Habari zenu wakuu
Mwanzoni mwa mwaka huu niliomba ushauri kuhusu mchumba wangu kukataliwa kupewa huduma alipoenda klinik nilipata majibu mazuri sana kutoka kwa watu mbali mbali waliopata nafasi ya kujibu. Sasa kwa kipindi cha miezi kazaa nimekua mtu wa mawazo sana baada ya huyo mchumba wangu kunambia mimba ilitoka ikiwa na week 13 tatizo ni aliniambia tiari ikiwa ni miezi Sita toka aliponiambia anamimba. Kwa kipindi chote nilikua naongea nae kila siku kwa simu au Skype na alikua ananitumia picha kuona mabadiliko ya mwili kama tumbo na nilikua na uhakika wa yeye kua na mimba kwa kipindi chote hicho cha miezi sita. Siku aliponiambia hana mimba na ilitoka ikiwa na miezi mitatu kweli mungu ndiye anajua tu lakini niliuzunika kupita maelezo. Kwa sasa bado kichwani nina maswali ingawa nilishamuuliza zaidi ya mara 1000 kweli alikua na mimba au alikua ananiongopea na kama kweli ilitoka ikiwa miezi mitatu na week moja kwa nini alisubilia kipindi chote hicho bira kunambia? Kwao najulikana na kwetu wanamjua na suala la kuanza familia tulikubaliana wote. Week tatu zijazo nitakua tena likizo nyumbani huko na nashindwa nini cha kufanya kuhusu huyu mchumba wangu. Ushauri wenu ni wa muhimu sana kwangu naomba mnishauri nini nifanye japo kwa kuanzia nikikutana nae tena.
Angalizo kwa wote ni story ya kweli iliyonitokea mimi