) unapokuwa mkubwa katika uwiano huu hasa kwa watu wenye magonjwa mengine tayari mfano moyo, mapafu, ini, figo pia uzee, n.k husababisha damu kurudi katika mapafu badala ya kuendelea na mzunguko wake wa kawaida...na kwa vile mapafu hutumika kwa kupumulia(Breathing), maji au damu yanapokuwa yakijaa husababisha mtu kushindwa kupumua vizuri, na wagonjwa/watu wengi husema "NIMEKABWA NA JINI ila baada ya kufungua madirisha liliondoka"...
  Watu wengi husema hivyo kwa sababu mtu ukisimama mkandamizo ni mkubwa na hivyo kulazimisha kutoka katika mapafu kwenda katika moyo, na ile damu kidogo inayobaki due to gravity haileti madhara..lakini pale mtu anapolala tena, mzunguko ule ule hutokea na hivyo kufanya mtu kushindwa kulala, ..kutumia mito(pillows) husaidia katika hali hii, lakini ikumbukwe kwamba the more the pillows the worse the condition.

  MUHIMU: Hali hii PND, "Kukabwa na jinamizi" hutokea na dalili nyingine kama kuchoka haraka,(katika kupanda ngazi, kutembea mwendo mfupi), mapigo ya moyo kwenda kasi, kusikia kizunguzungu n.k ila watu wengi hupuuzia kwani huona ni jambo la kawaida hadi pale hali inapokuwa mbaya kwa kushindwa kulala na hivyo kwenda hospitali..

  Ushauri: Ni vema kuwahi HOSPITALI hali hii inapojitokeza.
   
 4. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  JF naendelea kuikubali siku hadi siku, imekuwa chanzo cha maarifa.Asante sana Mkuu!
   
 5. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  dawa yake lala na mfupa wa nguruwe hapo chini ya kitanda : anyway jinamizi si ilo hapo kwenye avatar yako?
   
 6. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kule kwetu Katavi enzi zile nakua ni kwamba ukiota unakabwa kusema ukweli wanadai kuwa unakuwa umewangiwa.So dawa pekee niliyoambiwa na babu yangu ni kwamba ukijinyosha ukagusa ukuta au ukagusa mtu ulielala nae hapo hapo hiyo hali inatoweka.And this is proved kwa sababu mimi ikinitokea nikiweza kunyosha mkono na kushika ukuta au kumshika nilielala nae basi kwisha habari ya jinamizi
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2016
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  Nimekabwa sasa hivi..
   
Loading...